Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Watu sita wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha Lumalu kata ya Upolo - Kilosa wilayani Nyasa kuanguka katika mteremko wa Chunya wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.
Waliofariki kati yao ni walimu wanne wa shule ya msingi Lumalu ya mkoani humo, Mfamasia mmoja na dereva wa gari hilo walilolitumia kuelekea Nyasa katika shule ya sekondari Limbo, kikazi.
Akizungumza katika eneo la ajali, Salumu Ismail, Katibu Tawala Wilaya ya Nyasa, amewashukuru wananchi kwa kujitokeza katika eneo ilipotokea ajali na kutoa msaada.
Amewaomba ndugu wa marehemu kwenda kupima DNA kwa ajili ya utambuzi wa miili hiyo ambayo imehifadhiwa katika hospitali ya Mbinga mkoani humo.
Ajali hiyo imetokea leo Desemba 28, 2024 ambapo chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
TBC