Mhe. Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.
"Sasa ni wazi kwamba, mimi na wabunge wenzangu 18, tulionyanganywa uanachama wa CHADEMA juzi, tutarudishiwa uanachama wetu asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la CHADEMA litakapokutana kusikiliza rufaa yetu tuliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, juzi tarahe 27 Desemba 2020."
Haya ni maneno ya Mbunge mmoja wa viti maalum aliyeongea na mtandao wa Mama Amon, lakini ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani.
Alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na "tuhuma sita na ambazo ni hafifu na zisizo na mashiko kisheria."
Tuhuma sita dhidi ya kina Mdee
Mbunge huyo wa kike, aliyekuwa na ukakamavu hata kuliko baadhi ya Wabunge wa kiume kwenye Bunge lililopita, alizitaja hatua kwa hatua tuhuma hizo kama ifuatavyo:
“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa kushiriki katika mchakato wa kula njama ya kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi. ”
“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupanga njama za kuhujumu chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."
“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila kiongozi anatarajiwa awe na msimamo wa kuaminika, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama."
“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila mwanachama anatakiwa kujiepusha na upinzani dhidi ya chama na wagombea wake na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama hasa wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”
View attachment 1662912
Kivuli cha sehemu ya barua mojawapo iliyotumika kuwasilisha tuhuma kwa kina Mdee
"Kilichotushangaza zaidi ni kwamba, kwa tuhuma zote sita dhidi yetu walizozitaja kwenye barua ya tuhuma yenye ukurasa mmoja pekee, hakuna maelezo yoyote yenye kuonyesha nani alifanya nini, lini, kivipi, akiwa wapi, akiwa na nani, na kwa nini, jambo ambalo kisheria linamaanisha kwamba hakuna mashtaka yanayojibika tuliyopewa" anaongezea huyo Mheshimiwa Mbunge .
View attachment 1662269
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema
Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “kwa hiyo, tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”
Majibu katika rufaa ya kina Mdee
Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu.
Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.
“Mosi, ni kuhusu tuhuma zenyewe. Tunasema kwamba, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.
“Pili, ni kuhusu tuhuma zenyewe pia. Kusudi mtu atende kosa, lazima awe eneo la tukio. Lakini, ukweli ni kwamba, wengi wetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma ziliko ofisi za NEC na Chadema. Sisi kama viumbe wenye mwili hatuwezi kuwa sehemu zaidi ya moja kwa mpigo. Tunaongozwa na kanuni mbili, spatial locality and temporal locality (anwani ya mahali na anwani na muda). Mtu asiyekuwepo mahali fulani hawezi kutenda kosa mahali hapo,” anasisitiza Mbunge huyo.
“Tatu, ni kuhusu utaratibu. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.
“Nne, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.
View attachment 1662676
Devotha Minja (katikati) akiwa na begi lililo na kitu chenye ncha kali akiwaongoza wafuasi wa Chadema kwenye maandamano yaliyoziba njia ya kuelekea hotelini ambako kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilikuwa kinafanyika
"Na tano, ni kuhusu utaratibu vile vile. Tunapinga mtindi wa uandishi wa tuhuma dhidi yetu. Kawaida ya kuandika tuhuma ni kwamba lazima kuwepo na mambo mawili. Moja ni statement of offence (kanuni iliyovunjwa) na jingine ni particulars of offence (kitendo na mazingira yake). Katika barua za tuhuma dhidi yetu hakuna maelezo yenye kuonyesha kosa lilifanyika lini, wapi, kivipi, na pamoja na nani. Kamati Kuu iliandaa mashtaka ya kubahatisha tu. Kwa hiyo, tutaliomba baraza kuu ama kuielekeza kamati kuu kuandika upya mashtaka haya au kuyatupilia mbali kwa kuwa hayajakidhi vigezo vya tuhuma zinazojibika," anahitimisha maelezo yake Mheshimiwa Mbunge
Kwa kuzingatia haya yote, sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kwa ajili ya kuitisha Baraza Kuu ili likae, lipokee makabrasha ya mashtaka na utetezi, liyasome makabrasha hayo, liwasikilize watuhumiwa wakijieleza kwa mdomo, na hatimaye kuamua haki iko upande gani kati ya Kamati Kuu na kina Mdee.
