Mifano Yako sio hai!Hayo yote uliyotolea mifano hayafanani na hoja husika ya kupigia watu makelele!Mtu aseme aweke Spika kubwa nyumbani Kwake halafu afungulie mziki mkubwa usiku kucha halafu aachwe kisa Yuko huru?
Ndio maana hata club za usiku Zina utaratibu wake kuhusu masuala ya sauti!Sema tu rushwa imetawala na watu wanapiga mziki usiku kucha kwenye maeneo ambayo hayana sound proof!
Hizi dini zinavumiliwa tu na kelele zao wanazowaletea watu majumbani,na wao wanatakiwa kuelewa sio haki Yao Bali ni favour tu!
Na haya mambo Yako uswahilini tu,nenda Kwa mitaa ya matajiri huko uone kama Kuna hayo makelele!
Nadhani tuishie hapa kwani tunazunguka tu.
Adhana sio kelele kama jinsi mlio wa honi, gari, mbwa, jogoo anayewika, radi nk, honi, gari, mapikipiki, watoto, jogoo nk, milio yao inayosababu na faida katika jamii--- labda uniambie hakuna sababu na vinatoa milio kiwendawazimu!!
Adhana ni mwito kwa waumini kwenda kufanya ibada, ibada ni mafundisho ya hulka njema (morals) ---hutanielewa kama wewe ni ethiest, naamini wewe unaamini Mungu.
Imani za dini ndizo huweka misingi ya morals kwa watu na ndio maana utasikia marakadhaa viongozi wa kisiasa wakiwahimiza viongozi wa kidini kuwasaidia kuwajenga waumini wao kimaadili nk, ili kujenga jamii bora, hapo sasa utaona dini ina take part katika kujenga jamii, utawala kuzuia adhana ni kuweka kizingiti indirectly kwa dini kujenga hulka kwa waumini ambao ni sehemu ya jamii ya watu wote, unless tukubaliane kwamba nchi husika inafuata misingi ya Communism hapo ni kesi nyingine.
Ninachotaka kukuambia ni hiki; Dini ni imani ndani ya jamii na utawala bora ni ule unao Compromise imani, utamaduni, mila nk, za jamii husika ili kuleta amani, maelewano kati ya jamii na utawala nk.
Chuki ya adhana isiwapofusheni mkawa shortsighted msione mbali zaidi ya hapo juu ya kitu kinachoweza kutokea, suala hili ni mtambuka.