View attachment 2356136
Kuna mambo ambayo kila kiongozi hijipambanua nayo.
Ruto kuna namna kajinasibisha na JPM kwa kuchagua kundi la walalahoi ambao kawaita (husslers)
Kashughulikiwa bei ya mbolea kutoka sawa na TZS 125,800 mpaka 67,700. Hii itashusha gharama za uzalishaji wa mazao ya kilimo na kupelekea bai za unga kuwa nafuu kwa walio wengi.
Hili jambo lazima litawaudhi "wapigaji" kwenye mfumo wa mbolea na mengineyo.
Ruto kaanzisha wizara ya ushirika na SME, hapa akifanya kwa vitendo kwa kuipa wizara fedha itasisimua sana biashara ya kuchochea vijana wengi kuingia kwenye shughuli za uzalishaji, likewise itaongeza pato la serikali. It's very obvious mtu akiwa na fedha huwa anatumia, eventually serikali itaongeza tax base kwenye hili.
Ruto kajifananisha na JPM kwa kutaka liwezekano leo, lisingoje kesho; kama tume Mahakama ilishafanya kazi yake ya kupendekeza majaji, yeye katumia madaraka yake ya Urais kuwathibitisha na kutangaza kuapishwa kesho yake (ambayo ni leo)
Tuwape kongole jirani zetu 254, bila shaka wapepata mtu anaejali maisha ya watu wa kawaida. Huenda along the way akawa dikteta kama JPM, hapendi kuzungushwa kwa umangi meza na "michakato" na hapo ndipo wanaompinga asipokuwa mvumilivu atatumia nguvu.
Ila uzuri Kenya kuna namna katiba yao imetengeneza balance of power kwa kuwapa nguvu wasioridhika kwenda mahakamani.
Ruto alikwenda mahakamani kumpinga boss wake asiendelee na BBI na akafanikiwa. Wakenya wakiona anatoka kwenye mstari wanaweza kumpeleka mahakamani.
Tuwape kongole majirani kwa kuvuka kwenye uchaguzi na sasa wana rais mpya. Ruto ashughulikie haki za binadamu kwa kutaka polisi na vyombo vya usalama viwajibike kwenye udhibiti wa watu.
Jana kuna watu wamepigwa sana kwenye harakati za kuzuiliwa wasiingie ndani ya uwanja kushuhudia tukio la Rais wao mpya akiapishwa.
Nguvu ingetumika kuzuia pasi kutoa kipondo wa wananchi.