TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba


Positivity
Kudos


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika suala la Maadili nina uhakika Ruge anamchango hasi (Negative) kwa asilimia 100.

Fiesta imesaidia nini kimaadili katika Taiga letu?

Ni kwamba Ruge ameferiki kama MTU yeyote lakini napingana na suala la kukuza mambo.

Kwa jicho pana hata media alizokuwa akisimamia zilitumika kupromote Ushoga, Rejea Interview ya Kaoge.

Kusema kweli tuache unafiki.

Tazama, viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa ya kujenga ye kazi yake ikawa kubomoa.

Nasema hakuna Cha maana Ruge amelifanyia Taifa Letu, labda kwa Watawala na huko kwenye kampuni aliokuwa akiiongoza.
 
Mkuu naelewa hisia zako.
Lakini ukipata ka muda pitia Mhubiri 7:2.
 
Upumbavu na ujinga kutafuta wachawi wa msiba wa Ruge wakati wachawi na poisoners wameshiriki kulia pamoja nanyi,kulibeba jeneza lake na kuongoza msafara wa gari la maiti....SHAME ON YOU CLOUDS BOYS....
 
ILA Mange kuwa dada wa Taifa ni sawa shida ni Ruge tu? Wewe mwenyewe mbona mnafiki tu,kinachokuuma ni nini mazee? Can't you mind your fvcking business.
 
Sasa mtu alikua mkurugenzi wa radio kubwa, inayosikilizwa na watanzania wengi, alikua msaada mkubwa kwa ccm, amesaidia baadhi ya wasanii kwa hiyo msiba kuwa mkubwa sio kwamba alikua mtu muhimu kwa Taifa la hasha ila alikua mfanyabishara anayejihusisha na jamii, na wala sio kwamba alikua anasaidia jamii ila biashara zake zilimlazimu kujihusisha na jamii ili iendelee kukuwa zaidi, sasa wabongo wakiona hivyo wanajua wanasaidia kumbe mtu yuko kwenye business zake...! Ila pamoja na yote jamaa alikua mchapa kazi sana tuna la kujifunza kutoka kwake, ukikabidhiwa jukumu lifanye kwa nguvu zako zote na kwa moyo wote....! Clouds haikua yake ila kwa jinsi alivyokua anajishughulisha nayo unaweza Sema ni yake au ya baba yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya msiba kupita, nina list ya wanamuziki ambao kama nikisikia nyimbo zao zinapigwa mawinguni, basi nitajua jamaa msiba umewafunza jambo kubwa sana katika maisha. Vinginevyo nitajua jamaa kibri imekomaa kisawasawa.
 
Duuhhh aisee kwa iyo ni lazima watoke mbele hadharani na kusema kuwa Ruge alitufanyia ili na lile aiseee kweli watanzania kwa unafiki tumemzidi shetani.

Ngoja nianze na wewe tangia umezaliwa mpaka umekua na kuweza kujitegemea baba ako na mama ako wamekuwa wakikutunza kwa hali na mali na kwa kila kitu ikiwamo wao wenyewe kujinyima kwa ajili yako ili wewe upate unachokihitaji, sasa emu niambie ni lini ulitoka mbele za watu hadharani na kusema angalau zuri moja tu la wazazi wako walilokufanyia?

Na kwa unafiki wa aina hii ndugu mleta mada utakufa mlango wazi aisee

Nkikuuliza je hao uliowasema wakitoka mbele na kuyasema hayo unayowatuhumu nayo je yatamsaidia vip marehemu ama marehemu ana faidika nayo vip kwanini hukuona ni vusara kuwataka hawa watu wayaseme hayo mazuri aliyowafanyia bwana Ruge kipindi akiwa hai ili na yeye angalau ayasikie na kufarijika nayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa naamini kuwa unapokufa Malaika mtunza kumbukumbu hutumia siku ya kifo hadi kuvunjwa tanga kupembua mazuri na mabaya yako kutoka kwa wanaokusema vibaya na wanaokusema vizuri.


Tuishi katika hali ya Neema ya Utakaso.
 
Labda angeitwa Baba wa Taifa wa Kuharibu Vijana na Maadili hilo lingekuwa na mashiko.

Nashangaa Mkristo afe alafu hatuoni viongozi wa dini katika msiba hata kama mwisho atazikwa kidini, lazima kuna hitilafu mahali Fulani.

Watu wanaoharibu jamii yetu wanapewa sifa
wanaofanya mambo ya maana hata hawapewi attention yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…