Rostam Aziz mmiliki mpya wa tiGO Tanzania na Zantel

Rostam Aziz mmiliki mpya wa tiGO Tanzania na Zantel

Rostam Aziz na Kampuni ya Madagascar, Axian Group Ltd ni wamiliki wapya wa @Tigo_TZ baada ya kukamilika biashara ya mauziano na wamiliki wa awali Millicom International Cellular SA (NASDAQ-TIGO) na dili hilo limehusisha US$100M.

Katika taarifa ya Millicom International kwa umma. Hivyo, sasa Rostam anakuwa mwenyekiti wa Kampuni tanzu, MIC Tanzania.

Pia kwa pamoja na Axian Group Ltd wanamiliki kampuni ya Mawasiliano ya simu ya ZANTEL.

Imethibitishwa na CEO wa Millicom, Mauricio Ramos
Mmiliki mpya wa tigo za watanzania 😂😂😂😂
 
Tigo aka MIC group, Taifa gas, Primefuel, Caspian ltd, Hisa Mwadui diamond mine, Tancoal mine..... Mzee wa Caspian sea anachanja mbuga tu.....

Wanyonge tukomae tutoboe tuache kulialia....
 
Watanzania wooote kwa sasa wamekuwa wanasiasa, kutwa kucha kupambana na wanasiasa na mategemeo yao kwa 100% wameyaweka kwa wanasiasa....

Tanzania ni nchi iliyojaa fursa saana, tukomae tuache kulilia wanasiasa na kuamini matatizo yetu yanasababishwa na wanasiasa ilihali kuna jirani yako hapa hapa anamiliki 2bil kwenye account huku wewe unashangilia kuitwa mnyonge...

Tusitegemee saaana maendeleo huku Africa yaje leo, chanzo ni mifumo ya muda mrefo inayosababishwa na mambo meeengi ikiwemo athari zilizoachwa na wakoloni, siasa za kisasa za mabeberu, uchanga wa mataifa yetu, nk..
Kupambana na hizo athari kunahitaji kujitoa na vita ipiganwe vizazi na vizazi na sio Urais wa miaka 10 basi umasikini na unyonge uishe..
 
Tanzania ni nchi yenye ardhi kuubwa sana ambayo iko tupu kabisa na inarutuba, mito inayotiritika nk...

sasa hivi kila kijana, Mzee na watoto wote wanasiasa kutwa kuta kujadili siasa, Man U , Madrid nk....gharama za usajili wa hivyo vilabu, na taarifa zake zote...Ila sasa muulize huyo mtanzania bei ya mahindi alipo, au namna anaweza hata kulika mchicha tuta tatu...

Uvivu unatufanya tuamini hawa wanasiasa watakomboa maisha yetu....wakati unaishi Dar yenye wakazi zaidi ya 3mil na unashindwa kufikiri kupitia hii population unajikomboaje? au hapo mtaani kwenu kwenye wakazi 1000 wanawezaji kila siku kukupa tsh 100?
 
Sidhani kama kuna wakat utafika ambao watu wote tutakuwa kwenye uchumi wenye level sawa iwe Tz,Arabuni,Uropa au hata huko Asia. Na hata ikitokea hivyo dunia itajikuta ndani ya crisis kubwa sana.

Nachotaka kumaanisha hapa ni kwamba,watu wenye nafas ya kumiliki biashara kubwa kubwa km Rostam ni LAZIMA na MUHIMU kuwa nao. Kupitia wao,ajira nyingi zinatengenezeka na uchumi wa watu wengi kuchangamka kupitia ajira hzo. Pengine ni wajib wa serikal kutengeneza sera zitakazo waongoza hao matycoon ili wasigeuke wanyonyaji ktk mfumo wa biashara zao.

Nakumbuka enzi za Caspian kule Nyamongo,maisha yalichangamka sana iwe kwa vijana mtaani had kwa wakina mama wauza mboga na uji mitaani. Ugumu wa maisha ulianza pale mkuu alipoanza fitna kwa matycoon hao.

Hapa muhimu ni sera nzuri zenye muongozo safi ili tycoon apate ufanisi na faida yake pasipo kuumiza mfuko wa serikal wala kuwakamua sana wale wanaomfanyia kazi,na zihakikishe manufaa ya biashara yake yanaenea had kwa mwananchi mmoja mmjo mtaani basi.

Huko nyuma tuliaminishwa km matycoon ni mashetani wote huku tukijengewa fikra za kutembea tukijivunia kuwa fukara kwa kaulimbiu ya "wanyonge". Yaan serikal haifanyi biashara andthen ianze kuchukia wafanyabiashara😄😄😄😄 lilikuwa suala la mda tu uchumi ungebaki na upana wa mdomo wa chupa
 
Watanzania wooote kwa sasa wamekuwa wanasiasa, kutwa kucha kupambana na wanasiasa na mategemeo yao kwa 100% wameyaweka kwa wanasiasa....

Tanzania ni nchi iliyojaa fursa saana, tukomae tuache kulilia wanasiasa na kuamini matatizo yetu yanasababishwa na wanasiasa ilihali kuna jirani yako hapa hapa anamiliki 2bil kwenye account huku wewe unashangilia kuitwa mnyonge...

Tusitegemee saaana maendeleo huku Africa yaje leo, chanzo ni mifumo ya muda mrefo inayosababishwa na mambo meeengi ikiwemo athari zilizoachwa na wakoloni, siasa za kisasa za mabeberu, uchanga wa mataifa yetu, nk..
Kupambana na hizo athari kunahitaji kujitoa na vita ipiganwe vizazi na vizazi na sio Urais wa miaka 10 basi umasikini na unyonge uishe..
Elitwege anaomba ndugai na slaa waanzishe chama hahahaha

Ova
 
Kama Ni Kwenye Gari Unaambiwa Kaa Sawa Sawa Shikilia Vizuri Safari Imeanza Na Mwendo
 
Familia ya Rostam kama familia zingine za wenye asili ya Asia zimetajirika zamani hata kabla ya nchi kupata uhuru. Ni wafanya biashara wazuri. Wengi walikimbia Azimio la Arusha walihamia UK, Canada maana Nyerere alitaifisha biashara na mali zao baadaye zikamshinda. Kikwete enzi zile alienda Canada, US, UK kuwaomba warudi kama yule Museveni alivyowaomba WaAsia waliofukuzwa na Idi Amin warudi.
Unaijua vizuri familia ya Rostam ya Tabora au unaandika tu kiujumla jumla?!
Vipi na Wageni waliobaki wakawa wanateketeza Tembo wetu nao unawajua?!
 
Unaijua vizuri familia ya Rostam ya Tabora au unaandika tu kiujumla jumla?!

Pamoja na mambo yao yoote, hawa jamaa wanatabia ya kuendelea pale walipoishia wazee wao na kila kinachotafutwa ni kwa ajili ya Ukoo mzim, mmoja akitoboa basi wametoboa woote..

Ukiacha hayo yoote pia, wanalea watoto kuwa matajiri kwa kuwaelekeza kujisimamia, kusimamia, na kumanage business...hata wakienda shule wanasoma ili waje kufanya biashara sio kuajiliwa..
 
Kwan mgogoro wa Manji kumiliki tigo ulikwisha????

Back
Top Bottom