Ndio wanataka waruhusiwe kwenda bungeni kuendelea kutetea hayo uliyosema.Hamna lolote zaidi ya
njaa. Sie twataka haki, uhuru wa kuongea na mendeleo ya watu. Njaa zenu tupa kuleeee, miaka yote pesa ya ubunge mwabugia tu hamkujua kuna kesho?
Poli-tricks aside, huyu Hilda anaweza kuvifahamu vifungu vya katiba ya chadema vyema kuliko huyo anayemuita mzee Halima?! Tutasikia mengi.View attachment 1663319
Hii nimeona kwa mwana Twitter Hilda Newton. Naipachika hapa kama ilivyo...
Una maoni yoyote kuhusu mtazamo wa huyu mama mwenzio Mama Amon?
Huyo kiongozi wa kijeshi atakuwa mtanzania, au mta- outsource?!Yani Tanzania inabidi tupate kiongozi wa kijeshi aanzishe consetration camps kama zile za Hitler humo wajazwe maccm wateketezwe kwa gesi, hawa si binadamu wa kawaida, hawastahili kuishi kwenye dunia iliyostaarabika.
Acha wenye mbwa wale mbwa zao. Tunatizama tuTuhuma ya traitors ndio inapaswa kuthibitishwa. G19 are innocent until further notice.
Halima Halima Halima kweli miaka yote zaidi ya kumi na tano hukujifunza integrity???????
Huwezi kusema kuwa hukuhusika kwenye kosa kwa kuwa anayekuchagua ni either or....,,Abd that you believe one or the other ir both did select you????? That is such a lie!!!
Utasemaje either or wakati unajua fika kuwa bila sahihi ya KM wa chama chako huwezi kuwa mbunge wa JMT kufuatana na katiba ya nchi??????? Please get your team out of there! Unaaibisha young women of Tanzania!
Those who consudeted you role models are now grossly disapointef!!!
Hakuna mbadala ya katiba ya nchi!!!! Usidanganye wananchi waliokupa heshima miaka yote!!!
Wote waliohusika wanaljua hilo! Kama wamechagua kupinga maamuzi ya kamati Kuu wanajiletea aibu tu hapo! Wamgekiri tu wamekosea na kuomba msamaha! Na kuomba warudi chamani so that they at least remain with some semblance of respect! La sivyo dada zangu this will be your premature end of politics as well as respect!!
It is painful though, because you were elected MPs! But someone deprived you all of your rights!!!! VThat someone is none other than the party that you want to give ligitimacy to despite all they did to you!! Despite evidence of vilations Halima herself observed!!!! Yes, Chadema deserves those seats and many more but not that way!!!!
It us true toi that the big number of mps from chama kubwa that are now holding those seats did not earn them!!! That is very painful!!! You may threfore, argue that they are also viti maalumu obtained illegally so why shoukd you not do the same??? The earnings from the position of mheshimiwa MP are also so attractive that the $$$ zeros may be blinding your judgement!!!
But have you considered other alternatuves in your lives apart from MPs earnings???????Please do so!!! Many of you couldbe absorbed in big institutions! You are all brilliant people!!
Why would you want to disgrace yourselves because of money???? When you may do even better elsewhere???
I urge you to sit down and think long and hard!!!!!
Do not give legitimacy to the fallen giant!!!!
Millions still love Chadema despite the unjust blow dealt them by the powers known!!!
Chadema remains the only legitimate political party in Tz!!
Dont let it down by becoming the speaker’s MP!!!!!!!!!
Thank you!!!
Kuhusu jawabu hili Mbunge huyo alifafanua kuwa Katibu Mkuu, John Mnyika, anapaswa kujua zaidi majibu kwa kuwa kitabu chake cha dispatch kina muhuri wa Tume kuonyesha kuwa Tume imepokea nyaraka kutoka kwa Katibu Mkuu.
"Napenda watu wafahamu kuwa Bawacha waliwasilisha majina ya wanawake waliopatikana kupitia mchujo wa chama na Katibu Mkuu kuyafanyia kazi kwa kujaza na kusaini fomu zao yakiwa ni maandalizi ya kuyapeleka Tume. Kwa sasa kitabu cha dispatch cha Katibu, John Mnyika, kina Mhuri wa NEC kuonyesha kuwa nyaraka za chama zilizoandaliwa na Mnyika zilipokelewa NEC. Hivyo, ama alipeleka yeye Katibu na sasa anapindisha ukweli au ofisini kwake kuna mtu mmojawapo aliyepeleka nyaraka hizo baada ya kuwa zimeandaliwa na Mnyika. Kama mtu huyo ni miongoni mwa wabunge basi wabunge baki 18 hawahusiki. Na kama mtu huyo sio mbunge, basi wabunge wote 19 hatuhusiki na hakuna njama wanazosema," alihitimisha hoja yake Mbunge huyo.
