TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Dah! Wivu Hadi kwa Marehemu? We kilichokukera Nini ilihali waliosifia wamefanya hivyo kwa Utashi wao? Umekuwa Nani wa kuingilia Uhuru wa Watu kumsifia Ruge? Labda nikujibu kwa ufupi ili wivu wako upungue usije ukakusababishia UGONJWA wa Moyo.
1. Tamasha la Fiesta: pamoja na waliopata ajira ya kuburudisha, wapo pia waliofaidi kwa kuburudika. Yaani Ruge aliwapelekea Burudani ambayo wasingeweza kuifuata ilipo. Katika Tamasha Hilo, wapo waliouza maji, biscuits, mishikaki, chips, soda, vilevi, n.k. Pato walilolipata liliwasaidia familia, ndugu, jamaa na marafiki. Hii pekee imewafikia watu wengi unaowaona wanaomboleza.
2. THT, imeibua vipaji ambavyo vimesaidia kuongeza Pato la Taifa kupitia Sanaa! Sehemu ya Pato Hilo imetumika katika huduma za Jamii ambazo hata wewe na ndugu zako mmezitumia.
3. Malkia wa Nguvu + Kipepeo + Tamasha la Fursa: Wanawake na Vijana wameweza kupata Jukwaa la kuziona na kuzitambua fursa kadhaa wa kadha, na kwa kufanya hivyo impact Yake imeifikia Jamii.
So, wewe Kama ulitaka ukae hapo nyumbani kwa Shemeji yako kila kitu unakipata kwa Shikamoo halafu Ruge aje akuletee au akusaidie, utakuwa beyond MPUMBAV.U! Kama Jamii itashindwa ku appreciate hicho alichokifanya Ruge, itakuwa Jamii ya Hovyo kabisa (Bahati nzuri wamekuwa na Shukrani kwake na wameonesha katika msiba huu).
Mimi Binafsi sijawahi hata kukutana nae, na Kuna kipindi nilikuwa against baadhi ya Mambo anayofanya, lakini haikuondoa Mimi kujifunza Mambo mbalimbali kutoka kwake na namna Jamii ilivyoguswa kwa kadiri alivyoweza.

Swali kwako, WEWE UMEFANIKIWA NINI KATIKA JAMII? MCHANGO WAKO NI UPI? UTAACHA LEGACY GANI? (Nakuweka katika kundi ambalo litakuwa limehusika na mauaji ya Ruge (Kama inavyodaiwa) na mnajitahidi kuponda ili nafsi zenu zipate ahueni)

Sent using Jamii Forums mobile app

Positivity
Kudos


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika suala la Maadili nina uhakika Ruge anamchango hasi (Negative) kwa asilimia 100.

Fiesta imesaidia nini kimaadili katika Taiga letu?

Ni kwamba Ruge ameferiki kama MTU yeyote lakini napingana na suala la kukuza mambo.

Kwa jicho pana hata media alizokuwa akisimamia zilitumika kupromote Ushoga, Rejea Interview ya Kaoge.

Kusema kweli tuache unafiki.

Tazama, viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa ya kujenga ye kazi yake ikawa kubomoa.

Nasema hakuna Cha maana Ruge amelifanyia Taifa Letu, labda kwa Watawala na huko kwenye kampuni aliokuwa akiiongoza.
 
Mkuu naelewa hisia zako.
Lakini ukipata ka muda pitia Mhubiri 7:2.
 
Kwakweli, nianze kwa kutoa pole kwa vijana,wamama,na wazee wa Tanzania kwa kupatwa na msiba mzito sanaa hakika Ruge ameacha pengo la kubwa sana kwetu!

Pengo la kubwa ili hakika january Makamba ameliezea vyema tena kwa lugha iliyojaa Fasihi ambyo mara nyingi niliwai kukili kupia hapa jukwaani kuwa Makamba ni miongoni mwa Wanafasihi ambao nchi yetu tumejaaliwa


Sina lengo la kuelezea uzuri na ubaya wa Ruge,ila nataka nitumie fursa hii kuwakumbusha watu kama ALEX MSAMA mmiliki wa MSAMA PRODUCTION kujitokeza kuungana na watanzania kuomboleza msiba wa Ruge.

Nasema hivyo kwa sababu mchango wa Ruge kwa Alex Msama uko wazi,Alex msingi wake mkubwa wa Alex Msama tumjuaje leo hii kwa kila kitu anachofanya kilitokea clouds mikononi mwa Ruge.

Hakuna hasiye jua kuwa Alex Msama ni miongoni mwa vijana wa Tanzania ambao hawakubahatika kupata elimu ya juu,ila mtu huyu alipewa fursa ya kuwa miongoni mwa watamzania wachache walio pata fursa ya kutangaza kipindi cha nyimbo za injili hapo clouds,kipindi hiki ndicho kilichompatia msingi wa wazo la Tamasha la pasaka,tamasha ambalo leo hii limemfanya kutambulika Africa mashariki.

Leo hii anamiliki Television pamoja na Redio,nmesitikika skuona hata akijitokeza hadharani kuusema ukweli huu kipindi hiki cha msiba wake.

