RPC Safia Jongo: UTPC tusaidieni Geita, Waandishi wengi hawana Maadili

RPC Safia Jongo: UTPC tusaidieni Geita, Waandishi wengi hawana Maadili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Safia Jongo ametoa wito kwa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kuongeza nguvu na kuboresha hali ya utendaji wa Waandishi wa Habari Mkoani hapo kwa kile alichodai kuna changamoto ya utendaji na kukosekana kwa weledi.

Akizungumza katika Mkutano wa Wadau kujadili Mchango wa Sekta ya Habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, amesema Mkoa huo una changamoto ya weledi kwa Waandishi wa Habari kwa kuwa wengi wao hawazingatii taaluma zao, wanafanya kazi kwa makundi akidai kuna makundi takribani manne hali ambayo inachangia taarifa nyingi zinazoripotiwa kutokuwa na usahihi.

Ameongeza “Kukosekana kwa ushirikiano mzuri kunasababisha taasisi nyingine kama Jeshi la Polisi na zile za Serikali kutokuwa katika ushirikiano mzuri, natoa wito kwa UTPC kuongeza nguvu Geita hasa wakati huu wa Uchaguzi, ushiriano wao ni muhimu katika kutoa taarifa sahihi kwa Jamii.”
 
Back
Top Bottom