Uzi umeshiba sana, keep going ...🤛🤛🤛Habari za wakuu hapa ni vema uzi uachwe kuonesha nani kapoteza kwa namna tofaut tofauti,
Kuna Nyuzi nyingi Sana hapa ila huu utakuwa wa kitaalamu Na shuhuda nilizoshuhudiwa siyo kwa kusimuliwa
Wengi wameeleza chanzo cha Vita hii ila kwa hapa naonesha Matokea tu
1. Mpaka sasa week Jana natoka Moscow kulikuwa Na hali Ya sintofahamu juu Ya majenerali wanaokufa vitani,
Putin amepangua walinzi wake mara nne tokea vita imeanza, kutokana na kuhofia Usalama wake ,
2. Kuna Uhaba wa Bidhaa katika supermarkts na zimebaki zilizokaribia kuisha Muda wa matumizi,
3.mpaka tarehe 24/03/2022 warusi 1200 walikuwa wakipinga na kuandamana kukataa vita wamefungwa magerezani na watakuwa na kesi za kujibu
4. Wanajeshi wanaokufa ni wengi sana wa Urusi takriban wanajeshi 7000 wameuwawa kwa namba sahihi, Hii ni kwasababu wengi wao hawakuwa tayari na vita hii hawakupenda,
Ukawa mzozo mkubwa wa warusi kutengwa na Dunia
Waliosafiri Au waliobahatika Kusafiri wanaelewa hapa nikisema,
-Visa card yako haifanyi kazi,
-Hutaweza kulipa Au kulipwa na wadeni wako kwakuwa benki yako Iko disconnect
-hutapata visa Kwenda sehemu kadhaa Duniani hata Kama una maslahi huko
-Majumba Au mali ulizonazo zinawekwa rehani
Hayo ndo wanapitia warusi..
Suala la kutengwa Duniani kuhusu Biashara limemuumiza sana Urusi
1.Kuna nchi ambazo zilitaka kuonekana Neutral Kama India Lakin hakuna wakubishana na Dunia akaweza,
Natoa mfano tu
India na Marekani na Kwanini India hawezi poteza uchumi wake eti Kisa Ushikaji na Urusi
Watu wanadhani India ana uwezo wa kutenda Kunyume na USA.
Hebu tuangalie hapa.
Biashara kati ya India na Russia ni US$ 8 billion,
Kati ya hizo, india anaingiza US$ 2.6 wakati Russia anaingiza US$ 5.48 billion.
Biashara kati India na US ni US$ 113.391
Kati ya hizo, India anaingiza US$ 73 billion, wakati US wanaingiza over US$ 40 billion.
Yaani India abomoe uchumi wake kwa ajili ya Russia.
Kati the world largest trading partners 20 wa India duniani, Russia hayupo kabisa, halafu mnamuamini India akisema yeye hapangiwi cha kufanya...mnataka afee?.
Kabla ya kushabikia au kuyaamini maneno au taarifa zinazichapishwa. Huwa ninawafundisha watu kuwa siku zote kabla ya kuelezea maoni yao, au kuamua ku side na jambo, basi wawe wanaenda na facts zao, hata kama mhusika ndiyo anaongea, wewe just deal with the facts, the numbers, the data
Hivi India kujifaragua kwamba atanunua mafuta ya Urusi ni ya Muda tu!
Watu huwa wanaamini kuwa China na Marekani ni maadui. Siku zote nimekua nikisema China kamwe si aduiwa US. Wametuaminisha hivyo ila mimi nimegoma kuliamini hilo. Hao ni greatest partners na wanategemeana in so many ways baada ya US kuhamishia kule technolojia zake na viwanda vyake vingi kwa lengo la kupata cheap labours na masoko ambayo US asingeweza kukubalika.
Kwa kufanya hivyo aliondoa influence ya Russia kwa China. Mahusiano ya Russia na China yapo masikioni na kwa maneno zaidi, wakati mahusiano kati ya China na US ni ya dhahiri ingawa watu hawaoni, sababu ni ya kimkakati na kujizatiti zaidi. Hata ukiangalia among the Chinese wenyewe, wananchi wana prefer kuwa karibu zaidi na USA kuliko Russia.
Mwaka 2020 kulikua na Chinese 3.70+ milion wanaoishi USA, Wakati wachina waliokua wakiishi Russia mpaka mwaka 2021 walikua ni 39,000+ tu. Mind China na Russia anayesemekana kuwa greatest partner ni majirani wanao share border😅, inazidiwa hata na Japan ambaye ni taifa hasimu la Jadi la China lakini ndani ya Japan kuna Wachina 770,000+.
Hata Mongolia kuna Wachina wengi kuliko Russia, Mongolia kuna Wachina takribani 1.3 milion.
