Dah! Wivu Hadi kwa Marehemu? We kilichokukera Nini ilihali waliosifia wamefanya hivyo kwa Utashi wao? Umekuwa Nani wa kuingilia Uhuru wa Watu kumsifia Ruge? Labda nikujibu kwa ufupi ili wivu wako upungue usije ukakusababishia UGONJWA wa Moyo.
1. Tamasha la Fiesta: pamoja na waliopata ajira ya kuburudisha, wapo pia waliofaidi kwa kuburudika. Yaani Ruge aliwapelekea Burudani ambayo wasingeweza kuifuata ilipo. Katika Tamasha Hilo, wapo waliouza maji, biscuits, mishikaki, chips, soda, vilevi, n.k. Pato walilolipata liliwasaidia familia, ndugu, jamaa na marafiki. Hii pekee imewafikia watu wengi unaowaona wanaomboleza.
2. THT, imeibua vipaji ambavyo vimesaidia kuongeza Pato la Taifa kupitia Sanaa! Sehemu ya Pato Hilo imetumika katika huduma za Jamii ambazo hata wewe na ndugu zako mmezitumia.
3. Malkia wa Nguvu + Kipepeo + Tamasha la Fursa: Wanawake na Vijana wameweza kupata Jukwaa la kuziona na kuzitambua fursa kadhaa wa kadha, na kwa kufanya hivyo impact Yake imeifikia Jamii.
So, wewe Kama ulitaka ukae hapo nyumbani kwa Shemeji yako kila kitu unakipata kwa Shikamoo halafu Ruge aje akuletee au akusaidie, utakuwa beyond MPUMBAV.U! Kama Jamii itashindwa ku appreciate hicho alichokifanya Ruge, itakuwa Jamii ya Hovyo kabisa (Bahati nzuri wamekuwa na Shukrani kwake na wameonesha katika msiba huu).
Mimi Binafsi sijawahi hata kukutana nae, na Kuna kipindi nilikuwa against baadhi ya Mambo anayofanya, lakini haikuondoa Mimi kujifunza Mambo mbalimbali kutoka kwake na namna Jamii ilivyoguswa kwa kadiri alivyoweza.
Swali kwako, WEWE UMEFANIKIWA NINI KATIKA JAMII? MCHANGO WAKO NI UPI? UTAACHA LEGACY GANI? (Nakuweka katika kundi ambalo litakuwa limehusika na mauaji ya Ruge (Kama inavyodaiwa) na mnajitahidi kuponda ili nafsi zenu zipate ahueni)
Sent using
Jamii Forums mobile app