Rwanda inatumia mfumo wake wa ulinzi wa angani, Iron Dome

Yeah, Uganda wanazo chache, ila wakiwa na pilot wazuri sisi wenye J7 za kichina sioni tukitoboa kwenye dog fights hata wakiamua kufanya ground attack pia.

Sidhani kama tutafika huko kwenye j17 anytime soon. Pale ngerengere naona zimepark j7 za mchina tu.. i doubt if we do we have anyother variant?
 
Iron dome hao wanarusha wamevaa kandambili?na hapo wanaulizana tunaitupa vipi.
Hao wanakijiji wanaweza kupigana vita hao.
Iron dome inatupwa toka nyumba ya udongo.
Congo ni wajinga sanaa, wana uwezo kukifurusha hiyo kanchi dk 2 tu wamelala.
 
Bwana mdogo, ethics tu wengine zinatubana. Ila hujui chochote!
Mkuu sidhani kama ethics zinakataza kutaja aina na models za fighters na air defenses tulizonazo.

Nadhani kutaja location na mbinu inaweza ikawa mbaya ..ila model za ndege, au vitu kama submarines kama zipo au hazipo sioni kama ni kinyume cha ethics.
 
Kwa ufupi fahamu tupo vizuri!

Kelele za mitandaoni ni kawaida ya mtanzania kuongea.
 
Kwa ufupi fahamu tupo vizuri!

Kelele za mitandaoni ni kawaida ya mtanzania kuongea.
Hata Wacongoman wanasema jeshi lao liko vizuri..hakuna anae admit jeshi lake liko weak.

Kutuaminisha uzuri wa jeshi, tuletee facts. Uganda wa Sukhoi 30 wala hawajazifanya siri. Kwao ni jambo la kawaida. Sisi tuna J7 variant ya Mig 21. Na ndizo tunazoziona, unasemaje tuko vizuri
 
Tuna Chinese J-7G na old Soviet relics, Mig-21 Fishbed. Nina mashaka na airworthiness ya Mig-21 maana zimekula chumvi na ukizalimisha kuzitumia baada ya overhaul utaua sana marubani. Na J-7 ni copy ya Mig-21.

Huhitaji kuwa na rubani mzuri ukiwa na Su-30 variant yoyote anapigana na J-7, rubani kiazi kuliko wote kwenye mafunzo anaweza kipiga hicho kindege bila kuumiza kichwa.

Mig-21 na J-7 zina RCS kubwa hivyo zitaonekana haraka kwa Sukhoi, hazina powerful radars kwahiyo zitaonwa kabla hazijaona adui. Variant ya J-7 inayojitahidi inabeba PL-7 AAM ambayo maximum range ni 14km tu (sababu radar haioni mbali), wakati Su-30 inaweza ona mbali na AAM yake ya range fupi ni 40km, zipo za zaidi ya 100km ila najua Uganda hawawezi uziwa.

Injini ya J-7 ni moja na haina nguvu kama twin engines za Sukhoi kwahiyo turn rate, speed, climb rate ya Su-30 ni kubwa alafu ina g 9+ ambazo hata rubani mara nyingi huwa hamudu kufika.
Kwenye dogfight J-7 haiambulii kitu, vilevile autocanon ya Mig ina nguvu zaidi.

Kwenye ground attack ndio kabisa Su-30 ina option nyingi za rockets, free fall bombs, smart munitions, air to surface missiles sababu ina carrying capacity kubwa.

Range yake pia kubwa. Na hizi hazitakiwi zilinganishwe, moja ni kama second generation, nyingine fourth generation.
 
Nilikuwa natafuta comment yako kwenye hizi mambo.

Nielimishe kidogo mkuu, shell na missile tofauti nin
 
Mkuu anatuambia tuko vizuri....hoja nyepesi nyepesi bila kuzi backup na data.
 
Nilikuwa natafuta comment yako kwenye hizi mambo.

Nielimishe kidogo mkuu, shell na missile tofauti nin
Kwa lugha nyepesi, ni Kombora vs Mzinga.

Kombora/missile lina continuous propulsion kwa kutumia rocket au jet engine, baada ya kufyatuliwa, linamfumo wa ndani wa kuliendesha zaidi.

Mzinga/shell hii ni kama risasi kubwa. Mlipuko wa mwanzo wakati wa kufyatuliwa ndio unaoipa mwendo kuelekea kwenye target.
 
mito natumaini umeelewa
 
Asante nimekuelewa mkuu, tena umeeleza kwa lugha nyepesi hata sisi tusiowataalam tumeelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…