View attachment 3161491
Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma limetoa taarifa ya mauaji yaliotokea tarehe 14.11.2024 majira ya saa 12 asubuhi katika kitongoji cha Mbilo, kijiji cha Kizuka ,kata ya kizukatarafa ya Muhukuru wilaya ya Songea ,mwanamke aliyefahamika kwa jina la Ponsiana Dastan Kapinga (22)ameua kwa kupigwa na kitu kizito kichwani juu ya jicho la kushoto hadi kichwa kubonyea na mumwe aitwaye Mrtin Hyera baada ya kunyimwa tendo la ndoa
Kabla ya mauaji wawili hao walionekana alfajiri wakikimbizana mwanaume akiwa ameshika mpini wa shoka ndipo alipoenda kutekeleza mauaji hayo.
na baada ya kufanya mauaji hayo mtuhumiwa (mume) alimpigia simu shangazi yake Pulina Nchimbi na kumjulisha amemuua mke wake kwasababu ya kumnyima unyumba kwa muda mrefu. baada ya kutoa taarifa kwa shangazi yake akakimbia jeshi la polisi linaendelea na msako katika maeneo mbalimbali.