Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Adhana ni sehemu miongoni mwa sehemu katika ibada ya swala ya kiisilamu, Adhana ni Lazima itolewe kwa sauti na Adhana haina mbadala kwa njia yoyote kwani yenyewe inabeba ujumbe wa kiroho unaomuhamashisha mtu aache mambo mengine na akaswali, adhana ni wito wenye "spiritual admonitions" and can't be replaced by anything else.

Adhana mbali na kuamsha na kuwataarifu wenyeji juu ya muda wa ibada lakini pia inawajulisha wageni kwamba msikiti upo wapi na hivyo kuwaunganisha Wageni waisilamu na ndugu zao wenyeji wa kiislamu katika Swala nk, Uisilamu ni zaidi ya kuswali msikitini na kuondoka.

Shida iliyopo Rwanda ni 90+% ni Christians na wachache waliobaki ni Muslims hivyo utaona nguvu ya Udini imeshawishi kuwepo na hilo katazo hii ni tofauti na Tz ambapo kuna angalau 50/50% Muslims na Christians ambapo tumejengwa kuvumiliana katika masuala ya imani.

Kuzuia utoaji wa adhana ni pigo katika imani ya dini ya kiisilamu.
Mbona wakati anapitisha sheria ya kuwabana WaKristo hatukuona hoja yako hii ya ubaguzi wa kidini?. Mfano
1. Ni marufuku kulala na kuamka kwa Mkristo kisha kesho yake kujiita nabii au mtume mwenye kumiliki kanisa X bila kuwa na angalau shahada ya Theologia

2. Marufuku makanisani kutumia viongeza sauti wakati wa ibada zao maana ni kelele kwa wengine.

Niishie hapo, usije na hoja nyepesi kuwa Kagame ana ubaguzi wa Kidini bila kuwa na mifano anuai.

PK hana shida kama hao ndugu zetu wanaobagua wenzeo huko visiwani kisa tofauti za kiimani. Yeye moja ni moja kwa wote
 
Saudi Arabia pia, walishakataza Adhana saa 10:50 usiku washaanza makelele, yaani kero kuu, yaani ni kero kubwa, watu hawalali, ni makelele utafikiri miji ya matarumbeta. Ni kero sanaa sanaa.

Saudi Arabia pia, walishakataza Adhana saa 10:50 usiku washaanza makelele, yaani kero kuu, yaani ni kero kubwa, watu hawalali, ni makelele utafikiri miji ya matarumbeta. Ni kero sanaa sanaa.

Bado sisi sasa
 
Huku kwetu iwe viseversa makanisa na hizi ministry baadhi kwa kweli mnaboa sana haiwezekani uwalazimishe watu kusikiliza mambo yako hata kama ni mahubiri kila mtu ana haki ya kupata utulivu makelele saa nane za usiku sijui kuna ibada ya kufungua vifungo mnasumbua watu buree Ningeshauri Serikali Mama kama unapita hapa piga marufuku matumizi ya Speakers kubwa kwenye makazi ya watu mnaboa mno WATUMISHI NA MITUME MJIHESHIMU TAFADHALI[emoji122]
 
Adhana ni sehemu miongoni mwa sehemu katika ibada ya swala ya kiisilamu, Adhana ni Lazima itolewe kwa sauti na Adhana haina mbadala kwa njia yoyote kwani yenyewe inabeba ujumbe wa kiroho unaomuhamashisha mtu aache mambo mengine na akaswali, adhana ni wito wenye "spiritual admonitions" and can't be replaced by anything else.

Adhana mbali na kuamsha na kuwataarifu wenyeji juu ya muda wa ibada lakini pia inawajulisha wageni kwamba msikiti upo wapi na hivyo kuwaunganisha Wageni waisilamu na ndugu zao wenyeji wa kiislamu katika Swala nk, Uisilamu ni zaidi ya kuswali msikitini na kuondoka.

Shida iliyopo Rwanda ni 90+% ni Christians na wachache waliobaki ni Muslims hivyo utaona nguvu ya Udini imeshawishi kuwepo na hilo katazo hii ni tofauti na Tz ambapo kuna angalau 50/50% Muslims na Christians ambapo tumejengwa kuvumiliana katika masuala ya imani.

Kuzuia utoaji wa adhana ni pigo katika imani ya dini ya kiisilamu.
Sipingi madhumuni ya adhana. Tatizo ni kule kuhusisha wale wasiohusika. Kama ujirani wote ungekuwa ni Waislamu pekee, hapo ingekuwa sahihi kuwachokonoa wale Waislamu kaidi au dhaifu wanaotaka kuendelea kuvuta shuka. Hizo "spiritual admonitions" zitakuwa zinamfika mlengwa na hazimsumbui asiyehusika anayetaka ku-maximize usingizi wake kabla ya kuamka kwenda kupambana na mahitaji ya maisha. Kwa vitu ambavyo haviwezi kutekelezwa msikitini, njia mbadala itafutwe ya kuwafikia walengwa ambayo siyo kero kwa wasiohusika. Kwa mfano, mchana unaofuata ujumbe unaweza kutumwa kwa hao wakaidi ukiwakanya wanayofanya na kuwataka waongoke. Mradi tu asiyehusika habugudhiwi. Kwa maneno ya Rais Mstaafu Mwinyi, "Mbebaji hatabeba mzigo usiomhusu".
 