Hilo litakupa mwanga wa kujua kama kweli ni adui US na China ni maadui au laah.
Katika list ya Major trading Partner wa China Duniani, Marekani ni namba moja, halafu kuna European Eunion then kuna South Korea na Japan, wote hao ukiwataja unamtaja Marekani. US ndiye kampa mchongo China wa masoko hayo, ndiye aliyempa teknology, mitaji na viwanda na ndiye aliyewaambia jao wampokee.
Hata ukija kwenye mahusiano ya kijeshi, miongoni mwa partners watatu bora wa China, US ni mmoja wapo😅😅, ndiye anayempa technolojia za vifaa vya kijeshi na kubadilishana taarifa za kimafunzo na kimbinu...bado ni maadui kweli hao😅😅?
Uadui wa China na Marekani ni wa kutengenezwa tu.
USA siyo fala, hafanyi hizo investment ili kujiua, bali anajizatiti. They are there to stay, wamemtengeneza China ili kutoa sehemu ya wasiompenda kwenda ku ventilate ili wasije wakavimba wakapasuka wakakufa.
USA anawapenda sana😅😅 mpaka anajitengenezea adui mdori ili tu watu wafurahi😅.
US anajua hapendwi na interests zake zinawindwa kote duniani, hivyo basi, kupitia mitaji, viwanda, technology etc alizompatia China anakua amezipaka rangi na logo ya China biashara na products zake ma hivyo kuweza kuuza Russia , Iran na sehemu zote ambazo mmarekani hakubaliki, amnako wanamuona China kama mkimbozi na mbadala wa Marekani. Wasilolijua ni kuwa US anamtumia China.
UN kwenye mzozo wa Ukraine wamepiga kura ya kuweka azimio la kuitenga Russia kuhusiana na kitendo chake cha kuivamia Ukraine, nchi 141 ziliunga mkono azimio hilo, nchi 35 hazijupiga kura kati ya nchi zilizopiga kura, nchi tano zilipiga kura kupinga hilo azimio na hovyo kuiunga mkono Russia, nchi hizo ni Russia yenyewe, Belarus, Syria, Eritrea and North Korea._* China ambaye anasemekana ndiye adui namba moja wa US na rafiki wa damu wa Russia hayupo hapo😅😅.
Watu wanatumia elimu zao, kufanya future predictions, innovations, management, productions, strategising and so so.. aisee, sisi ndiyo kwanza tunatumia vikao bungeni kuponda elimu na kuifubaza, pambavu zetu sisi.
Hivo China Kama ni mshkaji wa Russia asinge sita
Kuhusu kulipa Kwa Ruble Mafuta ya Urusi
Tukubali Urusi alikuwa Namba one kuuza Ulaya mafuta na gesi haina Ubishi ila kumbuka mwenye Reserve kubwa ya Mafuta Duniani ni Venezuela, na Iran Yuko miongoni mwa wenye reserves kubwa
Ally wa US Yaan UK Kalipa deni la $400M kwa IRAN na watu wake ma spy wawili wameachiwa sasa kinachofuata watamfungulia vikwazo na wanunue mafuta yake .....kuziba pengo la ya Rusia ....Marekani nae kamaliza vikwazo vya Venezuela ili akombe mafuta...
Boris wa UK alienda arabuni pamoja na kwamba mfalme kanyonga watu 81 Jumamosi Ya week kadhaa zilizopita LAKINI MAFUTA YANAFUTA DHAMBI HIYO NA LEO NAJUA MFALME ATAMWAMBIA PM KUWA HAKIKISHA CHELSEA ANAINUNUA MTOTO WA DADA YANGU...KESHAWEKA MEZANI £2.7B Sawa na $3.5B
Leo UMOJA wa Ulaya pamoja na G7 wamemwambia Urusi we can’t buy your gas by Ruble tutatumia Sarafu yetu Yaan hawataki madafu,
Italy na Spain leo wametia Saini kujenga Bomba Lao la Mafuta Kuacha kutegemea ya Urusi,
Ujerumani ambayo ilikuwa na mradi wa ujenzi wa Bomba na Urusi Kama Nordic 2 imesitishwa na pia hawatanunua gesi kwa Ruble hata Urusi wenyewe wamekubali,
Kuna Suala la Sarafu ya Ruble kupanda ni Kwa Muda tu Kwakuwa impact on currency changes have some factors moja ikiwa pegging Kama aliyo Fanya Urusi but won’t be in long run , ni kwakuwa wanunuzi wanatafta ufumbuzi wa mbadala
Ntaendelea Uzi usiungwe kwingine plz……
mi nilipoona Balozi wa China anaenda Washington mwenyewe ku-declare kwamba china haijatoa silaha kuisaidia russia kwenye ile vita ya Ukraine basi nilijua tu china kumbe ni chui jike tu kwa Marekani