Chimbuko la rufaa ya kina Mdee
Takribani, mwezi mmoja uliopita, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kujiridhisha kwamba kina Mdee walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chadema.
Aidha, Kamati Kuu iliamua kuwavua nyadhifa zote walizokuwa nazo ndani ya Chama na hivyo kuwataka kukabidhi mali za Chama walizokuwa nazo, sambamba na kuwazuia kujihusisha na masuala yoyote yanayokihusu Chama.
Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.
Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua ya kuomba kurejea kwenye chama kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.
Magazeti ya Saed Kubenea yawaandama kimakosa kina Mdee
Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema."
View attachment 1662268
Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukwatuhumu kina Mdee kuanzisha vita ndani ya Chadema
Hata hivyo, Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. “Kwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,” alionyesha mshangao.
Taarifa zaidi zilizoufikia mtandao wa Mama Amon zinaonyesha kwamba, tangu siku za hivi karibuni, Saed Kubenea amenunua gazeti la Raia Mwema kutoka kwa wamiliki wake wa awali. Amekuwa analitumia kuwashambulia kina Mdee tangu walipofanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 01 Desemba 2020.
Kwa mfano, katika toleo la tarehe 02 Desemba 2020, Gazeti la Raia Mwema lilikuwa na habari kuu yenye kicha cha maneno “Sakata la Viti Maalum: Limekwisha Hilo,” iliyoendelezwa kwenye ukurasa wa 3.
Habari hii iliufahamisha umma habari isiyo na uthibitisho kwamba "mkakati wa kutengeneza uasi uliratibiwa na Mdee kwa kushirikiana na wenzake watatu, Bulaya, Tendega na Agnesta."
Ndani yake kulikuwa na makala iliyoandikwa na mtu aliyejitambulisha kama Issac Kimweri yenye kichwa cha maneno, “Halima James Mdee: Kutoka Ukamanda hadi Yuda Ikarioti (uk. 9).”
Makala hii pia ilichapwa kwenye gazeti la la mtandaoni, linalomilikiwa na Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisioniline.com, chini ya kichwa cha maneno: Halima James Mdee: Kutoka U-kamanda hadi yuda Iskarioti.
View attachment 1662810
Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukimtuhumu Mdee kuwa na tabia za Yuda Iskarioti
Aidha, katika gazeti la Raia Mwema kulikuwepo na makala ya Mwandishi Maalum yenye kichwa cha maneno “Mdee ameshindwa kujibu maswali? (uk. 11).”
Makala hii ilidai kimakosa kwamba "kitu pekee alichoweza kueleza Mdee na wenzake 18 katika mkutano huo ni uamuzi wao wa kuwasilisha rufaa ya kupinga kufukuzwa kwao na Kamayi Kuu (CC), kwenye Baraza Kuu la Taifa (BKT), basi." Makala hii ilikiuka kanuni za uandishi kwa zaidi ya 75%.
Maandiko haya matatu hayakuzingatia kanuni za uandishi kwani yalijaa habari za kupotosha ukweli na ukweli nusu nusu. Badala yake yalilenga kuharibu taswira chanya waliyo nayo kina Mdee na wenzake.
Mhariri wa gazeti hili jipya ambaye hatajwi popote gazetini, kama ilivyokuwa inafanyika hapo zamani, alibariki makosa haya. Mmiliki mpya wa gazeti hili, Saed Kubenea, ndiye anajua mhariri ni nani na ndiye anamtuma kufanya yote haya.
Mtupe tu huyo kipaza sautiNaona kasepa kanipotezea mpaka sasa.
Kwetu sisi cdm hatuna muda mchafu wa kuwapokea virus wa kisiasa kama nyinyiTayari nimejibu.
Ubunge wa viti maalum hautegemei uhalali au uharamu wa uchaguzi.
