Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Wano tajwa ni mafisadi...wana wa jua wenzao!!.......si wao peke yao ....wapo wenzao wanao onekana sio mafisadi...lakini ni mafisadi...

CCM ni chama cha madalali...
 
Sitegemei jipya lolote toka kwa RA, alichokipanga ni kuiponda kamati ya Mwakyembe na kumsafisha Lowasa. Naungana na maelezo ya Mwanakijiji aliyoyatoa wiki iliyopita. Mpango wa Agenda 21 group ni kujisafisha. RA anatumiwa na akina Karamagi na Lowasa.

Bunge lisipokuwa makini litayumbishwa hapa, kwani inawezekana nyuma ya RA yupo Mkuu wa Kaya.
 
Sitegemei jipya lolote toka kwa RA, alichokipanga ni kuiponda kamati ya Mwakyembe na kumsafisha Lowasa. Naungana na maelezo ya Mwanakijiji aliyoyatoa wiki iliyopita. Mpango wa Agenda 21 group ni kujisafisha. RA anatumiwa na akina Karamagi na Lowasa.

Bunge lisipokuwa makini litayumbishwa hapa, kwani inawezekana nyuma ya RA yupo Mkuu wa Kaya.

Yani kikwete kwa timing!!! HE IS ALWAYS OUT OF THE COUNTRY OR 'DOING SOMETHING VERY IMPORTANT'...WAKATI BUNGE LIKIWAKA MOTO!!
machoni mwangu kuna kitu.................
 
taratibu gigo utaingia pabaya ccm si chama cha madalali.

ukiibiwa na mtanzania usiseme watanzania wote wizi.


usihukumu chama kwa kosa la mwanachama
 
bring it on RA......bring it....and don't you ever think kuna wajinga hapa........

....this time pamoja na pesa zako....lakini ukakutana na watu smart......ukauvaa mkenge
 
bring it on RA......bring it....and don't you ever think kuna wajinga hapa........

....this time pamoja na pesa zako....lakini ukakutana na watu smart......ukauvaa mkenge

I hope that, Wabunge don't sell your power at cheap price, wakazieni hao mafisadi. Vita ya ufisadi sasa inapamba moto. Hivi kwanini RA, Lowasa, Karamagi, Msabaha, Gire na wote waliohusika na Richmond wasipelekwe kortini? ona sasa wanapata nguvu...
 
Nafikiri itakuwa busara hata kusikia kutoka kwenye kinywa chake. Maana misikendo aliyonayo siyo mchezo tunaweza taja mpaka asubuhi kila shughuli mbaya itokeayo tanzania yumo.

Inatakiwa angalau nayeye aseme kulikoni kila skendo ni yeye, Kagoda yumo, Kilimo tumo, Umeme yumo,.............

Mimi nafikiri katika uchangiaji wa hoja atakayo toa itabidi ziunganishwe skendo zote katika kufikia conclussion otherwise tutakuwa hatumtendea haki.

Nafikiri ikiwa hivi anaweza kutoka Bungeni mpaka mahakama kuu kama siyo segerea.
 
Speaker anafanya makosa makubwa mno, Rostam ni mtuhumiwa chochote anachotaka kusema apewe nafasi ili wabunge na wananchi wachambue.

Rostam akiremove hoja yake atakuwa amepiga bao la mwaka, maana uko mbeleni ukimwita fisadi atasema no nilipeleka ushaidi bungeni wakanikatalia kuutoa.

Let him say anything, then wabunge wamjibu ili haki ichukue mkondo wake.

PR ya speaker ni mbovu mno
 
Speaker anafanya makosa makubwa mno, Rostam ni mtuhumiwa chochote anachotaka kusema apewe nafasi ili wabunge na wananchi wachambue.

Rostam akiremove hoja yake atakuwa amepiga bao la mwaka, maana uko mbeleni ukimwita fisadi atasema no nilipeleka ushaidi bungeni wakanikatalia kuutoa.

Let him say anything, then wabunge wamjibu ili haki ichukue mkondo wake.