Katika hesabu kuna kitu kinaitwa ratio, pia kuna cross multiplication.Sabab za mikwaruzano zinafanana,na je impact ya hyo mikwaruzano inafanana.ccm wako madarakani zaidi ya miaka 40.
Upuuzi mtupu, hi hapo kwenye picha ya devotha Minja,umeonaje ndani ya pochi,kwamba Kuna kitu chene ncha kali,?Mhe. Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.
"Sasa ni wazi kwamba, mimi na wabunge wenzangu 18, tulionyanganywa uanachama wa CHADEMA juzi, tutarudishiwa uanachama wetu asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la CHADEMA litakapokutana kusikiliza rufaa yetu tuliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, juzi tarahe 27 Desemba 2020."
Haya ni maneno ya Mbunge mmoja wa viti maalum aliyeongea na mtandao wa Mama Amon, lakini ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani.
Alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na "tuhuma sita na ambazo ni hafifu na zisizo na mashiko kisheria."
Tuhuma sita dhidi ya kina Mdee
Mbunge huyo wa kike, aliyekuwa na ukakamavu hata kuliko baadhi ya Wabunge wa kiume kwenye Bunge lililopita, alisema kuwa sehemu ya barua ya tuhuma dhidi yao inazitaja tuhuma dhidi yao kama ifuatavyo:
"...ulikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama kwa kushiriki au kula njama ya kujiteua kuwa mbunge wa Viti Maalum ... [kinyume cha] ibara ya 7.7.17(q) ya Katiba... [na] kinyume cha kifungu cha Kanuni ya 10.2(iv), 10.3(iv) ya Kanuni za Chama, na pia kinyume cha Kanuni ya 3(a)(iii) na 3(e)(ii) ya Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."
View attachment 1662912
Kivuli cha sehemu ya barua mojawapo iliyotumika kuwasilisha tuhuma kwa kina Mdee
Kutokana na aya hii kama ikisomwa pamoja na Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama, Mbunge huyo alizitambua na kuzitaja tuhuma sita zinazowakabili kama ifuatavyo:
“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi. ”
“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa maana ya kuhujumu chama kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kula njama za kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kula njama za kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, jambo ambalo ni sawa na kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."
“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kushindwa kuonyesha msimamo wa kuaminika kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama."
“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kushindwa kujiepusha na upinzani dhidi ya maamuzi ya chama na makundi ya majungu yenye kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”
"Kilichotushangaza zaidi ni kwamba, kwa tuhuma zote sita dhidi yetu walizozitaja kwenye barua ya tuhuma yenye ukurasa mmoja pekee, hakuna maelezo yoyote yenye kuonyesha nani alifanya nini, lini, kivipi, akiwa wapi, akiwa na nani, na kwa nini, jambo ambalo kisheria linamaanisha kwamba hakuna mashtaka yanayojibika tuliyopewa" anaongezea huyo Mheshimiwa Mbunge .
View attachment 1662269
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema
Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “kwa hiyo, tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”
Majibu katika rufaa ya kina Mdee
Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu.
Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.
“Mosi, ni kuhusu tuhuma zenyewe. Tunasema kwamba, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.
Kuhusu jawabu hili Mbunge huyo alifafanua kuwa Katibu Mkuu, John Mnyika, anapaswa kujua zaidi majibu kwa kuwa kitabu chake cha dispatch kina muhuri wa Tume kuonyesha kuwa Tume imepokea nyaraka kutoka kwa Katibu Mkuu.
"Napenda watu wafahamu kuwa Bawacha waliwasilisha majina ya wanawake waliopatikana kupitia mchujo wa chama na Katibu Mkuu kuyafanyia kazi kwa kujaza na kusaini fomu zao yakiwa ni maandalizi ya kuyapeleka Tume. Kwa sasa kitabu cha dispatch cha Katibu, John Mnyika, kina Mhuri wa NEC kuonyesha kuwa nyaraka za chama zilizoandaliwa na Mnyika zilipokelewa NEC. Hivyo, ama alipeleka yeye Katibu na sasa anapindisha ukweli au ofisini kwake kuna mtu mmojawapo aliyepeleka nyaraka hizo baada ya kuwa zimeandaliwa na Mnyika. Kama mtu huyo ni miongoni mwa wabunge basi wabunge baki 18 hawahusiki. Na kama mtu huyo sio mbunge, basi wabunge wote 19 hatuhusiki na hakuna njama wanazosema," alihitimisha hoja yake Mbunge huyo.