Nimwache huyo Msama,niende kwa dada yetu SAIDA KAROLI.

ndgu zangu watanzania,msio elewa SAIDA karoli kabla hajaja DSM alikuwa ni msani mdgo sanaa na alikuwa akipiga miziki kwenye MABAR mbalimblai mkoani kagera.

Ruge alikuwa mtu wa kwanza kukutana nae Bar,kama haitoshi hata nauli ya kumleta mjini Dsm alipewa na marehemu Ruge,kilichotokea baada ya karoli kufika jijini DSM, KWA kweli Ruge hakujali kama ataonekana mtu anaependelea ndgu zake alimkabidhi midomoni mwa watangazaji wa clouds walau wamzungumzie pamoja n kipawa chake,
Saida karoli alivuma sanaa na kukipatia fedha ambayo hakuwai kuishika kutoka kwa wasikilizaji wake wa Bar huko mkoani kagera,ni pesa hizo zilizomfanya mpka leo hii Saida Karoli kuwa miongoni mwa wamiliki wa Nymba jijini Dsm maeneo ya mbezi.

Cha kusikitisha,leo hii SAIDA karoli yupo kimnya anaungana na AKINA REDJEIDII NA DUDUBAYA,Kumwombea mabaya kijana wetu hakika niwaombe mjitokeze na kuusema ukweli kbla ruge hajaoza kaburini kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upumbavu na ujinga kutafuta wachawi wa msiba wa Ruge wakati wachawi na poisoners wameshiriki kulia pamoja nanyi,kulibeba jeneza lake na kuongoza msafara wa gari la maiti....SHAME ON YOU CLOUDS BOYS....
 
ILA Mange kuwa dada wa Taifa ni sawa shida ni Ruge tu? Wewe mwenyewe mbona mnafiki tu,kinachokuuma ni nini mazee? Can't you mind your fvcking business.
 
Sasa mtu alikua mkurugenzi wa radio kubwa, inayosikilizwa na watanzania wengi, alikua msaada mkubwa kwa ccm, amesaidia baadhi ya wasanii kwa hiyo msiba kuwa mkubwa sio kwamba alikua mtu muhimu kwa Taifa la hasha ila alikua mfanyabishara anayejihusisha na jamii, na wala sio kwamba alikua anasaidia jamii ila biashara zake zilimlazimu kujihusisha na jamii ili iendelee kukuwa zaidi, sasa wabongo wakiona hivyo wanajua wanasaidia kumbe mtu yuko kwenye business zake...! Ila pamoja na yote jamaa alikua mchapa kazi sana tuna la kujifunza kutoka kwake, ukikabidhiwa jukumu lifanye kwa nguvu zako zote na kwa moyo wote....! Clouds haikua yake ila kwa jinsi alivyokua anajishughulisha nayo unaweza Sema ni yake au ya baba yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya msiba kupita, nina list ya wanamuziki ambao kama nikisikia nyimbo zao zinapigwa mawinguni, basi nitajua jamaa msiba umewafunza jambo kubwa sana katika maisha. Vinginevyo nitajua jamaa kibri imekomaa kisawasawa.
 
Duuhhh aisee kwa iyo ni lazima watoke mbele hadharani na kusema kuwa Ruge alitufanyia ili na lile aiseee kweli watanzania kwa unafiki tumemzidi shetani.

Ngoja nianze na wewe tangia umezaliwa mpaka umekua na kuweza kujitegemea baba ako na mama ako wamekuwa wakikutunza kwa hali na mali na kwa kila kitu ikiwamo wao wenyewe kujinyima kwa ajili yako ili wewe upate unachokihitaji, sasa emu niambie ni lini ulitoka mbele za watu hadharani na kusema angalau zuri moja tu la wazazi wako walilokufanyia?

Na kwa unafiki wa aina hii ndugu mleta mada utakufa mlango wazi aisee

Nkikuuliza je hao uliowasema wakitoka mbele na kuyasema hayo unayowatuhumu nayo je yatamsaidia vip marehemu ama marehemu ana faidika nayo vip kwanini hukuona ni vusara kuwataka hawa watu wayaseme hayo mazuri aliyowafanyia bwana Ruge kipindi akiwa hai ili na yeye angalau ayasikie na kufarijika nayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa naamini kuwa unapokufa Malaika mtunza kumbukumbu hutumia siku ya kifo hadi kuvunjwa tanga kupembua mazuri na mabaya yako kutoka kwa wanaokusema vibaya na wanaokusema vizuri.


Tuishi katika hali ya Neema ya Utakaso.
 
Labda angeitwa Baba wa Taifa wa Kuharibu Vijana na Maadili hilo lingekuwa na mashiko.

Nashangaa Mkristo afe alafu hatuoni viongozi wa dini katika msiba hata kama mwisho atazikwa kidini, lazima kuna hitilafu mahali Fulani.

Watu wanaoharibu jamii yetu wanapewa sifa
wanaofanya mambo ya maana hata hawapewi attention yoyote.
 
Amefanya jambo zuri sana dada jide
Screenshot_20190304-102848.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom