Mkuu haya ni madhara ya viongozi kuwaapuuza na kuwasahau wananchi kwa muda mrefu. Nchi ikishaingia kwenye stage ambayo wananchi wanakinukisha, basi kuwatuliza tena inakuwa ni vigumu kwani watu wenye njaa na hali mbaya ya maisha, wanakuwa na frustrations. Sisi wengine hapa Tanzania huwa tunapiga kelele kutaka mabadiliko kabla wananchi hawajaamka kutoka kwenye usingizi waliolala. Nakupia nchi kama Tanzania ikilipuka kuja kutulia inachukuwa muda mrefu sana. Angalia nchi zote zilikuwa na madiktekta na wakaondolewa kwa nguvu ya umma, hazitulii kwa haraka. Na hata zikitulia, cheche ndogo tu inaweza kulipua tena mambo.