PR ya speaker ni mbovu mno


nadhani kuna la zaidi lililomfanya 6 ashtuke, je RA kamtaja 'bwana mkubwa' kwamba anahusika kwenye dili?
 
nadhani kuna la zaidi lililomfanya 6 ashtuke, je RA kamtaja 'bwana mkubwa' kwamba anahusika kwenye dili?

Inawezekana kuna ukweli hapa, bwana mkubwa anaweza kuguswa, hila pamoja na hayo kuna taharifa alitoa mwanakijiji kuwa huyu bwana ana ripoti tofauti na ya mwakyembe. Sijui ameandika mwenyewe?

Lakini suala la kujichomoa halipo maana lazima RA ajieleze kwa wabunge na siyo suala la six kwa sababu iliamuliwa kikao kilicho pita.

Labda cha kujiuliza ni kuwa six hivi alitegemea RA akaangwe peke yake? Lazima afe na wengine tu. Hapa sisi yetu macho yalipangwa gizani(mkataba ulisainiwa usiku) lakini yataanza kutoka mchana kweupe.
 
nadhani kuna la zaidi lililomfanya 6 ashtuke, je RA kamtaja 'bwana mkubwa' kwamba anahusika kwenye dili?

RA hana ubavu wa kumtaja Mkuu wa kaya. Alichokiwasilisha itakuwa ni mapanga kwa Kamati ya Mwakyembe hivyo Bunge zima kuhusishwa kwamba lilimuonea EL.
 
RA hana ubavu wa kumtaja Mkuu wa kaya. Alichokiwasilisha itakuwa ni mapanga kwa Kamati ya Mwakyembe hivyo Bunge zima kuhusishwa kwamba lilimuonea EL.


RA ni mfa maji na anadhani watanzania bado tumelala, amechelewa sana, sio enzi hizi. Anachotakiwa kufanya ni kubwaga manyanga kama mwenzie EL then awajibishwe kisheria kama malipo ya kufanya ufisadi. Amefaidi vya kutosha P.A.Y.E yetu.
 
Speaker anafanya makosa makubwa mno, Rostam ni mtuhumiwa chochote anachotaka kusema apewe nafasi ili wabunge na wananchi wachambue.

Rostam akiremove hoja yake atakuwa amepiga bao la mwaka, maana uko mbeleni ukimwita fisadi atasema no nilipeleka ushaidi bungeni wakanikatalia kuutoa.

Let him say anything, then wabunge wamjibu ili haki ichukue mkondo wake.

PR ya speaker ni mbovu mno

Bunge ndo Mahakama siku hizi!! Judge ndo Sitta au?? Naona Rostam kawa Mwanasheria siku hizi..Where is the tanzanian legal system??..yani wamekuwa sidelined mpaka haibu!!
Judiciary mnatuabisha...yani hadi serikali (through pinda) wana uhahika mafisadi watashinda wakienda court!!


Nchi yetu ni UOZZO!!
 
Yaani akija na point ya kuiponda kamati haitamsaidia. Kama aliona kamati haifain kwa nini hakusema ilipoundwa.Anasubiri mpaka amehusishwa ndo aje kusema ni kazi bure.

Jamani nisaidieni.Hivi Waziri mkuu anapoitisha kikao cha CCM anatumia kofia ipi? Anaitisha kikao cha CCM kama Waziri mkuu,Mbunge, Kada au Mwanachama wa CCM? Na katiba yao inaimba vipi kuhusu hivyo vikao.
 
Hii kitu ati ze endi ovu ze dei lazima immalize 6, ujanjaujanja una mwisho wake na wataanguka kwa uzito wao wenyewe. Ngoja tusubiri!
 
Yaani akija na point ya kuiponda kamati haitamsaidia. Kama aliona kamati haifain kwa nini hakusema ilipoundwa.Anasubiri mpaka amehusishwa ndo aje kusema ni kazi bure.

Jamani nisaidieni.Hivi Waziri mkuu anapoitisha kikao cha CCM anatumia kofia ipi? Anaitisha kikao cha CCM kama Waziri mkuu,Mbunge, Kada au Mwanachama wa CCM? Na katiba yao inaimba vipi kuhusu hivyo vikao.


Kama kada kiongozi wa makada wa CCM bungeni!
 
