Rostam: Tuungane kukomesha vitendo vya kishetani katika nchi yetu. Poleni CHADEMA

Rostam mjanja sana, mara nyingi kwenye haya majanga ya kitaifa huwa anaingilia kati kumkingia kifua Samia.

Remember DPW, huyu Rostam kuna dili kubwa kalicheza kwa Samia sasa ndio analipa fadhila.
 
TAARIFA YA ROSTAM AZIZI KUFUATIA MAUAJI YA KIONGOZI WA KISIASA
View attachment 3091613
Katika siku za karibuni nchi yetu imeshuhudia kujirudia tena kwa matukio ya kikatili ambayo yamehusisha kuripotiwa kwa vitendo vya utekaji, utesaji na jana tukashuhudia tukio baya zaidi la mauaji ya kiongozi wa Chadema, Ndugu Mohamed Ali Kibao.

Naungana na Watanzania wema wote kutoa mkono wa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na viongozi na wanachama wa Chadema kwa msiba huo wenye kuhuzunisha sana.

Nimetiwa moyo sana na taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo alieleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kutoa pole kwa wafiwa na wakati huo huo kuagiza uchunguzi wa haraka wa tukio hilo na mengine kama hayo. Mheshimiwa Rais hakuishia hapo tu bali alitoa ujumbe mzito kwa kusema kuwa: "Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii."

Namuunga mkono Rais wetu ambaye kwa nafasi yake ndiye Mfariji Mkuu wa Taifa (Comforter-in-Chief) kwa kujitokeza na kuwafariji wafiwa na Watanzania na kuwatangazia hatua za mara moja ambazo amezichukua ili kukomesha ukatili huu.

Rais wetu siku zote ametuthibitishia kwa maneno na vitendo kuwa kamwe hakubaliani na matendo ya aina yoyote ya kuumizana ama kutotenda haki. Amejipambanua kuwa ni muumini thabiti wa haki kamili za kila binadamu.

Nikiwa raia wa Tanzania ambaye nimeitumikia nchi yetu katika nafasi mbali mbali za uongozi na ambaye nililelewa katika Taifa linalothamini tunu za utu na thamani ya ubinadamu wetu chini ya misingi ya uhuru na haki, nawaomba Watanzania wenzangu sote tuungane kukataa kurudishwa kwenye zama za giza ambapo utu na maisha ya mtu vilionekana havina thamani.

Naomba sote tuungane na Rais wetu kuhakikisha vitendo vya kishetani vya aina hii vinakomeshwa na havirejei tena katika nchi yetu. Sote tusimame pamoja kuona taifa letu linarudi katika misingi yake ya utu, uhuru na haki iliyojengwa na waasisi wake.

Rostam Azizi
9/9/2024
View attachment 3091604
Muuaji ni yule yule wa enzi za awamu ya 5 ila TISS wanaogopa kumuambia Rais kwa vile ni kijana pendwa
 
Ccm ina wanachama aina tatu, Ccm Intarahamwe, ccm Nyangumi, Ccm mafisadi Papa.

Lini Rostam aziz akawa na uchungu na watanzania hata atoe pole za aina hii?

Tunaomjua RA hapo ni ulaghai anafanya taarifa yake imemtaja rais Zaidi ya mara tatu.
Kuliko almaharum Ally kibao
Hata jambazi ana mke na huchimbiwa mkwala na mke
 
TAARIFA YA ROSTAM AZIZI KUFUATIA MAUAJI YA KIONGOZI WA KISIASA
View attachment 3091613
Katika siku za karibuni nchi yetu imeshuhudia kujirudia tena kwa matukio ya kikatili ambayo yamehusisha kuripotiwa kwa vitendo vya utekaji, utesaji na jana tukashuhudia tukio baya zaidi la mauaji ya kiongozi wa Chadema, Ndugu Mohamed Ali Kibao.

Naungana na Watanzania wema wote kutoa mkono wa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na viongozi na wanachama wa Chadema kwa msiba huo wenye kuhuzunisha sana.

Nimetiwa moyo sana na taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo alieleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kutoa pole kwa wafiwa na wakati huo huo kuagiza uchunguzi wa haraka wa tukio hilo na mengine kama hayo. Mheshimiwa Rais hakuishia hapo tu bali alitoa ujumbe mzito kwa kusema kuwa: "Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii."

Namuunga mkono Rais wetu ambaye kwa nafasi yake ndiye Mfariji Mkuu wa Taifa (Comforter-in-Chief) kwa kujitokeza na kuwafariji wafiwa na Watanzania na kuwatangazia hatua za mara moja ambazo amezichukua ili kukomesha ukatili huu.

Rais wetu siku zote ametuthibitishia kwa maneno na vitendo kuwa kamwe hakubaliani na matendo ya aina yoyote ya kuumizana ama kutotenda haki. Amejipambanua kuwa ni muumini thabiti wa haki kamili za kila binadamu.

Nikiwa raia wa Tanzania ambaye nimeitumikia nchi yetu katika nafasi mbali mbali za uongozi na ambaye nililelewa katika Taifa linalothamini tunu za utu na thamani ya ubinadamu wetu chini ya misingi ya uhuru na haki, nawaomba Watanzania wenzangu sote tuungane kukataa kurudishwa kwenye zama za giza ambapo utu na maisha ya mtu vilionekana havina thamani.

Naomba sote tuungane na Rais wetu kuhakikisha vitendo vya kishetani vya aina hii vinakomeshwa na havirejei tena katika nchi yetu. Sote tusimame pamoja kuona taifa letu linarudi katika misingi yake ya utu, uhuru na haki iliyojengwa na waasisi wake.

Rostam Azizi
9/9/2024
View attachment 3091604
Nchi hii imejaa miuaji ndani ua CCM
 
George orwell , the animal farm. Ama kweli kila masika na mbu wake. Twende kwetu mbezi bichi kule upepo unapovuma.
 
msisahau aliyefariki ni muislamu na pia muarabu, vinginevyo rostamu asingeongea chochote kile na ndiyo maana msiba unaonekana kugusa wengi angekuwa mgalatia wangebakia wenyewe tu na kejeli juu, some are more equal than others, RIP hata hivyo …
Kama Alivyofanya Shekhe Mwaipopo
 
Hivi wakati waislamu na mashehe wanatekwa, kufungwa jela, kusingiziwa ugaidi na hata kuuwawa hawa chadema na wanaharakati uchwara walikua wapi?
Watu wa tanga kuweni makini sana na wanasiasa ni waongo na wanafiki
Watawatumia sasa hivi kwa kuwa wana maslahi, yakiisha hamuwaoni

NB
Siungi mkono yaliyotokea na nalaani kwa nguvu zote
Ni chadema tu na Mh. Tundu Lisu walioongelea mashehe wa uamsho.
 
Back
Top Bottom