Rostam: Tuungane kukomesha vitendo vya kishetani katika nchi yetu. Poleni CHADEMA

msisahau aliyefariki ni muislamu na pia muarabu, vinginevyo rostamu asingeongea chochote kile na ndiyo maana msiba unaonekana kugusa wengi angekuwa mgalatia wangebakia wenyewe tu na kejeli juu, some are more equal than others, RIP hata hivyo …
Kwani chadema ni waislamu? Manake msiba ni wa chadema huu
 
Hivi wakati waislamu na mashehe wanatekwa, kufungwa jela, kusingiziwa ugaidi na hata kuuwawa hawa chadema na wanaharakati uchwara walikua wapi?
Watu wa tanga kuweni makini sana na wanasiasa ni waongo na wanafiki
Watawatumia sasa hivi kwa kuwa wana maslahi, yakiisha hamuwaoni

NB
Siungi mkono yaliyotokea na nalaani kwa nguvu zote

Bringing udini kwenye huu msiba is the lowest one can go.
 
Naona rais wetu, rais wetu nyingi tu kwenye huo ujumbe...ni ujumbe wenye nia ya kuwahadaa wenye vichwa vyepesi kwamba rais kweli ana nia ya dhati kutokomeza haya matukio ....hawa ndiyo wafadhili wenyewe wa magenge ya CCM ndani ya usalama yanayotoa uhai wa watanganyika wasio na hatio
Ccm ina wanachama aina tatu, Ccm Intarahamwe, ccm Nyangumi, Ccm mafisadi Papa.

Lini Rostam aziz akawa na uchungu na watanzania hata atoe pole za aina hii?

Tunaomjua RA hapo ni ulaghai anafanya taarifa yake imemtaja rais Zaidi ya mara tatu.
Kuliko almaharum Ally kibao
 
TAARIFA YA ROSTAM AZIZI KUFUATIA MAUAJI YA KIONGOZI WA KISIASA
View attachment 3091613
Katika siku za karibuni nchi yetu imeshuhudia kujirudia tena kwa matukio ya kikatili ambayo yamehusisha kuripotiwa kwa vitendo vya utekaji, utesaji na jana tukashuhudia tukio baya zaidi la mauaji ya kiongozi wa Chadema, Ndugu Mohamed Ali Kibao.

Naungana na Watanzania wema wote kutoa mkono wa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na viongozi na wanachama wa Chadema kwa msiba huo wenye kuhuzunisha sana.

Nimetiwa moyo sana na taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo alieleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kutoa pole kwa wafiwa na wakati huo huo kuagiza uchunguzi wa haraka wa tukio hilo na mengine kama hayo. Mheshimiwa Rais hakuishia hapo tu bali alitoa ujumbe mzito kwa kusema kuwa: "Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii."

Namuunga mkono Rais wetu ambaye kwa nafasi yake ndiye Mfariji Mkuu wa Taifa (Comforter-in-Chief) kwa kujitokeza na kuwafariji wafiwa na Watanzania na kuwatangazia hatua za mara moja ambazo amezichukua ili kukomesha ukatili huu.

Rais wetu siku zote ametuthibitishia kwa maneno na vitendo kuwa kamwe hakubaliani na matendo ya aina yoyote ya kuumizana ama kutotenda haki. Amejipambanua kuwa ni muumini thabiti wa haki kamili za kila binadamu.

Nikiwa raia wa Tanzania ambaye nimeitumikia nchi yetu katika nafasi mbali mbali za uongozi na ambaye nililelewa katika Taifa linalothamini tunu za utu na thamani ya ubinadamu wetu chini ya misingi ya uhuru na haki, nawaomba Watanzania wenzangu sote tuungane kukataa kurudishwa kwenye zama za giza ambapo utu na maisha ya mtu vilionekana havina thamani.

Naomba sote tuungane na Rais wetu kuhakikisha vitendo vya kishetani vya aina hii vinakomeshwa na havirejei tena katika nchi yetu. Sote tusimame pamoja kuona taifa letu linarudi katika misingi yake ya utu, uhuru na haki iliyojengwa na waasisi wake.