Nauliza..hivi 6 ana nini?maana kila hoja nzito yeye ndio huwa anakimbia alitaka kukikmbiaa kwenda usa..sababu aliogopa ripoti mwakyembe..sasa anaogopa maelezo ya RA..anaogopa nini??si ndio demokrasia ya bunge?hivi kuepa ukweli ndio busara siku hizi?asije mtu akamnyooshea kidole RA akichomoa hoja yake bungeni...
kuponda kamati haitamsaidia sana ingawa twajua kuwa wamejipanga sana kujitetea na kumsafisha EL..hatukubali mwaka huu..kama noma na iwe noma..haka ikimtaja mkuun wa kaya poa watu waitishe uchaguzi mwingine kwani lazima?si wapo wengine wenye uwezo kama wao kuongioza kwani nini bwana .......tumechoka kabisa mi nimepata hasira..juu hili..wanatuzingua tu hawa ina maana kweli richmund haina mwenyewe.........????????pesa walikuwa wanalipa kwenda account gani??nani alieileta hiyo kampuni ?msitufanye wote hatuna upeo hapaa....mnageuza geuza mambo...kama vipi...itisheni uchaguzi mwingine.................mna tu boree......
 
ukiibiwa na mtanzania usiseme watanzania wote wizi.

usihukumu chama kwa kosa la mwanachama

Kuna wakati inaweza kutokea ukaibiwa na Mtanzania na ukasema Watanzania wote ni wezi. Hiyo utokea iwapo mwizi huyo (Mtanzania) anatetewa na Watanzania wote kuwa si mwizi, na wakawa tayari kumficha asipelekwe mahakamani.

Na Watanzania hao hao wakaamua kutumia "siasa za majitaka" kusema wewe uliyeibiwa unamzushia huyo mwizi!

Ni Tanzania pekee unaweza kukutana na vitimbi hivi!!
 
Sitegemei jipya lolote toka kwa RA, alichokipanga ni kuiponda kamati ya Mwakyembe na kumsafisha Lowasa. Naungana na maelezo ya Mwanakijiji aliyoyatoa wiki iliyopita. Mpango wa Agenda 21 group ni kujisafisha. RA anatumiwa na akina Karamagi na Lowasa.

Bunge lisipokuwa makini litayumbishwa hapa, kwani inawezekana nyuma ya RA yupo Mkuu wa Kaya.

Kwanini Sitta ameogopa RA asijielezee mpaka aandike kwanza kile anachotaka kukisema MJENGONI? Sitta anaogopa nini? Sumthing fish here jamani! Mbona wale wengine hawakuandika waliyoyasema siku ile?sikumbuki kama kina Lowassa waliandika na kumpelekea Sitta kisha ndio wakasema.

Pengine...........

Sitta anaogopa Rostam angetoa ufafanuzi kama ifuatavyo:-

"Mheshimiwa spika kama unavyojua mfanya biashara yoyote lazma atengeneze faida.. na kutokana na pesa zangu nyingi kuzitumia nilishauriwa na best wangu EDO nianzishe Richmond na Richard mtoto wa Lowassa awe mmoja wa wanahisa, ili kurudisha change yangu niliyogharamia kwenye uchaguzi.

Mhe spika wote tunakumbuka zile pesa nilizochukua pale BoT hazikuvuka lengo kutokana na extension ya uchaguzi uliosababishwa na kifo cha mgombea mwenza wa Chadema ndio washkaji JK na Lowassa wakashauri nitoe mshiko wangu then mtukishika madaraka nitarudishiwa changu"

Wanagonga meza!

"Mhe spika kwa kuwa mimi ni creative sana ndipo nilibuni hii Richmond na best wangu akaja na mvua ya wa Thailand na bado tulikuwa na project nyingine za kurudisha chetu maana ahsante zenu mie kama mfanya biashara haziwezi kunisaidia"

Wanagonga Meza!

"Mhe Spika usijifanye umesahau pesa nilizokupa na vifaa vya kuhongonga jimboni kwako, usidhani zile fulana, kofia, khanga na posters ziliprintiwa na mawe mijihela ilinitoka mkubwa na ndio maana niliamua kuja na hili swala la Richmond"

Wanagonga Meza tena safari hii mpaka spika mwenyewe anagonga meza!!!!

