Ruto anaonyesha kila dalili za kuja kuwa Kama Magufuli

Ruto anaonyesha kila dalili za kuja kuwa Kama Magufuli

Ndivyo ilivyo, huo ndio ukweriii ndugu zangu.
Ukiona kiongozi yeyeto anaejificha kwenye dini au uzalendo feki wa kuvaa maskafu ogopa sana huyo ni hatari sana.
 
Bahati nzuri Ruto hana mamlaka na nguvu alizokuwa nazo Moi kutokana na KATIBA MPYA ya Kenya.
Pamoja na kuwepo kwa Katiba hiyo mpya Kenya, lakini kiongozi kama ni mhuni haiwezi kumzuia kuisigina katiba hiyo.
Mtu poa kama Uhuru Kenyatta mwenyewe aliipuuza katika mambo kadhaa aliyofanya wakati wa utawala wake.

Ruto ni jambazi, ngoja tuone atakavyojizuia kuisigina katiba hiyo.

Huyu tayari anayo historia ya uovu katika uongozi wake. Kuna watu kama akina Jacob Juma na wale mashahidi wa ICC waliopotezwa wakihusishwa na uovu wake.
 
Kenya wanatakiwa kuwa makini Sana na huyu jamaa Urais wake unaweza kuwa Kama wa Magufuli alivyofanya Tanzania

Naweka huu uzi ambao utakuwa kumbukumbu miaka 3 mpaka 4 ijayo Mara tu atakaposimika watu wake kwenye system zote za nchi.

Ruto sio kiongozi kwa mtazamo wangu bali ni mtawala.

Ruto,Trump na Magufuli wana sifa moja ya kuwa watawala Kama ambavyo Kikwete, Uhuru na Obama walivyokuwa viongozi.
Kwani akiwa kama magufuli si ndio vizuri? Nyie madhulumati wa umma ndio mnaona ni ubaya kiongozi kua na msimamo kutetea umma badala ya wala rushwa na wafanyabiashara wakwepa kodi na wafanya magendo.
 
Kenya wanatakiwa kuwa makini Sana na huyu jamaa Urais wake unaweza kuwa Kama wa Magufuli alivyofanya Tanzania

Naweka huu uzi ambao utakuwa kumbukumbu miaka 3 mpaka 4 ijayo Mara tu atakaposimika watu wake kwenye system zote za nchi.

Ruto sio kiongozi kwa mtazamo wangu bali ni mtawala.

Ruto,Trump na Magufuli wana sifa moja ya kuwa watawala Kama ambavyo Kikwete, Uhuru na Obama walivyokuwa viongozi.
Yaani Kikwete unamuweka kuwa kiongozi? Kumbuka si kila mwanasiasa anaweza kuwa kiongozi ila kila kiongozi anaweza kuwa mwanasiasa
Tafakari!
 
We jamaa naanza kuwa na wasiwasi na wewe, hivi unadhani Kenya ni Tanzania?

Wakenya wapo mbali kimifumo kutushinda sisi...

Kwa taarifa yako Wakenya wamempata Hichilema wao waliyekuwa wanamsubiri kwa hamu.

Kenya Rais hawezi kuiweka mihimili mingine ya serikali mfukoni mwake...

Mahakama ziko huru..... Wewe imagine mshindi wa urais ameamuliwa mahakamani kiuwazi kabisa.

Bunge liko huru, tena lina uwiano mzuri wa chama tawala na chama pinzani..

Baraza la Seneti, hili nalo lina uwiano mzuri wa chama tawala na ponzani...

Sasa mpaka hapo utasemaje Rais atakuwa dikteta? Kwa jinsi mifumo yao ilivyo thabiti ni ngumu sana.
Huyu ni mpuuzi tu, anafikiri Kenya rais anaweka mifumo mfukoni kama yule kichaa alivyofanya na sisi watz tukakaa kimya km makondoo. Shenzi type! Tuliongozwa na mwehu!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wakikuyu ndio wengi so upande wanaochagua unapata almost 30% ya kura zote. So kama sio ukabila wa WAKIKUYU Raila angekua ikulu maana tukiwa wakweli tu hivi Rigathi na Ruto kwa ufisadi wote ule walifaa kuwa Viongozi?

Huu Uzi tutakuja kufukua December, watu watamlilia uhuru arudi!! Ruto ni failure kote alikopita.

Halafu mbona Ruto sio Mkikuyu? Mgombea wa Uhuru ambae ndio Kiongozi wa hao Wakikuyu alikuwa Odinga

Sasa kama walikataa chaguo la Uhuru ambaye ndio mkikuyu mwenzao wakachagua Ruto wa kabila tofauti utasemaje ni wakabila?
 
Ni bora awe mtawala lakini amalize matatizo ya wa Kenya hasa njaa. Nimesikiliza hotuba yake juzi alipozungumzia kushusha bei ya mbolea na kuisambaza ndani ya wiki moja kuanzia sasa nikagundua huyu mwamba hapendi mambo ya kuchelewa chelewa ni kama JPM, na ninadhani pia watu wa namna hii huwa hawapendi kukwamishwa.

Watakao jaribu kumkwamisha huyu mwamba ndio watauona ubaya wake. Kwa ile hotuba yake nilimuona JPM ndani yake.
 
Majizi ya Nairobi yatakula kipigo cha mbwa kachoka
 
Back
Top Bottom