Tatizo sio CCM Wala Chadema au hyo katiba mpya unayoitaka, kumbuka unatakiwa kuwa na familia Bora ili wanaowasije kuwa watu wakulalamika lalamika kila wakati.
Amka acha ujinga fanya kazi kwa juhudi tafuta hela na ukishapata pesa utakuja kugundua kuwa kumbe Kuna mtaji mkubwa Sana kwenye nchi hii nao Ni watu wasiojitambua wanataka Nini sio wengine Bali Ni vijana waliowengi wakitanzania.
Tafuta pesa uipate, ili upate pesa au uishi maisha mazuri na familia yako na wanaokuzunguka hayaitaji katiba mpya Wala usaidizi wa CCM au chadema Bali n kujituma katika kutafuta pesa.
Ukipata pesa haya Mambo ya makato ya simu hutayaona makubwa Bali utaona n nafasi nyingine ya kupata zaidi kwa namna moja au nyingine. (Uamue usitumie simu kwa malipo ubaki na benki tuu au utumie simu kwa kunufaika wewe na wateja wako.)