“Pili, ni kuhusu tuhuma zenyewe pia. Kusudi mtu atende kosa, lazima awe eneo la tukio. Lakini, ukweli ni kwamba, wengi wetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma ziliko ofisi za NEC na Chadema. Sisi kama viumbe wenye mwili hatuwezi kuwa sehemu zaidi ya moja kwa mpigo. Tunaongozwa na kanuni mbili, spatial locality and temporal locality (anwani ya mahali na anwani na muda). Mtu asiyekuwepo mahali fulani hawezi kutenda kosa mahali hapo,” anasisitiza Mbunge huyo.
“Tatu, ni kuhusu utaratibu. Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, ibara za 6.5.1(a), 6.5.5 na 6.5.6, kila mtuhumiwa anapaswa kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kujibu ndani ya siku 14, na hatimaye kupata fursa ya kujitetea kwa mdomo baada ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Wao walitumia kifungu cha Katiba cha 6.5.1(d) kutuita kwa dharula ndani ya saa 48 wakitutaka kuhudhuria kikao cha uso kwa uso kwa sababu walidai kuwa kulikuwepo na sababu nzuri zinazohalalisha dharula hiyo. Lakini, hatukuona sababu ya kuhalalisha dharula hiyo. Lakini pia, kama waliona kuna dharula, Kamati Kuu ilikuwa na fursa ya kupata majibu yetu kidijitali, lakini hawakufanya hivyo. Haki yetu ya kupata tuhuma zilizoandikwa na muda wa kutosha kuandaa majibu dhidi ya tuhuma hizo haiwezi kufutwa kirahisi rahisi namna hiyo kana kwamba tuko vitani," anaeleza Mbunge huyo.
"Nne, ni kuhusu utaratibu vile vile. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.
“Tano, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.
View attachment 1662676
Devotha Minja (katikati) akiwa na begi lililo na kitu chenye ncha kali akiwaongoza wafuasi wa Chadema kwenye maandamano yaliyoziba njia ya kuelekea hotelini ambako kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilikuwa kinafanyika
"Na sita, ni kuhusu utaratibu katika suala jingine. Tunapinga mtindi wa uandishi wa tuhuma dhidi yetu. Kawaida ya kuandika tuhuma ni kwamba lazima kuwepo na mambo mawili. Moja ni statement of offence (kanuni iliyovunjwa) na jingine ni particulars of offence (kitendo na mazingira yake). Katika barua za tuhuma dhidi yetu hakuna maelezo yenye kuonyesha kosa lilifanyika lini, wapi, kivipi, na pamoja na nani. Kamati Kuu iliandaa mashtaka ya kubahatisha tu. Kwa hiyo, tutaliomba baraza kuu ama kuielekeza kamati kuu kuandika upya mashtaka haya au kuyatupilia mbali kwa kuwa hayajakidhi vigezo vya tuhuma zinazojibika," anahitimisha maelezo yake Mheshimiwa Mbunge
Kwa kuzingatia haya yote, sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kwa ajili ya kuitisha Baraza Kuu ili likae, lipokee makabrasha ya mashtaka na utetezi, liyasome makabrasha hayo, liwasikilize watuhumiwa wakijieleza kwa mdomo, na hatimaye kuamua haki iko upande gani kati ya Kamati Kuu na kina Mdee.
Chimbuko la rufaa ya kina Mdee
Takribani, mwezi mmoja uliopita, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kujiridhisha kwamba kina Mdee walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chadema.
Aidha, Kamati Kuu iliamua kuwavua nyadhifa zote walizokuwa nazo ndani ya Chama na hivyo kuwataka kukabidhi mali za Chama walizokuwa nazo, sambamba na kuwazuia kujihusisha na masuala yoyote yanayokihusu Chama.
Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.
Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua ya kuomba kurejea kwenye chama kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.
Magazeti ya Saed Kubenea yawaandama kimakosa kina Mdee
Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema."
