Ruto anaonyesha kila dalili za kuja kuwa Kama Magufuli

Ruto anaonyesha kila dalili za kuja kuwa Kama Magufuli

Kenya wanatakiwa kuwa makini Sana na huyu jamaa Urais wake unaweza kuwa Kama wa Magufuli alivyofanya Tanzania

Naweka huu uzi ambao utakuwa kumbukumbu miaka 3 mpaka 4 ijayo Mara tu atakaposimika watu wake kwenye system zote za nchi.

Ruto sio kiongozi kwa mtazamo wangu bali ni mtawala.

Ruto,Trump na Magufuli wana sifa moja ya kuwa watawala Kama ambavyo Kikwete, Uhuru na Obama walivyokuwa viongozi.
Huyu Jamaa atawasaidia sana Wakenya Kama alivyotusaidia sisi Mjomba Magu.
 
Nimemsikia akisema ataondoa bajeti ya IGP na (jeshi la polisi) kutoka ikulu na kuwapelekea wao ili kiwe chombo huru. Sasa, utamkejeli vipi huyu mwamba?!

Mimi namuona kama mtu mtendaji zaidi, kitu ambacho waafrika tunataka. Zaidi ya yote, ni kiongozi mwenye charisma kubwa na tunamtakia kila la kheri!
 
Atakuwa dictator zaidi ya Magufuli. Nimesikiliza hotuba zake, naona viashiria vyote vya tabia za Magufuli. Wakenya watajuta kutomchagua Raila kwani ndio hasa baba wa demokrasia ya Kenya.
Lkn kwa kuwa Kenya Kuna taasisi na mifumo imara atabanwa na hizo taasisi Kama Trump alivyobanwa kule Marekani akashindwa kufurukuta.
 
Kenya wanatakiwa kuwa makini Sana na huyu jamaa Urais wake unaweza kuwa Kama wa Magufuli alivyofanya Tanzania

Naweka huu uzi ambao utakuwa kumbukumbu miaka 3 mpaka 4 ijayo Mara tu atakaposimika watu wake kwenye system zote za nchi.

Ruto sio kiongozi kwa mtazamo wangu bali ni mtawala.

Ruto,Trump na Magufuli wana sifa moja ya kuwa watawala Kama ambavyo Kikwete, Uhuru na Obama walivyokuwa viongozi.
Tathmini yako iko kinyume kabisa. Jana hiyo hiyo wakati anahutubia baada ya kuPapishwa amechukua hatua ambazo ni kinyume cha hayo unahotabiri. Ametangaza kuteua majaji ambao walipitisbwa na Tu.me ya mahakama lakini Kenyatta akamute. Ameiongezea bajeti mahakama , amepiga marufuku serikali kuingilia polisi kwa kulazimisha wapinzani wa serikali kutengenezewa makosa ya jinai na polisi; pia ameipa autonomy katika masuala ya pesa ipate mgao wake inaotakiwa kupata bila kuhusisha ofisi ya Rais . Hizi sio dalili za mtu mwenye maamuzi ya, kiimla. Kumbuka polisi ndio tool kubwa ya watawala madikteta.
 
Atakuwa dictator zaidi ya Magufuli. Nimesikiliza hotuba zake, naona viashiria vyote vya tabia za Magufuli. Wakenya watajuta kutomchagua Raila kwani ndio hasa baba wa demokrasia ya Kenya.
Laila ni fungu la kukosa kama kwa Lisu na chama chake tu
 
We jamaa naanza kuwa na wasiwasi na wewe, hivi unadhani Kenya ni Tanzania?

Wakenya wapo mbali kimifumo kutushinda sisi...

Kwa taarifa yako Wakenya wamempata Hichilema wao waliyekuwa wanamsubiri kwa hamu.

Kenya Rais hawezi kuiweka mihimili mingine ya serikali mfukoni mwake...

Mahakama ziko huru..... Wewe imagine mshindi wa urais ameamuliwa mahakamani kiuwazi kabisa.

Bunge liko huru, tena lina uwiano mzuri wa chama tawala na chama pinzani..

Baraza la Seneti, hili nalo lina uwiano mzuri wa chama tawala na ponzani...

Sasa mpaka hapo utasemaje Rais atakuwa dikteta? Kwa jinsi mifumo yao ilivyo thabiti ni ngumu sana.
 
Back
Top Bottom