"Ahsanteni kwa kunisikiliza naomba kuwasilisha."

Wanagonga meza!!!!!


Hii ndio Sitta anayoiogopa wasije kuwekwa uchi maana akiwasilisha maelezo lazma aseme yale aliyowasilisha la sivyo atazimiwa kipaza sauti!

teh teh teh teh teh wanaogopana wenyewe kwa wenyewe.

Kete imekula KING.
 
Rostam azua kizaazaa
Maelezo yake yaficha siri nzito



na Happiness Katabazi



MAELEZO binafsi ya maandishi ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz yanayolenga kutoa utetezi kuhusu kuhusishwa kwake katika sakata la mkataba wa kufua umeme wa dharura kati ya Kampuni ya Richmond na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), yanaonekana kuwashtua Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka Dodoma zinaeleza kuwa, Rostam aliwasilisha maelezo yake binafsi kwa Spika juzi jioni majira ya saa 12:30, saa chache baada ya kupewa maelekezo yaliyokuwa yakimtaka afanye hivyo, siku moja kabla hajapewa fursa ya kujibu Azimio la Bunge.

Hata hivyo pamoja na kukidhi maelekezo hayo ya kikanuni, Rostam alishindwa kutoa maelezo yake hayo binafsi bungeni jana kutokana na sababu ambazo hadi hivi sasa gazeti hili halijaweza kuzithibitisha.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya Bunge zinaeleza kuwa, maelezo hayo ya Rostam yanaonekana dhahiri kubeba ujumbe unaoweza kusababisha kutokea kwa mtikisiko mwingine ndani ya Bunge, baada ya ule wa Richmond ambao ulisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari hizo, uzito wa maelezo hayo ya Rostam ambayo kwa kiwango kikubwa yanaonekana kukilemea chama tawala, ulisababisha mapema jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alazimike kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi ya CCM muda mfupi baada ya Bunge kuahirishwa jana mchana.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Rostam kuhusu maelezo yake binafsi jana, mbunge huyo hakuwa tayari kueleza lolote kwa undani zaidi ya kumtaka mwandishi kuwasiliana na ofisi za Bunge kwani yeye alikuwa ameshatekeleza maelekezo ya Spika.

“Nadhani mimi sina lolote la kusema la zaidi. Ninachoweza kukwambia ndugu yangu ni kwamba, niliwasilisha maelezo yangu ya maandishi kwa Spika jana jioni (Jumatano). Nasubiri kupangiwa muda wa kuyasema ndani ya Bunge kama nilivyoelekezwa katika mkutano uliopita wa Bunge. Watafuteni wahusika,” alisema Rostam huku akikataa kutoa maelezo mengine yoyote ya ziada.

Tanzania Daima ilipowasiliana kwa simu na Spika Sitta jana mchana, alikiri kupokea maelezo ya mbunge huyo kwa maandishi juzi majira ya saa 12:00 jioni na akasema tayari alikuwa ameshaanza kuyafanyia kazi.

Alisema baada ya kukabidhiwa maelezo hayo, jana asubuhi aliyapeleka kwa washauri wake ambao ni maofisa wa Bunge ili waweze kuyachambua kitaalam na kisha kumpatia ushauri unaofaa, kabla ya kumruhusu Rostam kuwasilisha utetezi wake huo.

“Mimi ni Spika, nina washauri wangu, hivyo nimewakabidhi maelezo (ya Rostam) ili wayachambue kitaalam na wakimaliza watakuja kunishauri, na ushauri huo ndiyo utakaoniruhusu nimpangie tarehe ya kuwasilisha maelezo yake bungeni au la,” alisema Spika Sitta.

Alipotakiwa kueleza iwapo kikao cha Kamati ya Uongozi cha CCM kilichoitishwa jana kinahusu maelezo hayo ya Rostam, Sitta alisema aliyekiitisha ni Waziri Mkuu na si yeye.

Pamoja na kukiri kuwa katika kikao hicho cha Kamati ya Uongozi ya CCM kilichoketi jana hiyo, suala hilo la Rostam lilikuwa moja ya mambo yaliyojadiliwa, Spika alisema kililenga kuzungumzia ajenda mbalimbali ambazo zimeibuka ndani ya Bunge hilo katika siku za karibuni.

