Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri


Ni makelele, sio kila mtu anahusiana na uislamu, tumieni simu kupigishana hayo makelele.
 


Mkuu, Huwezi kupindisha mafundisho na norms za dini ya kiislamu upendavyo, dini hii tayari imeishawekewa misingi yake na Mtukufu Mtume Muhammad (saw), kwamba hakuna mbadala wa adhana, kama.mbadala ungalikuwepo basi Mtume (saw) angeuainisha, mfano kabla ya kuswali inatakiwa kutawadha lakini kama maji ni shida au kutokana na hali ya mtu ilivyo kwa wakati huo imeruhusiwa "Kutayyamamu" huo ni mbadala wa kutumia maji katika kutawadha, kwa upande wa adhana hakuna mbadala wake.
 
Ni makelele, sio kila mtu anahusiana na uislamu, tumieni simu kupigishana hayo makelele.


Hapa tunajadiliana na watu wenye akili na hoja kama huna hoja you better stand aside and learn, if speaking is gold being quiet is Pearl .
 
"Uhuru wa kutoa adhana nk, unapoishia ndipo uhuru wa wengine unapoanzia", ----you are right and that's the best way to put it.
Umeniquote nje ya context!Kauli ya uhuru wa mwingine unapoishia ndipo wa mwingine unapoanzia humaanisha mtu mmoja asiwe na uhuru kupitiliza mpaka kuathiri uhuru wa mwingine!
Fikiri na Mimi nitumie uhuru huo,wakati wa adhana nami nifungulie maspika yangu na kuhamasisha watu waamke wakafanye mazoezi,mwingine afamye hivyo hivyo,kutakalika hapo mtaani?
Mimi nilikuwa nakaa Karibu na msikiti hapo kahama mjini,nilikuwa nimefikia Lodge na bahati mbaya nilikuwa nimemwambia rafiki yangu anifanyie booking ya lodge wiki nzima!
Nilikaa siku 2,nikahamia huko Phantom nje ya mji!Sababu ni hayo makele!
 
Kila mtu ana uhuru wa kuabudu, anachokitaka ila tu asivunje katiba ya nchi. Tanzania sio Rwanda,
Ndio maana korona Mungu kawaponya nayo lakin nchi zingine Kuna huzuni, nchi na nchi hazifanani, na mtu na mtu hawafanani. Kila mtu ana Neema tofauti Kwa Mungu.
 
Hapa tunajadiliana na watu wenye akili na hoja kama huna hoja you better stand aside and learn, if speaking is gold being quiet is Pearl .

Usipangie watu namna ya kujadili, ndio kama hivyo mnapigia watu makelele ya uislamu ambayo hawahusiani nayo.
Ni kama ule ujinga kule zenji wa kuchapa viboko wanaokutwa wakila hata wasio waislamu au hawana hata mpango huo kwenye maisha.
Fanyeni yenu bila kusumbua watu, mna matatizo sana ya kulazimisha watu huo uislamu.
Rwanda sio nchi ya kidini kama kwa wale wenye hiyo dini huko uarabuni.
 
Tuambiane ukweli
Sio busara kuwapigia watu makelele kila alfajiri tena wasio wa imani yako.

Tuambiane ukweli sio busara makanisa ya mtaani hasa walokole kuweka mifumo ya mziki kwenye makanisa yao alaf wanafungulia sauti kubwa kifupi tunakwazana sana wakuu.

Mungu hahitaji kipaza sauti wala spika ili kusika maombi yako.

Watu wa imani wamegeuka kero kwa wenzao hii sio sawa, tuabudu bila kuudhi wengine.

Hata wenye mabaa wanatukwaza sana mtu anapiga mziki usiku mnene watu wamepumzika.

Serikali ichukue hatua
 
Enzi za Yesu/Muhammad haya maspika hayakuwepo, je ibada Zilikua hazifanyiki?Mungu alikua hasikii maombi Yao?

Kitu gani kilitokea hapa katikati mpk haya maspika yakaanza kuwekwa kwny makanisa/misikiti?
 
Mpk hapo sijaona umuhimu wa spika tena.
 
viongozi wanatofautiana kule Dodoma kwenye kumuaga màgufool Uhuru Kenyatta alisimamisha hituba yake kwa sekunde kadhaa kuipisha adhana
 
TEna saivi Kuna wakimbizi kutoka Afghanistan Na Syria watatua apo
Ndio vzr,watengenezewe Guantanamo bay yao Kule visiwa vya iwawa.

Na bado Denmark itaingia deal jingine na Rwanda la style hio ya kuwapokea wahamiaji.
 
Ukiona watu wanaanza kumchukia Mungu mjue mwisho wa dunia unakaribia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…