RRRR ya Rais Samia Watanzania wengi wanaoishi kimazoea hawatoielewa haraka

Unaishi kimazowea, badilika. "Reform and rebuild yourself".
Shikamoo Bibi, ni mimi mjukuu wako. Naomba tusipangiane R.
R nazozijua ni hizi
1. R- Rushwa (wizi, upigaji, kulamba asali)

2. R- Retailing (kuuza vitu vya nchi)

3. R- Recycling (kurudisha watu wa zamani, kurudisha madudu ya zamani)

4. R- Roaming (kusafirisafiri, kuzururazurura)

naomba kuwasilisha
 
Mkukuta ,mkurabita, kilimo kwanza , big result now na mengi yalizikwa.

Hakuna jipya chini ya CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo yoite ni8 mazowea, sasa hivi hakuna mazowea, kuna "reform na Revuilding".

Kwenye kilimo sasa hivi Tanzania ndiyo nchi pekee duniani inawezesha vijana wake kwa kuwa elimu, mashamba (yao wenyewe) kwaanzishia maisha, vifaa vya kisasa vya kulimia, mpaka visima inawachimbia na mabwawa inawajengea.

Hilo ni bonge la "reform" kwenye kilimo, kama unataka kuwa mkulima ziwahi fursa: Pitia hapa ujionee:

Wachana na mazowea zisome R za mama uitumie fursa. Usidanganywe.
 
Sasa kama anajua watu hawataelewa / haeleweki na bado anatumia medium ile ile kujaribu kuwaelewesha huoni kwamba hana tofauti na mtu asiyefanya chochote ?

Katika Maendeleo ambayo ni Sustainable lazima yawe ya-kujumuisha walengwa; bottom up approach na sio top to bottom..., wao wananchi ukiwashirikisha wanaelewa zaidi wanachotaka wewe kazi yako ni kuwa-facilitate..., (hayo mambo ya mawazo individual na kufanya vitu kwa fikra zako kafungue kampuni binafsi ufanye unachotaka - Nchi inabidi iendeshwe kwa kutumia Taasisi na mawazo / kushauriana na wadau)

Tulikuwa na kasumba ya miradi ya Magufuli sasa hivi Mawazo ya Mama sijui baada ya miaka mitano itakuwa ni mawazo ya nani !!! (Na yote haya yanafanyika kwa Gharama kubwa ya Kodi za Mwananchi)
 
Hayo yoite ni8 mazowea, sasa hivi hakuna mazowea, kuna "reform na Revuilding".

Kwenye kilimo sasa hivi Tanzania ndiyo nchi pekee duniani inawezesha vijana wake kwa kuwa elimu, mashamba (yao wenyewe) kwaanzishia maisha, vifaa vya kisasa vya kulimia, mpaka visima inawachimbia na mabwawa inawajengea.

Hilo ni bonge la "reform" kwenye kilimo, kama unataka kuwa mkulima ziwahi fursa: Pitia hapa ujionee:

Wachana na mazowea zisome R za mama uitumie fursa. Usidanganywe.
Failing state
 
falsafa hii ipo ndani ya Qur'an na inakwenda deeeper sana
Ulimaanisha hivi au? Acha utani wewe! Labda ujitoe ufahamu! Huyu ni Mungu au Binadamu mwenye chuki, hasira, jazba,kisasi, roho mbaya, wivu n.k. Unahisi atataka amani huyu?

Surah 47 Muhammad, Ayat 4-4​

فَاِذَا لَقِيۡتُمُ الَّذِيۡنَ كَفَرُوۡا فَضَرۡبَ الرِّقَابِ ؕ حَتّٰٓى اِذَاۤ اَثۡخَنۡتُمُوۡهُمۡ فَشُدُّوۡا الۡوَثَاقَ ۙ فَاِمَّا مَنًّۢا بَعۡدُ وَاِمَّا فِدَآءً حَتّٰى تَضَعَ الۡحَـرۡبُ اَوۡزَارَهَا ۛۚ  ذٰ لِكَ ۛؕ وَلَوۡ يَشَآءُ اللّٰهُ لَانْـتَصَرَ مِنۡهُمۡ  وَلٰـكِنۡ لِّيَبۡلُوَا۟ بَعۡضَكُمۡ بِبَعۡضٍؕ وَالَّذِيۡنَ قُتِلُوۡا فِىۡ سَبِيۡلِ اللّٰهِ فَلَنۡ يُّضِلَّ اَعۡمَالَهُمۡ‏ ﴿47:4

4. Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a´mali zao
 
1. R- Rushwa (wizi, upigaji, kulamba asali)

2. R- Retailing (kuuza vitu vya nchi)

3. R- Recycling (kurudisha watu wa zamani, kurudisha madudu ya zamani)

4. R- Roaming (kusafirisafiri, kuzururazurura)
Jionee R zinavyofanya kazi:

Hiyo ya juu ime cover sekta inayoajiri wengi Tanzania kuliko nyingine yoyote. Hii chini imecove ajira, vijana wahini ajira kwenye mashirika ya umma, sasa hivi haina haja ya kupitia utumishi, wanaajiri wenyewe kwa vihgezo vyao. Hizo ndiyo reforms za mama, wewe hata kama chadema nenda tu, huulizwi kasdi ya chama:

RRRR za falsafa ya mama Samia ina manufaa makubwa sana, tena sana kwa kila Mtanzania na kwa Tanzania kwa ujumla.

