Bro rwanda ni nchi ndogo sana,kigoma pekee ni kubwa hivyo madarasa kwao ni kitu kidogo tu
Sent from my SM-N960F using
JamiiForums mobile app
Ishu sio udogo au ukubwa wa nchi, ishu ni maono ya viongozi, nchi yao wanataka iwe wapi, mfano ndani ya miaka ishirini na hatua gani watazichukua kutimiza maono yao.
Ukimuweka Kagame Tanzania na hawa viongozi wa Tanzania ukiwapeleka kuongoza Rwanda mambo yatakuwa kinyume.
Mfano kwa TZ, shida za maji, umeme, ajira, miji iliyopangwa, afya, elimu, makazi, miundombinu, kilimo, uvuvi, ufugaji, masoko, mazingira ya uwekezaji, biashara, kodi zenye uhalisia, wezeshi, kuondoa urasimu, rushwa.
Tungekuwa na viongozi makini kwa miaka yote 60 hadi sasa tungetakiwa tuwe tumepiga hatua kubwa sana.
Ila sisi tunaendelea kuchagua watu wasio na uwezo wala weledi vigezo vyetu ni vya kisiasa, kiukabila, kiukanda, kijinsia, kidini, umaarufu, kusifia,mapambio.