Hili la kutubu ni moja ya maeneo makubwa sana yatakayo wapeleka Wakatoliki motoni.
Bwana wetu Yesu Kristo alitusisitizia "usihukumu, usije ukahukumiwa"
Who are you kuhukumu?.
Ukifanya dhambi unamkosea Mungu, hivyo kama ni kutubu, ni kutubu kwa Mungu na sio kwa mwanadamu.
Toba ya kweli ni baina ya mkosaji na Mungu wake, ili kufanya toba ya kweli huhitaji kwenda kuungama kwa Padri, hata ukitubu wewe mwenyewe tuu, tena kimoyomoyo, toba yako inafika, ndio maana Bwana wetu Yesu Kristo alitusisitizia, "tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo" . Nani alikuwako moyoni mwa Ruge zile siku zake za mwisho za uhai wake?.
Kanisa Katoliki linataka matendo, Yesu amefundisha mambo ya moyoni, who are they to judge?.
Ingekuwa Mungu Baba anatoa daily list ya wanaiongia mbinguni na motoni, kuna wengi mngekuwa surprised na kupigwa na butwaa pale mnapoona wale wakamilifu wetu, maaskofu, mapadri na viongozi wetu wa dini wakitupwa motoni, huku wadhambi wakiingia mbinguni. Yesu alikuja kwa ajili ya wakosefu na sio wakamilifu. Alisema" wote wenye mizigo, nitawapumzisha". Ruge aliishakabidhi mizigo yote kwa Yesu mwenyewe na sasa amepumzishwa. Nyie endeleeni na kuwategemea binaadamu, mtafanywa kuni...
P