Alipotakiwa kueleza nini kilikuwa kimejiri ndani ya kikao hicho kuhusu hatima ya maelezo binafsi ya Rostam, alisema yeye binafsi alishindwa kuhudhuria kwa kuwa, wakati kikifanyika alikuwa na ugeni wa Balozi wa Uingereza hapa nchini, aliyekwenda ofisini kwake kumuaga.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kwamba, hoja ya Rostam ilijadiliwa kwa zaidi ya saa moja, na kwamba baadhi ya wajumbe walifikia hatua ya kumtaka aiondoe, pendekezo ambalo hadi jana jioni mbunge huyo alikuwa amelikataa.

Mbunge mmoja wa CCM aliyezungumza na gazeti hili jana jioni ambaye alikiri kuyaona maelezo hayo binafsi ya Rostam, anasema kikubwa kinacholeta wasiwasi ni nini kinachoweza kutokea iwapo mbunge huyo wa Igunga ataruhusiwa kutoa utetezi wake bungeni.

“Mambo yamekuwa mazito, wakubwa wamejadili hoja hii kwa zaidi ya saa nzima. Tumeambiwa kuwa wamemtaka ayaondoe maelezo yake yanayoeleza mambo mengi mapya kuhusu Kamati Teule ya Richmond iliyoongozwa na Dk. (Harrison) Mwakyembe. Mimi nimeyasoma maelezo hayo ya Rostam, tunasubiri tuone nini kitatokea ingawa naamini ni mambo mazito,” alisema mbunge huyo.

Alisema, katika maelezo yake hayo, Rostam anatarajia kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu namna Kamati ya Mwakyembe ilivyofanya kazi, kujiuzulu kwa Lowassa na mawaziri wengine wawili, na namna yeye mwenyewe alivyohusishwa katika sakata hilo.

Hali hii imefikia hapo baada ya juzi, Sitta kumzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake binafsi bungeni akimtaka kwanza atimize masharti ya kanuni za Bunge yanayomtaka kuwasilisha kwake (Spika) hoja yake kabla hajaitoa bungeni.

“Nilimwambia haiwezekani akawasilishe maelezo yake kabla hajawasilisha kwa Spika kwa maandishi na nimemwelekeza arudi akayaandike maelezo yake, kisha ayawasilishe kwangu, angalau siku moja kabla, ndipo nitamruhusu asimame bungeni na kutoa maelezo yake.

“Baada ya kumwelekeza hivyo, Rostam alinielewa na akaniaidi kwamba atafanya kama nilivyomwelekeza, hivyo akileta kesho (jana Alhamisi) maelezo yake, basi kesho kutwa (leo) nitamruhusu ayatoe,” alisema Sitta alipozungumza na gazeti hili juzi.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Na.50 (1), mbunge yeyote anaweza kwa idhini ya Spika, kutoa maelezo binafsi bungeni yanayolenga kufafanua kuhusu jambo lolote linalomhusu na lililoifikia jamii.

Hata hivyo kanuni hiyo ya 50 (2) inaonyesha dhahiri kutoa unafuu kwa mbunge mwenye maelezo binafsi, ambayo akishayatoa katika muda usiozidi dakika 15, basi hakutakuwa na mjadala kuhusu jambo hilo.

Uamuzi wa Rostam kutoa maelezo yake binafsi unatokana na Azimio la Bunge lililofikiwa baada ya ombi lililotolewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wenye utata wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond, iliyoingia na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alilazimika kutoa hoja ya kulitaka Bunge lidai maelezo binafsi kutoka kwa Rostam, baada ya mbunge huyo wa Igunga, ambaye jina lake lilitajwa katika ripoti ya kamati teule ya Bunge likimhusisha na mkataba huo wenye utata wa Richmond, kuipinga ripoti ya kamati teule.

Rostam katika mchango wake wa kujadili ripoti hiyo ya kamati teule, alikanusha kuhusika katika na kampuni hiyo, na akaeleza wasiwasi wake kwamba, kamati hiyo iliendelea kufanya kazi nje ya muda wake ambao ulimalizika Desemba 31, mwaka jana.

 
Back
Top Bottom