MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Wewe unamsifia Dikteta!!??.
Ni ujinga kuingiza udikteta katika masuala la imani, imani imo moyoni mwa watu.
Adhana ya kiislamu ni nasaha ya kiimani pia mbali na wito wa kuwajulisha watu muda wa swala.
Kupinga utolewaji wa adhana ni kupinga mafundisho ya dini ya kiislamu, adhana haijaanza leo, imeanzishwa na mjumbe wa Mungu Mwanzilishi mtukufu wa Dini ya kiislamu Mtume Muhammad (saw), hivyo kwa maneno mengine kuzuia utolewaji wa adhani ni kupingana na takwa la Mungu kwa mujibu wa Uisilamu.
Tutakaa hapa tukibishana na kuvutana bure na hatutafikia suluhu ila ninachokueleza ni hichi;--
"Kama adhana ni maagizo na maneno ya Mungu na Kagame au yeyote katoa maamuzi ya kuzuia maneno hayo yasitamkwe inavyopaswa ni kiumbe wa Mungu basi Mungu mwenyewe ndiye hakimu"
Tutarudi hapa na tutajulishana matokeo tuombe Mungu atupe uhai tu.
Ni makelele, sio kila mtu anahusiana na uislamu, tumieni simu kupigishana hayo makelele.