View attachment 1662268
Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukwatuhumu kina Mdee kuanzisha vita ndani ya Chadema
Hata hivyo, Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. “Kwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,” alionyesha mshangao.
Taarifa zaidi zilizoufikia mtandao wa Mama Amon zinaonyesha kwamba, tangu siku za hivi karibuni, Saed Kubenea amenunua gazeti la Raia Mwema kutoka kwa wamiliki wake wa awali. Amekuwa analitumia kuwashambulia kina Mdee tangu walipofanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 01 Desemba 2020.
Kwa mfano, katika toleo la tarehe 02 Desemba 2020, Gazeti la Raia Mwema lilikuwa na habari kuu yenye kicha cha maneno “Sakata la Viti Maalum: Limekwisha Hilo,” iliyoendelezwa kwenye ukurasa wa 3.
Habari hii iliufahamisha umma habari isiyo na uthibitisho kwamba "mkakati wa kutengeneza uasi uliratibiwa na Mdee kwa kushirikiana na wenzake watatu, Bulaya, Tendega na Agnesta."
Ndani yake kulikuwa na makala iliyoandikwa na mtu aliyejitambulisha kama Issac Kimweri yenye kichwa cha maneno, “Halima James Mdee: Kutoka Ukamanda hadi Yuda Ikarioti (uk. 9).”
Makala hii pia ilichapwa kwenye gazeti la la mtandaoni, linalomilikiwa na Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisioniline.com, chini ya kichwa cha maneno: Halima James Mdee: Kutoka U-kamanda hadi yuda Iskarioti.
View attachment 1662810
Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukimtuhumu Mdee kuwa na tabia za Yuda Iskarioti
Aidha, katika gazeti la Raia Mwema kulikuwepo na makala ya Mwandishi Maalum yenye kichwa cha maneno “Mdee ameshindwa kujibu maswali? (uk. 11).”
Makala hii ilidai kimakosa kwamba "kitu pekee alichoweza kueleza Mdee na wenzake 18 katika mkutano huo ni uamuzi wao wa kuwasilisha rufaa ya kupinga kufukuzwa kwao na Kamayi Kuu (CC), kwenye Baraza Kuu la Taifa (BKT), basi." Makala hii ilikiuka kanuni za uandishi kwa zaidi ya 75%.
Maandiko haya matatu hayakuzingatia kanuni za uandishi kwani yalijaa habari za kupotosha ukweli na ukweli nusu nusu. Badala yake yalilenga kuharibu taswira chanya waliyo nayo kina Mdee na wenzake.
Mhariri wa gazeti hili jipya ambaye hatajwi popote gazetini, kama ilivyokuwa inafanyika hapo zamani, alibariki makosa haya. Mmiliki mpya wa gazeti hili, Saed Kubenea, ndiye anajua mhariri ni nani na ndiye anamtuma kufanya yote haya.
Kuwaita covid19 "G19" ni matumizi mabaya ya alphabet
Upuuzi mtupu, hi hapo kwenye picha ya devotha Minja,umeonaje ndani ya pochi,kwamba Kuna kitu chene ncha kali,?
Hujui hata unachotetea.ww ni Covid 19 tu.Vipi kuhusu kuwaita kina devota minja na hilda newton COVID19+?
Na wewe ni covid19+ tu.Hujui hata unachotetea.ww ni Covid 19 tu.
Ni matumizi mabaya ya pandemic kuwaita wanaharakati covid19+Vipi kuhusu kuwaita kina devota minja na hilda newton COVID19+?
1:- lini? Siku mmekula kiapo.
Ndio Huyu tunaona ile video yake 😜😘
Halafu ukaongezea na 'ndilolo'Mama Amon, nyie hamjakisaliti CHADEMA, mmetusaliti sisi tusio wanachama wa chama chochote ila tuliweka imani yetu kwenu.
Dawa ya upumbavu wenu ni kichapo tu kwa miaka yote mtakayokaa bungeni, next time mtajifunza umuhimu wa kuweka maslahi ya umma mbele kuliko huo mtumbotumbo wako uliojaa mbalaga na makatapela na kisyesye na kifughe na kipome
Mama Amon kokote aliko anatumiwa na walioishiwa hoja lakini wana bidii ya kuokoteza cha kusema.Mama Amon mmekera ,
Leo mfumo dume uwepo Chadema na si vyama vingine ?!
Hivi viti 19 vingetoka tu, kwa utaratibu na si huu wa kuwahiana , tena kwa kushirikiana na wasaliti wenu waliohakikisha hampati
Jimbo hata moja !!