Achana na huyo Bikidude kwisha habari yake.Kwetu sisi cdm hatuna muda mchafu wa kuwapokea virus wa kisiasa kama nyinyi
Hivi unajua ni kwanini Ccm na Cdm walipata viti maalumu ?! . Ni kwa sababu walistahili na ndiyo maana vingine havikupata .Swali hili ni irrelevant kwenye mada ya sasa.
Hata kama ilikuwa neither free nor fare, it doesn't follows that, kusiwepo na wabunge wa viti maalum kutoka Chadema.
Walidhani wangeendelea kuichezea cdm kama walivyo aminishwa na NdugayeAchana na huyo Bikidude kwisha habari yake.
Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Wewe hata shetani atakukana siku ya mwisho, kwahiyo sasa hivi unamgeuka kiongozi wenu wa waasi Halima Mdee?Jua yafuatayo:
1. Dispatch book ya Katibu Mkuu, Mnyika, ina mhuri wa NEC kuonyesha wamepokea barua na fomu za wapendekezwa wa ubunge viti maalum Chadema.
2. Hii maana yake ni kwamba:
(a) Ama Mnyika alipeleka kabrasha na sasa anajibaraguza
(b) Au kuna mtumishi wa ofisi ya Mnyika, Madam X, alimlia timing na kubeba nyaraka zilizoandaliwa na Mnyika pamoja na dispatch na kupeleka NEC.
3. Kwa hiyo:
(a) Ama Mnyika aadhibiwe peke yake,
(b) Au Mnyika pamoja na Madam X waadhibiwe pamoja,
(c) Lakini, kama Madam X ni miongoni mwa wabunge 19, basi wabunge 18 hawana hatia.
4. Kwa hiyo, propaganda za Covid19 sio sawa.
5. Atafutwe mkosaji na kuadhibiwa, lakini hii habari ya mwalimu kukuta kelele darasani na kuadhibu wanafunzi wote ni uhuni.
I shout a big No!
Karibu Sumbawanga,
Kwetu kuchele!
Sabab za mikwaruzano zinafanana,na je impact ya hyo mikwaruzano inafanana.ccm wako madarakani zaidi ya miaka 40.Kama sitaki uongozi wa nchi kutoka kwa chama chenye mikwaruzano, na uongozi wa sasa CCM una mikwaruzano, na uongozi mbadala una mikwaruzano, nakosa sababu ya kuuondoa uongozi wa sasa nilete huo mbadala.
Kwa sababu, nitafaidika nini kuondoa chama kimoja che mikwaruzano na kuleta kingine chenye mikwaruzano?
CHADEMA walitakiwa watuoneshe wao wako tofauti na CCM, wako bora kuliko CCM, hawana matatizo ambayo yako CCM.
Lakini wameshindwa, wametuonesha wao ni sawa tu na CCM.
Sasa kama chama chenye mikwaruzano tunacho tayari, CCM, kwa nini tukiondoe hicho na tuweke kingine chenye mikwaruzano?
Ninaamini baraza kuu la Chadema haliwezi kufanya makosa, na ikitokea wakawarudisha hawa malaya wa kisiasa basi ndio mwisho wa Chadema, wasahau sapoti kutoka kwa Watanzania wazalendoHivi unajua ni kwanini Ccm na Cdm walipata viti maalumu ?! . Ni kwa sababu walistahili na ndiyo maana vingine havikupata .
Kwa maana hiyo kila chama kati ya hivi viwili, kinastahili kufanya mambo yake bila kuingiliwa au kuwekewa mitego. Ccm na viongozi wake wafanye yao na si kuingilia majukumu ya Cdm na kamati zake. Vivyo hivyo Chadema.
Halima na team yake hawastahili kwa sababu za kughushi na kuingia bungeni, na baadaye kukaidi wito wa kamati kuu ya chama chao ya angalau kusikilizwa. Hawastahili kurudishiwa huo uanachama
Nafikiri hata kwa kwa viti maalumu iwe hivyo, ila wasipewe na NEC bali na vyama vyao na uwe ndio utambulisho wao kwa mamlaka ya bunge na wasindikizwe na kiongozi wa chama na mwakilishi wa Kamati kuu ya Chama husika.Wabunge wa majimbo wanaposhinda uchaguzi ukabidhiwa certificate ya ushindi na Nec, na hiyo ndio inakuwa utambulisho wao bungeni kwenye kujisajiri.
