Mkuu Kasheshe,
I hope credibility yako inapanda sana kwa kumtetea Rostam, ambaye alipoitwa bungeni na kamati ya Mwakyembe, hakujibu kabisa, lakini alipooonekana alidai kuwa alikuwa safari, sasa baada ya kurudi safari kilichomzuia ni nini kwenda mbele ya kamati?
Mimi sina tatizo na utetezi wako kwa sababu wote hatuwezi kuwa on one side, lakini ukileta maneno ya credibility ambayo so far hakuna aliyeuliza ya kwako kwa kumtetea huyu proven fisadi, then inaleta maswali ya nini hasa nia yako? Kwamba usiulizwe au what?
Unawezaje kumsafisha kiongozi Fisadi aliyemfunga, Rage jela bila sababu ya msingi ili kumsaidia mtandao mwenziwe Kapuya, sasa utamsafishaje huyu? Unapoona mpaka Rais wa Jamhuri ameshindwa kumbeba hata hawara wa rafiki yake mpenzi kwenye uwaziri ujue huyo hasafishiki, ukiona hata rafiki yake mpenzi anamtosa kutoka kwenye uweka hazina wa CCM, ujue huyo ni mchafu period na hasafishiki, ukiona anahangaika majumbani mwa wabunge wanaotaka afikishwe kwenye sheria ujue kuna kitu anakijua kuwa hakiko sawa na tabia zake, kwa sababu asingekuwa mchafu basi angesubiri tu kwenda mahakamani, Rostam ni fisadi ndio maana majuzi amehamisha kampuni zake za Richimonduli na Dowans kwa Manji, ukiona kiongozi wa taifa kama yeye anahangaika mpaka kununua Ze-Comedy ili kuwapunguza makali ya kutoa ufisadi, basi ni huyu ananuka sana uchafu wa ufisadi,
Siku zinaanza kufikia ukingoni ndio maana sasa anahaha kila kona mara kanisani, mara manyumbani kwa wabunge anafikiri kila mbunge ni kama Serukamba? Asubiri tu siku ya siku inakuja tena karibuni sana, kumtetea ni haki yako ndio hasa demokrasia, lakini it has nothing to na credibility yako, unless unataka kusema kuwa kwetu wananchi kudai responsibility kutoka kwa kiongozi wa taifa inahusiana na credibility ya wananchi nafiri hiyo hoja ni foolish na pathetic, ni haki yangu kama mwananchi kutaka kujua iwapo huyu fisadi atachukuliwa hatua za kisheria, kama ni credibility you can have it,
Lakini huwezi kuzuia haki yangu mkuu ya kuuliza maswali genuine kama vile ni kwa nini baada ya kushutumiwa na ufisadi sasa anahamisha kampuni zinashutumiwa kwa Manji, lakini hakuhamisha Vodacom ambayo inajulikana kuwa anamiliki majority share kihalali?
Mkuu Kasheshe, ukijiheshimu utaheshimiwa bro, sitaki kuamini kuwa credibility yako ina anything to do na utetezi wako wa fisadi wa taifa letu namba moja yaani Rostam! Lakini bado ninakuheshimu sana, ila huyu Rostam hasafishiki ndio maana hata Rais wa Jamhuri aliamua amtose kwenye uweka hazina wa CCM, na pia kumtosa hawara yake aliyekuwa waziri.
Lakini ni haki yako kumtetea ndio maana demokrasia, Ahsante Mkuu!