Rufiji: Vijiji 23 vimekumbwa na mafuriko makubwa kutoka Bwawa la Umeme la JNHPP. Je, Tathmini ya athari kwa mazingira ilipuuzwa kabla ya ujenzi?

Wewe mwenyewe unasemaje tatizo lilikuwepo, Kwa hiyo chanzo chake sio uwepo wa Bwawa.
La kujiuliza sasa ni kwanini uwepo wa Bwawa hakujatatua tatizo.
Na ukumbukmbe matarajio ya awamu ya Tano na matarajio ya awamu ya February yalikuwa tofauti, mpaka kumalizika Kwa Bwawa Hilo na kuanza uzalishaji .
Sasa watu wenye uelewa huanza kufanya ulinganishona tofauti za taarifa za Awamu ya Tano na za Awamu ya February.akisaidiwa na Nepi Nawea
 
Soma mada wewe mjinga
 
Serikali ilete mafuriko halafu taasisi na watu binafisi tuguswe?
Serikali iguswe tu kivyake.
 
Hilo Dubwasha siku liseme lijambe tu kidogo.Kuna story zitapigwa miaka na miaka na Vilembwekeze wa Nchi.

Vilembwe wa Kina Mwijaku,Mashalavu watasimulia sana huko mbeleni.
 
Mamia ya wananchi hawana mahali pa kuishi, huku wengine 55 kutoka Kaya 15 wakihifadhiwa katika Shule za Msingi wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani.

Ni baada ya nyumba zao kufunikwa na maji yanayotoka katika bwawa la Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP).

Mbali na kukosa makazi, watu hao wako hatarini kukumbwa na njaa baada ya mazao yao kuzama kwenye maji mashambani.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Aprili 4, 2024 katika Kijiji cha Mohoro wilayani humo, Diwani wa Mohoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rufiji, Abdul Chobo amesema tathmini za kila siku zinaonyesha maafa yanaendelea kuongezeka.

Hata hivyo, amesema wamewataka watu hao watafute sehemu nyingine ya kuhamia kwa sababu Jumatatu Aprili 8, 2024 shule zinafunguliwa.

Amesema hakuna kifo kilichotokea tangu mafuriko yalipoanza na jitihada za kuwaokoa zinaendelea.
 
Wazungu walipokataa huu mradi waliyajua yote haya.

Mungu wabariki Wazungu
 

View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1775954878486954481?t=KzTuuvW3q_kKLhd_QOXebA&s=19
 
Wajenge crown dams--maji extra yajaze vibwawa vidogo vidogo--wakodishie wavuvi wa samaki--walime kambale kibiashara---changamoto ni fursa!
Sasa kwa nn wasitengeneze bwawa lingine ambalo litakuwa lipokea maji yaliyozid kwenye bwawa la mwalimu nyerere
Kama kabla ya ujenzi wangefanya EIA haya yote yangezingatiwa ila Kwa sababu Kuna mtu alikuwa mjuaji sana basi ndio matokeo yake haya Sasa

View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1775954878486954481?t=KzTuuvW3q_kKLhd_QOXebA&s=19
 
Mtu mweusi anahitaji ukombozi wa kifikra na kiroho.
Blackman
 
Tuna viongozi wengi wasiozingatia taaluma za watu.

Mungu awanusuru wananchi wenzetu huko Rufiji
 
Kila project kubwa duniani huwa inachangamoto. Fuatilia Mega projects youtube Utagundua hilo.

Maji yangechepushwa mapema mngeanza kupika kelele kuwa maji yanafunguliwa ili mitambo ishindwe kujiendesha shida ya umeme iendelee.

Ishu ina control mechanism. Naamini miaka ya mbeleni itaisha. Faida za bwawa ni nyingi kuliko hasara. Kazi indelee
 
Siyo tathmini ya maziningira kupuuzwa bali ni kutokana na kufungulia bwawa hilo pole pole wakati likiwa limejaa na kusababisha lifurike. Juzi bwawa wamfungulia, halafu etiu wakalifunga na hivyo kusababisha overflow. Iwapo lingefunguliwa njia zake zote sawasawa kulingana na design, kusingekuwa na tatizo lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…