Huyo Hilda still a kid akacheze na wenzake [emoji41]View attachment 1663319
Hii nimeona kwa mwana Twitter Hilda Newton. Naipachika hapa kama ilivyo...
Una maoni yoyote kuhusu mtazamo wa huyu mama mwenzio Mama Amon?
Kwa ccm hakuna linaloshindika, yule Boniface Jacob wa ubunge alikuwa na barua ya kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la ubunge, kufika kwa mkurugenzi anaambiwa mgombea wa Chadema ameshachukuwa fomu.Nafikiri hata kwa kwa viti maalumu iwe hivyo, ila wasipewe na NEC bali na vyama vyao na uwe ndio utambulisho wao kwa mamlaka ya bunge na wasindikizwe na kiongozi wa chama na mwakilishi wa Kamati kuu ya Chama husika.
Andunje kawalisha tangopori nao bila kutafakari wakalifakamiaWalidhani wangeendelea kuichezea cdm kama walivyo aminishwa na Ndugaye
Yaani hawa tunawagonga nyundo bila huruma hawahitajiki ndani ya cdmAndunje kawalisha tangopori nao bila kutafakari wakalifakamia
Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Na jinsi alivyonyang'anywa umeya?Kwa ccm hakuna linaloshindika, yule Boniface Jacob wa ubunge alikuwa na barua ya kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la ubunge, kufika kwa mkurugenzi anaambiwa mgombea wa Chadema ameshachukuwa fomu.
Yani Tanzania inabidi tupate kiongozi wa kijeshi aanzishe consetration camps kama zile za Hitler humo wajazwe maccm wateketezwe kwa gesi, hawa si binadamu wa kawaida, hawastahili kuishi kwenye dunia iliyostaarabika.
Imetoka hiyo. Hawana pa kutokea. Mleta uzi anaonekana kuwa wakili wao.Kuwaita covid19 "G19" ni matumizi mabaya ya alphabet
Behold. Matumbo war in offing!Wenye akili wanasubiri kikao kikae maamuzi ya rufaa yatolewe, mengine yote ni umbea na ujinga. Kupoteza muda.
Sijui kwanini unahangaika hivi.
[emoji16][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] dah majibu mengine yanaumiza sana.Zamani tukiwa wadogo kuna wakati wavulana walikuwa wanapanga kupigana lakini wanawekeana masharti tupigane lakini hakuna kushikana korodani. Kuna ugomvi wa aina hiyo siku hizi? Hoja za kisheria ni ugomvi kama ugomvi mwingine.
Mkuu hakika wewe ni koboko na umeutendea haki huu uzi.Mhe. Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.
"Sasa ni wazi kwamba, mimi na wabunge wenzangu 18, tulionyanganywa uanachama wa CHADEMA juzi, tutarudishiwa uanachama wetu asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la CHADEMA litakapokutana kusikiliza rufaa yetu tuliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, juzi tarahe 27 Desemba 2020."
Haya ni maneno ya Mbunge mmoja wa viti maalum aliyeongea na mtandao wa Mama Amon, lakini ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani.
Alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na "tuhuma sita na ambazo ni hafifu na zisizo na mashiko kisheria."
Tuhuma sita dhidi ya kina Mdee
Mbunge huyo wa kike, aliyekuwa na ukakamavu hata kuliko baadhi ya Wabunge wa kiume kwenye Bunge lililopita, alizitaja hatua kwa hatua tuhuma hizo kama ifuatavyo:
“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi. ”
“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kula njama za kuhujumu chama kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kula njama za kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kula njama za kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, jambo ambalo ni sawa na kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."
“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kushindwa kuonyesha msimamo wa kuaminika kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama."
“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kushindwa kujiepusha na upinzani dhidi ya maamuzi ya chama na makundi ya majungu yenye kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”