RPC Kinondoni aliyemwambia Mbowe hachomoki ndiye alimwambia Lema hashindi Arusha

RPC Kinondoni aliyemwambia Mbowe hachomoki ndiye alimwambia Lema hashindi Arusha

Nchi zingine zinalinda watu wao kwetu tupo busy kuwapunguza ili kuendelea kutawala mbaya sana...Katiba mpya ni muhimu mno mno...
 
Kumbe huyu RPC ambaye alimtolea maneno mabaya Mbowe kuwa "this time huchomoki tutakupiga na kesi ya ugaidi(kwa maneno ya John Mrema) "vile vile aliwahi kumwambia Lema akiwa RCO Arusha kuwa hatashinda uchaguzi kwa sababu yeye ni Kada. Maneno haya aliyasema ndugu Godbless Lema mbunge mstaafu Arusha mjini kupitia kipindi cha mtandaoni cha Maria Space.

Hili ndio jeshi letu la polisi, kiongozi wake anafanya kazi kwa kusukumwa na siasa kuumiza wengine makusudi. Jeshi linaendeshwa kwa misukumo ya kisiasa tuseme kuwa Tanzania tunailinda upendo na mshikamano wetu? Hawa si ndio polisi wavuruga amani?

IGP Simon Siro hili ndio jeshi lako linalofanya kazi na kujawa kibri kufikia hatua hii. Si ajabu hii taarifa iliyosomwa na jeshi la polisi ilikua na maneno ya huyu RPC.

Ni dhambi kubwa sana kumtuhumu mtu kesi nzito kiasi hicho ikiwa hajawahi hata kutishia mtu mabati.

Itakuwa ni a aibu sana kwa Jeshi la Polisi siku akigundulika hana hatia maana kesi yoyote ile ni ushahidi.
Na ndiye alimtuma afande Jumanne kwenda kupandikiza pembe za ndovu shambani kwa yule Mzee wa Arusha waliyempora milioni tisini
 
Mnalia lia sana hao police hawakai mbinguni wana familia zao na ndugu zao tafuteni namna za kuwapa maumivu
Hapana ndugu. Hawa ni watanzania na hatuwezi kuishi kwa kulipiza kisasi. Labda nao wanafuata amri tu pasipokujua. Utawala unaofuata sheria ukija nao watafuata sheria. Kumbuka nao wanateseka kwa njia moja ama nyingine. tuwasaidia na kuwapenda.
 
Upendo kwenye chuki na uonevu?? Ilikuwa enzi za mitume na manabii
 
Back
Top Bottom