Mama Amon bila Ubunge wa kutunukiwa na Ndugai na CCM hauwezi kumpa game fresh Baba Amon ?Mhe. Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.
"Sasa ni wazi kwamba, mimi na wabunge wenzangu 18, tulionyanganywa uanachama wa CHADEMA juzi, tutarudishiwa uanachama wetu asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la CHADEMA litakapokutana kusikiliza rufaa yetu tuliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, juzi tarahe 27 Desemba 2020."
Haya ni maneno ya Mbunge mmoja wa viti maalum aliyeongea na mtandao wa Mama Amon, lakini ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani.
Alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na "tuhuma sita na ambazo ni hafifu na zisizo na mashiko kisheria."
Tuhuma sita dhidi ya kina Mdee
Mbunge huyo wa kike, aliyekuwa na ukakamavu hata kuliko baadhi ya Wabunge wa kiume kwenye Bunge lililopita, alisema kuwa sehemu ya barua ya tuhuma dhidi yao inazitaja tuhuma dhidi yao kama ifuatavyo:
"...ulikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama kwa kushiriki au kula njama ya kujiteua kuwa mbunge wa Viti Maalum ... [kinyume cha] ibara ya 7.7.17(q) ya Katiba... [na] kinyume cha kifungu cha Kanuni ya 10.2(iv), 10.3(iv) ya Kanuni za Chama, na pia kinyume cha Kanuni ya 3(a)(iii) na 3(e)(ii) ya Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."
View attachment 1662912
Kivuli cha sehemu ya barua mojawapo iliyotumika kuwasilisha tuhuma kwa kina Mdee
Kutokana na aya hii kama ikisomwa pamoja na Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama, Mbunge huyo alizitambua na kuzitaja tuhuma sita zinazowakabili kama ifuatavyo:
“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi. ”
“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa maana ya kuhujumu chama kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kula njama za kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”
“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kula njama za kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, jambo ambalo ni sawa na kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."
“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kushindwa kuonyesha msimamo wa kuaminika kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama."
“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kushindwa kujiepusha na upinzani dhidi ya maamuzi ya chama na makundi ya majungu yenye kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”
"Kilichotushangaza zaidi ni kwamba, kwa tuhuma zote sita dhidi yetu walizozitaja kwenye barua ya tuhuma yenye ukurasa mmoja pekee, hakuna maelezo yoyote yenye kuonyesha nani alifanya nini, lini, kivipi, akiwa wapi, akiwa na nani, na kwa nini, jambo ambalo kisheria linamaanisha kwamba hakuna mashtaka yanayojibika tuliyopewa" anaongezea huyo Mheshimiwa Mbunge .
View attachment 1662269
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema
Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “kwa hiyo, tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”
Majibu katika rufaa ya kina Mdee
Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu.
Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.
“Mosi, ni kuhusu tuhuma zenyewe. Tunasema kwamba, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.
Kuhusu jawabu hili Mbunge huyo alifafanua kuwa Katibu Mkuu, John Mnyika, anapaswa kujua zaidi majibu kwa kuwa kitabu chake cha dispatch kina muhuri wa Tume kuonyesha kuwa Tume imepokea nyaraka kutoka kwa Katibu Mkuu.
"Napenda watu wafahamu kuwa Bawacha waliwasilisha majina ya wanawake waliopatikana kupitia mchujo wa chama na Katibu Mkuu kuyafanyia kazi kwa kujaza na kusaini fomu zao yakiwa ni maandalizi ya kuyapeleka Tume. Kwa sasa kitabu cha dispatch cha Katibu, John Mnyika, kina Mhuri wa NEC kuonyesha kuwa nyaraka za chama zilizoandaliwa na Mnyika zilipokelewa NEC. Hivyo, ama alipeleka yeye Katibu na sasa anapindisha ukweli au ofisini kwake kuna mtu mmojawapo aliyepeleka nyaraka hizo baada ya kuwa zimeandaliwa na Mnyika. Kama mtu huyo ni miongoni mwa wabunge basi wabunge baki 18 hawahusiki. Na kama mtu huyo sio mbunge, basi wabunge wote 19 hatuhusiki na hakuna njama wanazosema," alihitimisha hoja yake Mbunge huyo.
