Rostam: Tuungane kukomesha vitendo vya kishetani katika nchi yetu. Poleni CHADEMA

Rostam: Tuungane kukomesha vitendo vya kishetani katika nchi yetu. Poleni CHADEMA

TAARIFA YA ROSTAM AZIZI KUFUATIA MAUAJI YA KIONGOZI WA KISIASA
View attachment 3091613
Katika siku za karibuni nchi yetu imeshuhudia kujirudia tena kwa matukio ya kikatili ambayo yamehusisha kuripotiwa kwa vitendo vya utekaji, utesaji na jana tukashuhudia tukio baya zaidi la mauaji ya kiongozi wa Chadema, Ndugu Mohamed Ali Kibao.

Naungana na Watanzania wema wote kutoa mkono wa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na viongozi na wanachama wa Chadema kwa msiba huo wenye kuhuzunisha sana.

Nimetiwa moyo sana na taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo alieleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kutoa pole kwa wafiwa na wakati huo huo kuagiza uchunguzi wa haraka wa tukio hilo na mengine kama hayo. Mheshimiwa Rais hakuishia hapo tu bali alitoa ujumbe mzito kwa kusema kuwa: "Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii."

Namuunga mkono Rais wetu ambaye kwa nafasi yake ndiye Mfariji Mkuu wa Taifa (Comforter-in-Chief) kwa kujitokeza na kuwafariji wafiwa na Watanzania na kuwatangazia hatua za mara moja ambazo amezichukua ili kukomesha ukatili huu.

Rais wetu siku zote ametuthibitishia kwa maneno na vitendo kuwa kamwe hakubaliani na matendo ya aina yoyote ya kuumizana ama kutotenda haki. Amejipambanua kuwa ni muumini thabiti wa haki kamili za kila binadamu.

Nikiwa raia wa Tanzania ambaye nimeitumikia nchi yetu katika nafasi mbali mbali za uongozi na ambaye nililelewa katika Taifa linalothamini tunu za utu na thamani ya ubinadamu wetu chini ya misingi ya uhuru na haki, nawaomba Watanzania wenzangu sote tuungane kukataa kurudishwa kwenye zama za giza ambapo utu na maisha ya mtu vilionekana havina thamani.

Naomba sote tuungane na Rais wetu kuhakikisha vitendo vya kishetani vya aina hii vinakomeshwa na havirejei tena katika nchi yetu. Sote tusimame pamoja kuona taifa letu linarudi katika misingi yake ya utu, uhuru na haki iliyojengwa na waasisi wake.

Rostam Azizi
9/9/2024
View attachment 3091604
Hongera Rostam Aziz kwa kauli thabiti .

Kwenye hili la kupoteza uhai wa watu kwaajili ya kulinda au kutafuta madaraka au kwa nia nyingine yoyote ni ushetani mkubwa, ni uharamia ambao hautakiwi kupata kivuli cha kujificha.

Hawa watekaji na wauaji, kama Taifa tusimame pamoja, na kuwaona kuwa ni maadui wa Taifa. Kwa kuanzia Mafwele na kundi lake wakamatwe haraka, waeleze walikokowaweka watu wote waliowateka.

Huo uovu ukilindwa na kuuacha uendelee, bila ya kujali upo CCM au CHADEMA, unaweza kuuawa wakati wowote. Hawa wauaji wanatengeneza himaya yao, wakijijenga wanaweza kuwaua hata viongozi wa nchi wakapokonya madaraka. Maana kwao kupata au kifanikisha chochote wanachokitaka, ni kwa kuua. Waliokitengeneza hicho kikosi cha mauaji kinachoitwa Task Force wasidhani wao wapo salama.
 
