RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

Mkuu nakuunga mkono. Wanatakiwa waweze kutofautisha artist attire na utupu. Ile ilikuwa ni creativiry ya hali ya juu kimavazi ya kisanii. Alichokifanya ni kurembesha maeneo nyeti ambayo kisanii jicho ndiko lingeingia hapo pia ndiko viewrs na followers na likes mitandaoni ili kukuza brand yake. Aisee bado tuna safari ndefu sana. Miezi 6 kufungiwa? Kwa uchumi upi huo? Walioajiriwa hapo mapato kibao na kampuni ya wasafi media pia tunapoteza mapato. Kama haina maadili kikwao Tisiaraei basi wawapige tu spana siku 3 au 5 inatosha. CCM hoyeee.
hawa wapigwe hata spana mwaka mzima.

"wapinzani watetereke" by Chuchu sijui Zuchu
 
🤣🤣🤣🤣🤣Mkuu. Mimi nimeona kawaida sana sana. Hivyo viurembo alivyozungushia maeneo pendwa ndiyo Tisiaraei wanalilia. Mimi sikuwa nimeona bali nilisikia tu. Sasa aliyetuwekea picha hapa ndiyo amenifungua macho kumbe hakuwa uchi bali artistic attire yake ndiyo timeshindwa kuielewa.
Nchi inaongozwa na washamba washamba Sana kuna uchi gani hapo?
 
Nilishangaa sana multichoice kuziondoa ITV na Start TV kwenye king'amuzi chao (binafsi naamini yale yalikua maelekezo kutoka nanilii) halafu wakaiweka Wasafi TV; nilishangaa sana yaani
 
Hao TCRA itabidi wapunguziwe mamlaka, itakuwa wanatumika tu na washindani wa kibiashara wa watu.

Miezi sita as if wametangaza kupindua serikali.

Hizo ni ajira za watu na ni uwekezaji pia lazima adhabu zizingatie na hayo.
Upo sahihi ila hizi television zinaupumbavu mwingi sana,wengine watajifunza
 
Wana
wanyoosha balaa raia. Wakiiba sh.100 kwa wateja million 2 tu washarudisha hela zao.
Na Target kubwa ya hizo regulatory authorities siku hizi imekuwa ni kukusanya pesa, siyo kuboresha ay kusimamia huduma. Ni mwendo wa kuviziana tu, ukosee uliwe.

Nchi hii ndio maana watu wanakwepa kodi maana issue siyo kodi tu.

Siku hizi kila kitaasisi kinakusanya pesa.

1. TCRA

2. TARURA
3. NEMC .
4. TMDA
5. Serikali za mitaa

6. TRA

7. TCCIA ( Hawa wanachukupesa za Kurusha drone 🤓🤓

8. Halmashauri
9. TBS
10. Traffic Polisi

11. DPP




Na CCM hawajakufuata kutembeza bakuli la shughuli za chama na michango ya mwenge
 
Hawa Wasafi dizain flani kama walitaka kuleta mazoea hivi. Au walizani....
kisa walimpigia mheshimiwa kampeni, ndo wakivunja sheria wasishughulikiwe?
Hii ndo serikali ya chuma a.k.a mwamba ukizingua lazma uketishwe kwenye kuti la moto bila ya kujali ulifanya nini na wee ni nani
Waliipenda wenyewe chaguo lao milele na wavimbe wa pasuke TCRA mbele kwa mbele
Mitano Tena.
 
TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha kurusha matangazo kwa miezi sita kuanzia leo kutokana kwa kukiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui ya utupu.

Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money akicheza ‘utupu’ kinyume na Kanuni katika tamasha la “Tumewasha Live Concert” lililorushwa Januari Mosi 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

Aidha Wasafi Tv wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.

Pia soma > Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?
Japo ni adhabu nzuri lakini haikustahili.
Maana hapo kuna ajira za watu wengi pamoja na mapato yanapotea kwao.
Bora wangewapa adhabu ya kuwafungia hata kwa mda mchache au kutoa faini au vyote kwa pamoja.
Ila si kwa miezi yote hiyo.
Nitarudi...
 
Hao TCRA itabidi wapunguziwe mamlaka, itakuwa wanatumika tu na washindani wa kibiashara wa watu.

Miezi sita as if wametangaza kupindua serikali.

Hizo ni ajira za watu na ni uwekezaji pia lazima adhabu zizingatie na hayo.
mkuu hata mimi ninashangaa cjui hii nchi inaongozwa na watu aina gan
 
Back
Top Bottom