RPC Muroto atoa onyo kwa BAWACHA, asema wanaotaka kuandamana watakipata wanachokitafuta wakasimulie wenzao huko Geita

RPC Muroto atoa onyo kwa BAWACHA, asema wanaotaka kuandamana watakipata wanachokitafuta wakasimulie wenzao huko Geita

Polisi wa Bongo ni Form-Four failures.Wale waliokuwa wana Division Four ya mwisho kabisa ndio walikwenda upolisi.Wanatumia miguvu mingi zaidi kuliko akili😡
 
Haya maandamano yataanzia wapi? Yanakwenda Bungeni ili kuachieve nini pale Bungeni? Sidhani kama kuandamana kwenda Bungeni kutaachieve chochote as far as this issue ya Wabunge 19 is concerned.

Based on experience, utashangaa hiyo kesho wapangaji wenyewe wa maandamano wakaingia mitini na wasijitokeze barabarani
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amesema ofisi yake haina taarifa rasmi za maandamano ya bawacha hivyo atakayeandamana atakutana na mkino wa dola.

Kamanda Muroto amewataka akina mama hao waliopanga kuandamana waje na computer na madaftari ya kuchukulia notisi ili waandike kile watakachokutana nacho kisha wakawafundishe na wenzao wa huko Geita ili liwe somo la keheshimu sheria na taratibu zake.


My take; Kwa kuwa Bawacha hawajaanza Safari ni busara wakahairisha kama Simba na Yanga!

====

Jeshi la polisi Dodoma limewataka baraza la wanawake Chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa Geita (BAWACHA) kuacha kufanya maandamano, Hii ni kufuatia baraza hilo kutangaza kufanya maandamano kupinga wabunge 19 wa viti maalumu kutoka cha hicho

kauli hiyo imetolewa leo na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

"Tumepokea tishio kwa njia ya mtandao kwamba baraza la wanawake chadema(bawacha)wilaya ya Geita kwamba wanampango wa kufanya maandamano kushinikiza spika awaondoe wabunge 19 pale bungeni kwamba hawapo kihalali"Amesema kamanda Mroto

"Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na kamanda Dodoma, kama wanataka kujifunza waje na Kompyuta na madaftari waandike notes ili somo watakalolipata wakawafundishe na hao waliowatuma, Waje na bukta kutakuwa na mazoezi ya masafa mafupi, maana watatoka jasho tutawaandalia maji ya kuoga kama wakitaka ya moto au ya baridi watayapata, tunawasubiri"

"Kuna lugha za kinyaa , wanawaita akinamama wenzao Covid-19 , hii ni mbaya waje Dodoma Tutawapa chanjo" - Kamanda Gilles Muroto.
Hapa ndipo huwa nashindwa kuelewa maana ya 'freedom of expression' (uhuru wa kutoa mawazo, maoni, kuonyesha hisia hadharani ili mradi mtu havunji sheria za nchi). Sina hakika sana kama hii haki ya kikatiba inatafsiriwa vizuri .
 
Nilisikia kuwa walishafukuzwa ila wamekata rufaa.Je kukata rufaa huwa inatengua maamuzi ya hukumu au mpaka rufaa iamuliwe?
Tofautisha maamuzi ya chama na ya mahakama .Mahakama ya chini ikihukumu jela unaenda utakata rufaa ukiwa jeka chama cha siasa sio mahakama katiba ndio hutumika kamati kuu imewafukuza sio final wamekata rufaa baraza kuu hivyo bado wanachama kikatiba ndio baraza linatakiwa kuwasikiliza wasingekuwa wanachama baraza kuu lisingeweza kusikiliza kesi zao sababu kazi yake kusikiliza rufaa za wanachama sio za wasio wanachama
 
Tofautisha maamuzi ya chama na ya mahakama .Mahakama ya chini ikihukumu jela unaenda utakata rufaa ukiwa jeka chama cha siasa so mahakama katiba ndio hutumika kamati kuu imewafukuza sio final wamekata rufaa baraza kuu hivyo bado wanachama kikatiba ndio baraza linatakiwa kuwasikiliza wasingekuwa wanachama baraza kuu lisingeweza kusikiliza kesi zao sababu kazi yake kusikiliza rufaa za wanachama
Duh sasa Halima alipeleka kiambatanishi gani hapo kwa Ndugae kuwa kateuliwa na CDM? Na Je kwa nini Halima asihamie tu CCM ili kumaliza mzozo?
 
Kamanda Muroto tambua kuwa haki ina upofu ndio maana haibagui mtu. Awe maskini,awe tajiri au mwanaCCM au mwanaChadema.

Akina mama wa chama chetu kuandamana sio kosa ni haki yao. Kama ni suala la taarifa siku hizi hata e mail zipo. Kama unahitaji taarifa kupitia kwa Ocd unaweza kupata

ANDHA KANOON
View attachment 1779056
Wasisahau bukta
 
Back
Top Bottom