Hivi wakati waislamu na mashehe wanatekwa, kufungwa jela, kusingiziwa ugaidi na hata kuuwawa hawa chadema na wanaharakati uchwara walikua wapi?
Watu wa tanga kuweni makini sana na wanasiasa ni waongo na wanafiki
Watawatumia sasa hivi kwa kuwa wana maslahi, yakiisha hamuwaoni

NB
Siungi mkono yaliyotokea na nalaani kwa nguvu zote
Ndugu yangu umekosa uungwana au umekosa kumbukumbu au siyo mfuatiliaji.

Hivi unakumbuka ni mara ngapi Lisu aliongelea suala la mashekhe kuwekwa kizuizini? Mbona Lisu alipinga mara nyingi na kusema kuwa kama hao mashekhe wana makosa kwa nini hawafikishwi mahakamani?
 
Pamoja na kelele zote hizi bado hawataki kusema chochote? Hata pole? Nini kibaya zaidi kitawatokea kama kuna mtu kapoteza uhai? Sidhani kuna kutishwa hapo huku ni kuwa insensitive na kutaka kampuni yao ipite under the radar.

Hawa ni wafanaya biashara. katika mazingira yenye uonevu, biashara yao inaweza kupewa misukosuko sana. Ndio maana wanakaa kimya. Ingawa, nchi hii, kama wameamua kupata wahusika, hata siku moja haitapita
 
Ndugu yangu umekosa uungwana au umekosa kumbukumbu au siyo mfuatiliaji.

Hivi unakumbuka ni mara ngapi Lisu aliongelea suala la mashekhe kuwekwa kizuizini? Mbona Lisu alipinga mara nyingi na kusema kuwa kama hao mashekhe wana makosa kwa nini hawafikishwi mahakamani?

Kuna watu wengine huwezxi kuwaelimisha. Wamepata Ilmi, ambayo inazidi elimu kwa kiasi kikubwa sana🤣🤣🤣🤣🤣
 
Walishatoa toa tamko.

Hakuna biashara ina thamani kuliko uhai wa mtu. Kila mtu anajua wao hawahusiki kwenye hili unaweza toa pole na upande wako wa story kutoa sintofahamu kwenye jamii. Eventually wametoa na wametoa zaidi kuliko hata nilivyotarajia hadi jina la mtu wanayemshuku wamemtaja wakati kesi ipo under investigation.
 
Kukamata wahalifu ni kazi ya polisi. Wamesharipoti. Sio kazi yao kupeleleza au kukamata waliohusika. Mengine haya ni uongo na nuonezi au yana chembe chembe za kutaka biashara ya mtu iathirike
 
Kukamata wahalifu ni kazi ya polisi. Wamesharipoti. Sio kazi yao kupeleleza au kukamata waliohusika. Mengine haya ni uongo na nuonezi au yana chembe chembe za kutaka biashara ya mtu iathirike

I have no idea what you're talking about.

Mimi niliuliza wametoa tamko kwa umma which they did eventually. Sijauliza ushahidi, tamko kwa polisi or anything.
 
Ndugu yangu umekosa uungwana au umekosa kumbukumbu au siyo mfuatiliaji.

Hivi unakumbuka ni mara ngapi Lisu aliongelea suala la mashekhe kuwekwa kizuizini? Mbona Lisu alipinga mara nyingi na kusema kuwa kama hao mashekhe wana makosa kwa nini hawafikishwi mahakamani?
Sio kuongea bwashee, ni mishe mishe kama zile za jana, wamewahi kufanya?ukiondoa jana?
Kuna watu wengine huwezxi kuwaelimisha. Wamepata Ilmi, ambayo inazidi elimu kwa kiasi kikubwa sana🤣🤣🤣🤣🤣
Umeona sasa elmu akhera ilivyofanya kazi jana? Hao waliosoma hiyo elimu dunia wamefanya nini zaidi ya kugeuza binocular? 😇😇😇🤣🤣🤣🤣🤣,
Wapeni inchi waislamu muone ukombozi utakavyokuja fasta,

Hata uhuru wa Tanganyika ulichangiwa pakubwa na Tanga
 
Back
Top Bottom