Nakupinga kidogo hapo. Kuwa na pesa kunaweza kumpa mtu nguvu katika maeneo fulani, lakini pesa pekee si sawa na kuwa na power kwa kila kitu. Fedha ni tawi moja la nguvu, si chanzo pekee cha ushawishi.
Mtu anaweza kuwa na pesa nyingi, lakini akakosa mambo mengine yanayojenga power, kama mtandao na connections alizojenga kwa uaminifu na historia ya muda mrefu, nafasi ya kimkakati isiyotokana na fedha pekee, upatikanaji wa taarifa muhimu, uwezo wa kushawishi watu kupitia haiba na ushawishi binafsi, heshima na jina lililojengwa (reputation), uwezo wa kufikiri kimkakati (strategic thinking), n.k.
Kwa hiyo si kila mwenye pesa nyingi ana kiwango sawa cha power. Pesa inaweza kufungua milango, lakini namna mtu anavyotumia rasilimali zake, connections zake, taarifa na vingine ndiyo huamua ukubwa wa power wake.