“Pili, ni kuhusu tuhuma zenyewe pia. Kusudi mtu atende kosa, lazima awe eneo la tukio. Lakini, ukweli ni kwamba, wengi wetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma ziliko ofisi za NEC na Chadema. Sisi kama viumbe wenye mwili hatuwezi kuwa sehemu zaidi ya moja kwa mpigo. Tunaongozwa na kanuni mbili, spatial locality and temporal locality (anwani ya mahali na anwani na muda). Mtu asiyekuwepo mahali fulani hawezi kutenda kosa mahali hapo,” anasisitiza Mbunge huyo.
“Tatu, ni kuhusu utaratibu. Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, ibara za 6.5.1(a), 6.5.5 na 6.5.6, kila mtuhumiwa anapaswa kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kujibu ndani ya siku 14, na hatimaye kupata fursa ya kujitetea kwa mdomo baada ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Wao walitumia kifungu cha Katiba cha 6.5.1(d) kutuita kwa dharula ndani ya saa 48 wakitutaka kuhudhuria kikao cha uso kwa uso kwa sababu walidai kuwa kulikuwepo na sababu nzuri zinazohalalisha dharula hiyo. Lakini, hatukuona sababu ya kuhalalisha dharula hiyo. Lakini pia, kama waliona kuna dharula, Kamati Kuu ilikuwa na fursa ya kupata majibu yetu kidijitali, lakini hawakufanya hivyo. Haki yetu ya kupata tuhuma zilizoandikwa na muda wa kutosha kuandaa majibu dhidi ya tuhuma hizo haiwezi kufutwa kirahisi rahisi namna hiyo kana kwamba tuko vitani," anaeleza Mbunge huyo.
"Nne, ni kuhusu utaratibu vile vile. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.
“Tano, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.
View attachment 1662676
Devotha Minja (katikati) akiwa na begi lililo na kitu chenye ncha kali akiwaongoza wafuasi wa Chadema kwenye maandamano yaliyoziba njia ya kuelekea hotelini ambako kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilikuwa kinafanyika
"Na sita, ni kuhusu utaratibu katika suala jingine. Tunapinga mtindi wa uandishi wa tuhuma dhidi yetu. Kawaida ya kuandika tuhuma ni kwamba lazima kuwepo na mambo mawili. Moja ni statement of offence (kanuni iliyovunjwa) na jingine ni particulars of offence (kitendo na mazingira yake). Katika barua za tuhuma dhidi yetu hakuna maelezo yenye kuonyesha kosa lilifanyika lini, wapi, kivipi, na pamoja na nani. Kamati Kuu iliandaa mashtaka ya kubahatisha tu. Kwa hiyo, tutaliomba baraza kuu ama kuielekeza kamati kuu kuandika upya mashtaka haya au kuyatupilia mbali kwa kuwa hayajakidhi vigezo vya tuhuma zinazojibika," anahitimisha maelezo yake Mheshimiwa Mbunge
Kwa kuzingatia haya yote, sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kwa ajili ya kuitisha Baraza Kuu ili likae, lipokee makabrasha ya mashtaka na utetezi, liyasome makabrasha hayo, liwasikilize watuhumiwa wakijieleza kwa mdomo, na hatimaye kuamua haki iko upande gani kati ya Kamati Kuu na kina Mdee.
Chimbuko la rufaa ya kina Mdee
Katika kikao cha 27 Novemba 2020, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kudai kujiridhisha kwamba kina Mdee walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chadema.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwaambia waandishi wa habari kuwa kina Mdee wamefukuzwa kwa sababu ya kupatikana na makosa ya usaliti, kughushi nyaraka, kujipeleka bungeni kuapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum bila ridhaa ya chama, na kushirikiana na wanaokitakia mabaya chama cha Chadema.
Kwa mujibu wa tamko la Mbowe, msimamo wa Chadema ni kwamba hawakubaliani na mchakato wa uchaguzi Mkuu wa 2020 na matokeo yake, na kwamba, kwa sababu hiyo, hawako tayari kufanya uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum, kwani hilo litakuwa sawa na kuhalalisha wanachokiita wizi wa kura za Chadema.
Mbowe alisema kuwa, wakati Chama chake kikiendelea kushikilia msimamo huo, ghafla kina Mdee walionekana Bungeni Dodoma wakila kiapo cha ubunge mbele ya Spika, Job Ndugai.
Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa mbele ya Baraza Kuu dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.
Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua kwenda kwenye Kamati Kuu, kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama, ili kuiomba ifanye marejeo ya maamuzi yake na kuwarejeshea uanachama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.