Ruvuma: Ajali yaua Watu 6 wakiwemo Walimu 4 wa Shule moja

Ruvuma: Ajali yaua Watu 6 wakiwemo Walimu 4 wa Shule moja

View attachment 3187039
Watu sita wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha Lumalu kata ya Upolo - Kilosa wilayani Nyasa kuanguka katika mteremko wa Chunya wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.

Waliofariki kati yao ni walimu wanne wa shule ya msingi Lumalu ya mkoani humo, Mfamasia mmoja na dereva wa gari hilo walilolitumia kuelekea Nyasa katika shule ya sekondari Limbo, kikazi.

Akizungumza katika eneo la ajali, Salumu Ismail, Katibu Tawala Wilaya ya Nyasa, amewashukuru wananchi kwa kujitokeza katika eneo ilipotokea ajali na kutoa msaada.

Amewaomba ndugu wa marehemu kwenda kupima DNA kwa ajili ya utambuzi wa miili hiyo ambayo imehifadhiwa katika hospitali ya Mbinga mkoani humo.

Ajali hiyo imetokea leo Desemba 28, 2024 ambapo chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

TBC
View attachment 3187042
View attachment 3187043
Ngoma imesanda na kuripuka!

Hapo siyo rahisi mtu kusevu, aliyejeruhiwa ama kuzimia kwa mshituko anakuja kumalizwa na moto.

Ndiyo maana ndugu wanahitajika kwenda kupima vinasaba, wameteketea kwa kuungua na kupoteza utambulisho.
 
Waafrika hasa watanzania wana kufa sana kutokana na ujinga, uzembe na kuishi kwa mazoea.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja. Usitishike na maneno ya wapumbavu wachache wanaokubeza na kukudhihaki. Ni kweli tupu waafrika tunaangamia kwa upumbavu wetu lakini hili watu hawataki kulisikia kabisa.

Mfano kwnye vyombo bya moto unakuta dreva amelewa et anaendesha gari au pkpk. Barabara mbovu analazimisha spind kubwa hata anachowahi hakijulikani. Magari hayakaguliwi kuna kama yanafaa kw safari au laa ya ani ni ujinga ujinga tu
 
Ajali nyingi hapa Tanzania zinatokana na ujinga, uzembe na upumbavu wa Raia.

Mijitu haitii na wala haizingatii sheria za barabarani, ndio maana inakufa kama kuku.
 
Back
Top Bottom