Kwa hili Rwanda nawapongeza sana, zile kelele za alfajiri zinakera sana.

Hii ni Taharifa ya BBC...

Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo.

-

Mwezi uliopita mamlaka ilipiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye misikiti asubuhi na mapema, ikisema kuwa ilikiuka sheria za uchafuzi wa kelele ambazo zinakataza kelele zaidi ya decibel 55 wakati wa mchana na decibel 45 usiku katika maeneo ya makazi.

-

Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu. View attachment 2188599

Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app
Hii habari ya 2018 na sio misikiti tu mpaka makanisa yamefungwa
Screenshot_20220416-075553.jpg
Screenshot_20220416-075757.jpg
 
Kama hoja ndo kama yako naunga mkono uamzi wa Kagame. Hapa duniani kila jamii au imani ina Mungu wao ambaye hafanani na huyo wa kwako au wa mwingine. Hivyo huo utukufu unautambua pekee yako na sio wote. Hata upande wa makanisa alishapiga ban watu kujifanyia watakavyo. Kongole Prezida Kagame

Wewe unamsifia Dikteta!!??.
Ni ujinga kuingiza udikteta katika masuala la imani, imani imo moyoni mwa watu.

Adhana ya kiislamu ni nasaha ya kiimani pia mbali na wito wa kuwajulisha watu muda wa swala.

Kupinga utolewaji wa adhana ni kupinga mafundisho ya dini ya kiislamu, adhana haijaanza leo, imeanzishwa na mjumbe wa Mungu Mwanzilishi mtukufu wa Dini ya kiislamu Mtume Muhammad (saw), hivyo kwa maneno mengine kuzuia utolewaji wa adhani ni kupingana na takwa la Mungu kwa mujibu wa Uisilamu.

Tutakaa hapa tukibishana na kuvutana bure na hatutafikia suluhu ila ninachokueleza ni hichi;--

"Kama adhana ni maagizo na maneno ya Mungu na Kagame au yeyote katoa maamuzi ya kuzuia maneno hayo yasitamkwe inavyopaswa ni kiumbe wa Mungu basi Mungu mwenyewe ndiye hakimu"

Tutarudi hapa na tutajulishana matokeo tuombe Mungu atupe uhai tu.
 
Mliongea na Mungu yupi hivyo? .Mungu yupi alikwambia hivyo sababu kuna Miungu tofauti na kila mtu huabudu Mungu wake huyo Mungu wake atakavyo
Wewe uliongea na miungu yote watu wanayoiabudu wakakwambia hilo? Sababu Mungu wako sio wangu na nisimtambui na wewe wangu humtambui
Mathayo 6 : 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
 
Mathayo 6 : Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
Baltimayo kwenye Bibliia alisali kwa kupiga makelele miyowe Yesu mwana wa Daudi unirehemu .Maombi yake yakasikilizwa na Yesu akamponya
 
Adhana ni sehemu miongoni mwa sehemu katika ibada ya swala ya kiisilamu, Adhana ni Lazima itolewe kwa sauti na Adhana haina mbadala kwa njia yoyote kwani yenyewe inabeba ujumbe wa kiroho unaomuhamashisha mtu aache mambo mengine na akaswali, adhana ni wito wenye "spiritual admonitions" and can't be replaced by anything else.

Adhana mbali na kuamsha na kuwataarifu wenyeji juu ya muda wa ibada lakini pia inawajulisha wageni kwamba msikiti upo wapi na hivyo kuwaunganisha Wageni waisilamu na ndugu zao wenyeji wa kiislamu katika Swala nk, Uisilamu ni zaidi ya kuswali msikitini na kuondoka.

Shida iliyopo Rwanda ni 90+% ni Christians na wachache waliobaki ni Muslims hivyo utaona nguvu ya Udini imeshawishi kuwepo na hilo katazo hii ni tofauti na Tz ambapo kuna angalau 50/50% Muslims na Christians ambapo tumejengwa kuvumiliana katika masuala ya imani.

Kuzuia utoaji wa adhana ni pigo katika imani ya dini ya kiisilamu.
Sioni msingi wa kusumbua watu wengine Kwa makelele Kwa interest ya dini Moja!Uhuru wa mtu unapoishia ndipo wa mwingine unapoanzia!
Inaweza kuwa justified within community ya waislam pekee!
 
Sioni msingi wa kusumbua watu wengine Kwa makelele Kwa interest ya dini Moja!Uhuru wa mtu unapoishia ndipo wa mwingine unapoanzia!
Inaweza kuwa justified within community ya waislam pekee!

"Uhuru wa kutoa adhana nk, unapoishia ndipo uhuru wa wengine unapoanzia", ----you are right and that's the best way to put it.
 
Back
Top Bottom