Rostam Aziz: Mjadala wa Bandari unajadiliwa kishabiki. Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana

Rostam Aziz: Mjadala wa Bandari unajadiliwa kishabiki. Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana

Mwekezaji ambaye Mkurugenzi wa Taifa Group, Rostam Azizi amesema kuwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi Nchi imekubaliana Serikali hisifanye biashara kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kuchochea maendeleo.

Amesema kwa upande wake hana tatizo na mjadala wa Bandari lakini katika kufuatilia mjadala huo anachukizwa mjadala huo kuwa wa kishabiki na kuibua udini na ubaguzi "Unamuona kiongozi mkubwa anaanza kuzungumza Uzanzibar na Utanganyika"

Amesisitiza kuwa mjadala huo umekuwa ukijadiliwa kishabiki sana huku akidai kuwa Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana.

Ameyasema hayo katika mjadala unaendelea Serena Hoteli leo Jumatatu, ambao umeandaliwa na taasisi ya Media Brains “Kulinda na Kuendeleza Umoja wa Kitaifa Wakati wa Mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi” (Protecting and Promoting National Cohesion in Times of Political and Economic Reforms).

Baadhi ya washiriki katika mjadala huo ambao wanatarajiwa kutoa maoni ni Katibu wa TEC, Padre Kitima, Jenerali Ulimwengu, Zitto Kabwe, Godbless Lema, Steven Wasira, Prof. Kitila Mkumbo

(Taarifa zaidi katika mjadala huu zitaenedelea kukujia).

View attachment 2662260
Huyo si ndiyo Wakala wa matapeli wa kimataifa wanaojiita wawekezaji,ata hiyo DPW Kuna mkono wale lazima.Na mind you huyu jamaa ni Wakala wa CIA East and Central Africa.
Umeichukua Kampuni ya Tigo,ghafla Bei za vifurushi zikaanza kwenda juu!
 
rostam ni fisadi papa apuuuzwe hana hoja yoyote ya msingi ya kusikilizwa

anaposema mtu anazungumzia uTanganyika na uzanzibar kwani si ndio kilichotokea?anadhani watu wanaongea kutokea wapi au alitaka wawe wanafiki wasiliseme hilo wakati ndio uhalisia wenyewe?

we rostam veepee
 
Mnyamwezi wa Igunga Tabora

Ndiyo mbunifu alieifanya serikali kuanzisha mfumo wa Bima ya Afya

Mwaka 1995 akiwa mbunge wa Igunga alianzisha mfumo wa Bima ya Afya, mkapa aka copy kwake na kuuingiza serikalini.

Wewe mzalendo umefanya nini kwa Tanzania?
Unaelewa maana ya ubunifu?.Kuna nchi zina sera ya boma ya afya toka miaka ya hatujapata uhuru.sasa miaka hiyo mkapa alikua rais wawapi ili rostam awe mbunifu?
 
Back
Top Bottom