R hizi 4 za mama Samia zina fursa kubwa sana ndani yake, kwetu sote. Nawaasa Watanzania tusikurupuke na tusibaki kutawaliwa kimazowea na wala tusiwe na fikra za mama Samia kuwa anatawala kama tulivyozowea.

Mama Samia amekwenda mbali sana, tena ya mazowea na upeo wa kawaida. Katuleta fursa za ajabu kwenye falsafa yake ya RRRR. Natumai wote tutachukuwa muda tuisome na tuielewe, tujielimishe ili tuzitumie fursa zinakuja na hizi RRRR.

Namshauri sana Waziri wa Habari na Wasemaji wote wa Serikali, kila mmoja kwa nafasi yake aielezee na kuifundisha falsafa kimaelezo na kivitendo. Na hili ni kwa mawaziri wake wote na watendaji waliomuelewa, waielezee na waifanyie kazi kwa vitendo ili Watanzania tuzione na kuzijuwa fursa ziliopo.

Nawaasa wale mawaziri na watendaji wakuu wa serikali ambao hawajamuelewa, wakiendelea kmazowea na kutoielewa hii falsafa ni heri wajiondoe wenyewe, la sivyo watashushwa njiani.

Nahisi, Hussein Bashe, kaielewa sana hii falsafa na anafanya kweli Reforms, kisasa. Upande mwingine, naona Kitila nae ameanza kumuelewaa. Sina shaka kabisa na Mchechu kuwa amemuelewa mama vilivyo na analidhihirisha hilo kinaga ubaga.

Watu ambao nawaona bado hawajamuelewa ni pamoja na Kassim Majaliwa na Makamo wa Rais. Nawwaona bado wanataka kuendelea kimazowea.

R ya kwanza ni Reconciliation, unaweza kutafsiri kama kupatanisha au mapatano lakini kiuhakika, falsafa hii ipo ndani ya Qur'an na inakwenda deeeper sana. Nawashauri wote, wapitoe aya zo zinazohusina na "reconciliation" ili waipate vyema.

Wengi wetu, hata mimi mwanzoni nilidhani inaishia juu ya meza na kupeana mikono na chadema. Nikaona mbona ipo "too shallow", lakini nilipoingia na kuanza kuichimba na kuichambuwa dhanna nzima kwa undani, nikaiona yenyewe tu, bila zile R nyingine mtu anaweza kuandika thesisis kumi au zaidi za PhD na zote zikapita with "flying colors".

Kwa kuwa dhanna hii moja ni bdefu sana tena, ntakuwa nikiitowa vipande vipande vyake kidogokidogo wakati uzi unaendelea.

Vijana zitumieni fursa, kuna watu watajaribu kuzibania kimazowea, msikubali, sasa hakuna mazowea. Pia nawashauri vijana ambao hawazioni fursa, waulize tuwaoneshe zilipo.

Ahsante sana mama Samia. You are the best.
Hizo R nne yeye mwenyewe hazitoki moyoni mwake achilia mbali kuziamini. Ni siasa tu!
 
Ikiwa ukisoma huelewi basi hata macho hayaoni:

Sawa bi kidude, tangu asubuhi hatuna umeme hapa kwetu
 
1. R- Rushwa (wizi, upigaji, kulamba asali)

2. R- Retailing (kuuza vitu vya nchi)

3. R- Recycling (kurudisha watu wa zamani, kurudisha madudu ya zamani)

4. R- Roaming (kusafirisafiri, kuzururazurura)
Ndo maana halisi ya hizo r hongera mkuu
 
Mwite mama wewe sio kila mtu. Utatumiaje kiingereza wakati ni mswahili wa Makunduchi? Mwanannchi wa kawaida wala hashughuliki kutaka kujua maana yake ni kitu gani na inafaida gani katika maisha yake.

Ili uwe mwalimu mzuri unatakiwa uwe mbunifu kuwezesha somo lako lieleweke kwa ufasaha na haraka tayari kwa utekelezaji wa pamoja kuliko kuwa na mawazo ya kigeni wakati kuna hazina ya mawazo ya wazawa kwa mawasiliano ya lugha ya wazawa.
What Are The 4Rs? The 4Rs, Refuse, Reduce, Reuse, and Recycle, are a simple way of reminding us how we can make a difference.
 
Back
Top Bottom