Rostam Azizi
9/9/2024
View attachment 3091604
Na waliofanya vitendo vya utekaji na wanaowatuma ni mashetani hawatakiwi kuheshimiwa. Wao ni kulaaniwa hata kizazi cha tano
 
msisahau aliyefariki ni muislamu na pia muarabu, vinginevyo rostamu asingeongea chochote kile na ndiyo maana msiba unaonekana kugusa wengi angekuwa mgalatia wangebakia wenyewe tu na kejeli juu, some are more equal than others, RIP hata hivyo …
Udini uko ndani yako unakutafuna.
Hivi hukuwahi kusikia kuwa Salim Turky ndiye aliyefadhili safari ya matibabu ya Tundu Lisu kwenda Nairobi?
Turky ni wa dini gani?
Au Tundu Lissu naye ni mwarabu na mwislam?

Huu udini unaopenda kushabikia unakupa faida gani ?
 
TAARIFA YA ROSTAM AZIZI KUFUATIA MAUAJI YA KIONGOZI WA KISIASA
View attachment 3091613
Katika siku za karibuni nchi yetu imeshuhudia kujirudia tena kwa matukio ya kikatili ambayo yamehusisha kuripotiwa kwa vitendo vya utekaji, utesaji na jana tukashuhudia tukio baya zaidi la mauaji ya kiongozi wa Chadema, Ndugu Mohamed Ali Kibao.

Naungana na Watanzania wema wote kutoa mkono wa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na viongozi na wanachama wa Chadema kwa msiba huo wenye kuhuzunisha sana.

Nimetiwa moyo sana na taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo alieleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kutoa pole kwa wafiwa na wakati huo huo kuagiza uchunguzi wa haraka wa tukio hilo na mengine kama hayo. Mheshimiwa Rais hakuishia hapo tu bali alitoa ujumbe mzito kwa kusema kuwa: "Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii."

Namuunga mkono Rais wetu ambaye kwa nafasi yake ndiye Mfariji Mkuu wa Taifa (Comforter-in-Chief) kwa kujitokeza na kuwafariji wafiwa na Watanzania na kuwatangazia hatua za mara moja ambazo amezichukua ili kukomesha ukatili huu.

Rais wetu siku zote ametuthibitishia kwa maneno na vitendo kuwa kamwe hakubaliani na matendo ya aina yoyote ya kuumizana ama kutotenda haki. Amejipambanua kuwa ni muumini thabiti wa haki kamili za kila binadamu.

Nikiwa raia wa Tanzania ambaye nimeitumikia nchi yetu katika nafasi mbali mbali za uongozi na ambaye nililelewa katika Taifa linalothamini tunu za utu na thamani ya ubinadamu wetu chini ya misingi ya uhuru na haki, nawaomba Watanzania wenzangu sote tuungane kukataa kurudishwa kwenye zama za giza ambapo utu na maisha ya mtu vilionekana havina thamani.

Naomba sote tuungane na Rais wetu kuhakikisha vitendo vya kishetani vya aina hii vinakomeshwa na havirejei tena katika nchi yetu. Sote tusimame pamoja kuona taifa letu linarudi katika misingi yake ya utu, uhuru na haki iliyojengwa na waasisi wake.

Rostam Azizi
9/9/2024
View attachment 3091604
Taarifa muhimu sana hii ila...
P
 
Hivi wakati waislamu na mashehe wanatekwa, kufungwa jela, kusingiziwa ugaidi na hata kuuwawa hawa chadema na wanaharakati uchwara walikua wapi?
Watu wa tanga kuweni makini sana na wanasiasa ni waongo na wanafiki
Watawatumia sasa hivi kwa kuwa wana maslahi, yakiisha hamuwaoni

NB
Siungi mkono yaliyotokea na nalaani kwa nguvu zote
Kwa hiyo wewe watu kutekwa ovyo na kuawa unaona ni tatizo la kidini?
 
Watakuwa wametishwa. Na kama wababe walihusika ndio balaa kabisa. Tusiwaonee bure wenye basi

Pamoja na kelele zote hizi bado hawataki kusema chochote? Hata pole? Nini kibaya zaidi kitawatokea kama kuna mtu kapoteza uhai? Sidhani kuna kutishwa hapo huku ni kuwa insensitive na kutaka kampuni yao ipite under the radar.
 
Back
Top Bottom