Rostam Aziz mmiliki mpya wa tiGO Tanzania na Zantel

Rostam Aziz mmiliki mpya wa tiGO Tanzania na Zantel

Tanzania ni nchi yenye ardhi kuubwa sana ambayo iko tupu kabisa na inarutuba, mito inayotiritika nk...

sasa hivi kila kijana, Mzee na watoto wote wanasiasa kutwa kuta kujadili siasa, Man U , Madrid nk....gharama za usajili wa hivyo vilabu, na taarifa zake zote...Ila sasa muulize huyo mtanzania bei ya mahindi alipo, au namna anaweza hata kulika mchicha tuta tatu...

Uvivu unatufanya tuamini hawa wanasiasa watakomboa maisha yetu....wakati unaishi Dar yenye wakazi zaidi ya 3mil na unashindwa kufikiri kupitia hii population unajikomboaje? au hapo mtaani kwenu kwenye wakazi 1000 wanawezaji kila siku kukupa tsh 100?
Natamani watanzania walio busy kudai Katiba na walalamikaji mitandaoni wakisikie na wakuelewe. Miaka mitatu iliyopita nikitumia likizo yangu vizuri nilienda Lindi, nikaona fursa ya ardhi nikafuatilia nikapata acre 120 kwa bei ndogo saaana. Nikajenga banda la mtunza shamba na kuanza kulisafisha. Hadi sasa acre 60 nimeshapanda mikorosho na ndani take nimepiga ufuta kwa msimu huu. Kwa picha za video nazotumiwa, kila kitu kinaenda poa. Tulio mbali tunaziona fursa lakini wenyeji kazi ni kulialia tu.

Hawa watu wenye asili ya Asia wanasoma fursa na wanaanzia mbali kupanga mambo yao na pia ni muendelezo wa generation after generation na hawaamini kwenye kuajiriwa hata kidogo. Tofauti na sisi, Mkurugenzi wa shirika anampa memo mwanae akaajiriwe kwa mshahara wa milioni kwa mwezi badala ya kumpa muongozo wa kujiajiri. Tutaendelea kulalamika hadi mwisho wa uhai wetu huku wachache wakiendelea kula keki.
 
Janja sana.... Vodacom walilegea wakaingia kwenye soko DSE, jamaa akaona hakuna tena biashara huko. Kaamia zake Tigo, na ule mpango wa kulazimisha hizi kampuni za simu kwenye DSE sidhani kama bado upo.
Kiherehere cha Voda tu, wengine waliona watulie maana haina faida kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zantel inamilikiawa na Tigo.

Na Rostam Share zake Voda ambayo ni kampuni kubwa Kuliko Tigo zilikuwa ni asilimia 30, kuna maajabu gani Akimiliki Tigo?

Na kwako Ushindani ni mgeni mmoja kama Millicom Toka Luxembourg amiliki Kampuni Tanzania lakini kampuni hio hio hapaswi kumiliki Mzawa?
Masikini na wapinzani wana roho mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom