Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nasikiliza clouds nyimbo za huzuni hapaa!sina rahaa!!!Huyu baba kaniuma Kweli. Ndo nimesikia mda huu. Nimepatwa mshituko mpaka kichwa kinauma.
Poleni wafiwa.
Mi naamini taifa limempoteza mtu muhimu sana.
Pumzika ruge.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ameen(كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَنْ زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ)
[Surat Aal-E-Imran 185]
185. Kila nafsi itaonja mauti, na bila
shaka mtapewa ujira wenu sawasawa
siku ya Kiyama. Na aliyewekwa mbali
na Moto na kuingizwa Peponi, basi
amefaulu; na maisha ya dunia hii si kitu
ila ni starehe idanganyayo.
_________________________
Mchamungu mmoja katika pita zake alikutana na mzee mmoja, akamsalimia yule mzee, akamkumbatia na akambusu. Kisha akamuuliza una miaka mingapi mzee wangu(?). Bila hiyana mzee akajibu miaka aliyonayo. Akamwambia nina miaka 63.
Yule mchamungu akamwambia unafahamu kwamba umetembea safari iliyokuchukua miaka 63 kuelekea kwa mmiliki wako(Mungu)? Na unafahamu kwamba ukifika kwa mmiliki wako ni lazima atahitaji habari ya hiyo safari yako ilikwendaje? Ni majibu yepi uliyomuandalia?
Mzee wa watu hakuwa na jibu, akabaki analia.
Guys! Umri wetu ni mfupi sana. Huu uhai, afya, mali tunazomiliki, uzuri( ma HB na Masista du) haya yasitusahaulishe sana. Tule bata sawa ila tukumbuke Mungu yupo. Kama Duniani tunawekeana taratibu za kuishi sisi kwa sisi vipi yeye Mungu mwenyewe? Unafikiri katuacha tuishi tunavyotaka wenyewe? Tujipange.
Pole kwa wanafamila, ndugu, jamaa na marafiki na Tanzania kwa ujumla.
Yafaa mauti kuwa mawaidha tosha.
hakuna ugonjwa mzuriWith Kidney failure, sitashtuka sana! Siombi hayo lakini ule ugonjwa si mzuri katu. All metabolic wastes have no exit outside the body!