Rostam Aziz ni powerful kiasi hicho kama anavyopambwa mitandaoni?

Ni kweli kwa asilimia mia Moja . connection yake nje ya nchi, kimataifa ni kubwa mno
1.Ana uwezo wa kuzuia jambo kimataifa lenye madhara na akasikilizwa na
Kiufup ni back up kubwa na ni msaada pia ndani na nje ya nchi .usipuuze
 
Mtu yoyote mwenye pesa ana nguvu. Rostam ana pesa nyingi mno
Nakupinga kidogo hapo. Kuwa na pesa kunaweza kumpa mtu nguvu katika maeneo fulani, lakini pesa pekee si sawa na kuwa na power kwa kila kitu. Fedha ni tawi moja la nguvu, si chanzo pekee cha ushawishi.


Mtu anaweza kuwa na pesa nyingi, lakini akakosa mambo mengine yanayojenga power, kama mtandao na connections alizojenga kwa uaminifu na historia ya muda mrefu, nafasi ya kimkakati isiyotokana na fedha pekee, upatikanaji wa taarifa muhimu, uwezo wa kushawishi watu kupitia haiba na ushawishi binafsi, heshima na jina lililojengwa (reputation), uwezo wa kufikiri kimkakati (strategic thinking), n.k.


Kwa hiyo si kila mwenye pesa nyingi ana kiwango sawa cha power. Pesa inaweza kufungua milango, lakini namna mtu anavyotumia rasilimali zake, connections zake, taarifa na vingine ndiyo huamua ukubwa wa power wake.
 
Umetumwa wewe
 
Connections na influence zinakuja na pesa mkuu. Mtu mwenye pesa asipokuwa na influence au connections, ni yeye tu hajataka.
 
Connections na influence zinakuja na pesa mkuu. Mtu mwenye pesa asipokuwa na influence au connections, ni yeye tu hajataka.
Kuna baadhi ya connections zinahitaji zaidi ya pesa.

pesa ni kigezo mojawapo lakini levels za hio mitandao hujengwa zaidi na uaminifu, historia, loyalty, n.k. huwezi kuzinunua tu kwa kumtuma house boy apeleke gunia la pesa.
 
Mkuu duniani kote matajiri ndio wanaongoza dunia, hao maraisi ni bendera tu na mara zote matajri ndio huamua nani awe raisi nani asiwe raisi, hata kule duniani pamoja na Trump kuwa raisi mwenye ukwasi mkubwa lakini amewekwa pale na matajiri kama Elon Musk, wao wanachojali ni interest zao na si wananchi, huomchezo kwa sasa ndio umeanza kutumiwa na lile bonge nyanya la Zimbabwe kwa viongozi wa Africa,japa hilo bonge nyanya nalo ni kuwadi tu nyuma yake ni matajiri wa kizungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…