Tigo na Vodacom watakua wanavunja sheria kwa kuwa na umiliki wa wageni kwa asilimia 100
SOURCE: http://www.tcra.go.tz/regulation/THE%20COMMUNICATIONS%20LICENSING%20REGULATIONS%202005.pdf
USHIRIKIANO NI JAMBO LA MAANA!
Nyie mfanye kazi yenu huko Tanzania na mimi hapa USA nitafanya yangu!
Na nimeshasema kabla hajaja hapa WASHINGTON...AFANYE KAZI ZA WANANCHI!
Tusileteane madaharau kabisa kwani na sisi tunapambana..Hii issue si ya kupambana huko Bongo peke yake!
Naomba mungu sana, nasi tupate Bob Woodward na Carl Bernstein wa Tanzania. Maanake TZ hatuna kabisa majournalist.
Sasa Muungwana akija huko anahitajika ajibu maswali mengi tu... na makosa aliyofanya Bush, pale G8 ni kutangaza urafiki wake na JK.
Hilo linafanya media ya US, kumchambua JK..which,ni kizuri kwetu,kwa sababu media ya huko itaanza kuchimba mengi tu...tungojee hiyo agosti.
Na wenzetu wa JF mlioko huko US mngeanza kuto info kwa hayo media za huko.
Habari za uhakikia kabisa ni kwamba Rostam Aziz ameanza kuhamishia mali zake nje ya nchi, sababu anahofia mambo yanavyokwenda serikalini kwa sasa. Kwa ushahidi tayari ameweka rehani hisa zake zote 35pc za Vodacom Afrika Kusini. Kabla ya kuhamishia hisa zake, alikua amenunua hisa za Planetel za mwenzake Peter Noni na mkewe, naye alifanya hivyo kuhofia mambo yanavyokwenda ofisini kwake BoT. Rostam alichukua hisa zote 35pc za Watanzania kupitia kampuni zake za Caspian na Mirambo. Nimethibitisha kwa macho yangu mwenyewe nikiwa bongo kwamba Chenge akiwa Waziri wa miundombinu alimsaidia kwa nguvu zake zote Rostam kufanikisha mkakati wake huo wa kuhamisha hisa zake nje kwa kisingizio cha kuweka rehani. Kuna watu serikalini walipinga (na wanaendelea kupinga) lakini jamaa aliwazidi kete kwa kusadiwa na Chenge na sasa inaelekea amefanikiwa kwa kiasi. Zaidi nitawaletea maana naharakisha kurejea majuu. Nitamwachia Invisible mambo yote ili siku mwafaka amwage hadharani
Ndio nasema hilo haliwezekani Ni kazi ya serikali kutengeneza mazingira mwafaka kwa sekta binafsi na wafanyabiashara kufanya biashara zao na wakati huohuo kuhakikisha kwamba inaziba mianya yoyote, kwa njia ya sheria, kanuni, n.k., ya kuliingiza hasara taifa na kupoteza mapato halali kwa njia ya kodi. Inavyoonekana ni kama vile tulitaka Rostam asitumie mianya iliyokuwepo na ambayo ipo ya kumfanya apate faida haraka na kubwa, I bet hili haliwezekani kwa mfanyabiashara yeyote, simply because hiyo sio kazi yake!
CCM walipoamua kuwakumbatia wafanyabiashara waliamua pia kukumbatia utapeli na ujanjaujanja wa wafanyabiashara kama akina Rostam. Rostam anasema wazazi wake walianza biashara tangu 1852, sasa cha kujiuliza ni kwa nini yeye amejulikana kuanzia kipindi cha wakati wa Mwinyi na kushamirisha biashara zake kipindi cha kampeni za urais wa 2005? Ni kwamba huko nyuma hapakuwa na loop holes za kijinga kama zilivyo sasa.
Tuache kuwa simplistic because simplicity is the enemy of truth. Hatuwezi kuishinda vita ya ufisadi kwa kuwashambulia mawakala wa ufisadi; ifike mahala tuamue ama kuwashambulia wazalisha ufisadi CCM au kama, hatuwawezi, tukae kimya na tukubaliane kwamba hayo ndiyo maisha yetu!
NAMWAMBIA TENA KAMA HAWEZI URAIS AJIUZULU MARA MOJA!
LA SIVYO WASHINGTON ASIRUKE!
kwi Kwi Kwi
Kazi Kweli Kweli, Watanzania Kwa Ukali Wa Maneno Tu Hawajambo, ... Vitendo Thubutu!
Kila La Heri Ndugu Yangu Jmushi, Nitakufahamisha Lini Anakuja Huko Washington!
Hii habari ya Vodacom ni muhimu sana na ukweli wa mambo ni Rostam hizo 35% sio zote zake, na yeye ana partners kwenye hiyo ownership ambao walikuwa vigogo wa juu mno wenye vingora.
Originally Posted by moelex23 View Post
Hii habari ya Vodacom ni muhimu sana na ukweli wa mambo ni Rostam hizo 35% sio zote zake, na yeye ana partners kwenye hiyo ownership ambao walikuwa vigogo wa juu mno wenye vingora.
``
Wandugu hawa waarabu walikuwa wakifanya nini miaka hyo?huenda hao wazee wake walikuwa ma-ajenti wa ukoloni.