Ruto: Niliwapa Fursa zote Gen Z Ili tufikie muafaka wameshindwa kuzitumia wakijidai wao ni zaidi, sasa Basi!

Wamesema niondoe Finance Bill nami nimeiondoa, Nimewaita tukutane wanasema wao hawana Viongozi tukutane X, nimeenda huko X wote wamenikimbia, sasa Wanataka nini zaidi?

Nasema sasa imetosha hatuwezi kuendelea namna hii

Chanzo: Citizen TV
Watamuondoa ni suala la muda tu
 
Ifike sehemu waheshimu mamlaka
Mkuu haya ni madhara ya viongozi kuwaapuuza na kuwasahau wananchi kwa muda mrefu. Nchi ikishaingia kwenye stage ambayo wananchi wanakinukisha, basi kuwatuliza tena inakuwa ni vigumu kwani watu wenye njaa na hali mbaya ya maisha, wanakuwa na frustrations. Sisi wengine hapa Tanzania huwa tunapiga kelele kutaka mabadiliko kabla wananchi hawajaamka kutoka kwenye usingizi waliolala. Nakupia nchi kama Tanzania ikilipuka kuja kutulia inachukuwa muda mrefu sana. Angalia nchi zote zilikuwa na madiktekta na wakaondolewa kwa nguvu ya umma, hazitulii kwa haraka. Na hata zikitulia, cheche ndogo tu inaweza kulipua tena mambo.
 
Hatari sana 😳
 
Shida ya Kenya ni moja tu, wa Kikuyu na wa Luo hawa wanadhani wengine hawana haki ya kutawala. Ndio wanachochea hizi fujo mambo ya Finance Bill ni sababu tu ya kutokea lakini agenda kubwa kuliko hivyo.
 
Kwakweli hawaeleweki, ili madai yao yasikilizwe na siku za mbeleni wangekua na msimamo wa vitu wanavyopigania.

Wanapewa hiki wanasema wanataka wanataka na kile.
Tatizo la viongozi kujisahau kwa muda mrefu. Kinachotokea sasa hivi ni wingi wa vijana wasio na kazi kutoa frustration zao. Ni ngumu sana kumtuliza kijana asiye na future na mwenye njaa na mbaya zaidi wengi ni ma-jobless. Tukiwaambia CCM walete mabadiliko kabla mambo hayajawa mabaya wanatoa kebehi. Utekaji wanasema ni ''drama''. Tozo kubwa wanaita ''vitozo''. Tukilalamika wanasema ''tuhamie Burundi''. Machinha wakilalamika kufukuzwa wanaambiwa ''hivi mtu unafanyaje umachinga mpaka mvi zinatoka''. Tafakarini!
 
Kuna kitu cha kujifunza hapa, hii inaonesha viongozi watangulizi wa nchi za Afrika walivyo na Kwa upekee kabisa Kenya.
Gen-Z wanaweza kutulia kabisa viongozi wa Kenya wakiacha unafiki na usaliti wa unaosukumwa na uchu wa madaraka na siasa za kitabaka kwenye masuala ya kitaifa.

Nina hakika Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, Rails Odinga wakiangalia maslahi ya Taifa lao wanaweza kuwaelewesha Gen-Z njia sahihi zaidi. Siasa za namna hii ni siasa za hovyo sana kwa Taifa.

Mungu awavushe salama ndugu zetu Wakenya.
 
GenZ hawataki yeyote katika hao watatu. Katiba Mpya mkononi mwa wahuni Ni shida
 
Back
Top Bottom