Rwanda wanajenga kinu cha Nyuklia; sisi bado tuna maono ya kujenga madarasa miaka 60 ya uhuru

"Elimu ni ukombozi " wakati mwingine napata wasiwasi , kutokana na mambo yanayofanywa na wasomi wa nchi hii. Angali watu wenye PHD Tanzania , wanafanya mambo ya ajabu ajabu ambayo inafikia mahali naona elimu haina maana yoyote
Sifa moja kuu ya msomi ni Integrity, kuwa na PhD siyo kuelimika: Nadhani hili tuliweke sawa kabisa mkuu.
 
Sawa.....

Kwa hiyo NUCLEAR ENERGY ina source nyingine mbali na URANIUM?!!!Khaa 😳😳
 
Taratibu unaanza kujitambua, bado tu hujamjua mchawi ni nani, sisi wengine ambao tushamjua tunakusubili juu tuendelee na mambo makubwa zaidi. Nasema hivi sababu unaitaja CDM wakati haijawahi kushika nchi hata mwaka mmoja ktk hiyo miaka 60
 
Mkuu umeonja pombe leo siku ya Mwalimu Nyerere?.Hiyo hoja yako kati ya Marekani na Tanzania haieleweki.
Hoja yako umeijenga kwa kuangalia udogo wa Rwanda kama sababu ya wao kuendelea!

Nikakuukiza Kama sababu ya nchi kuendelea ni udogo wa nchi mbona TANZANIA Ni ndogo kwa marekani na hatuna Maendeleo kushinda Marekani!

Badala uje kujibu hoja unatokwa Hedhi Kama Mbuzi Jike.

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Sawa komredi...

Mathalani Rwanda watanunua hayo mafuta na hizo urani....probably kutoka humuhumu Afrika....

Ok mkuu
 
Unalinganisha na Marekani na Tanzania. Marekani ina miaka 240 ya uhuru wakati Tanzania ndio kwanza inakaribia miaka 60. Marekani ni taifa lenye watu wa kila aina kuna wayahudi, wahindi, wazungu mpaka wamasai wapo Marekani.

United States of America, ni muunganiko wa majimbo uliozaa Marekani. Tanzania ni nchi moja tu haundwi na muunganiko wa mataifa mbalimbali.
 
unawashwa wewe, unajua mikakati ya CHADEMA wewe?
Wewe mda wote upo unaangalia porn unTEGEMEA KUJULIA WAPI HIZO SERA?
 
Zanzibari ni Tarafa?
 
Kinu cha nyukria ndio maendeleo?
Na kama mojawapo ya sera mbadala ya maendeleo ya Chadema ni wananchi kushirikiana kutatua matatizo yanayowakabili wenzao na wanaonyesha mfano kwa kuchangia familia za makomandoo na kuwalipia faini wale wote waliojikuta katika matatizo wakati wakipigania chama chao? Kuna ubaya gani?

Amandla...
 
Bro rwanda ni nchi ndogo sana,kigoma pekee ni kubwa hivyo madarasa kwao ni kitu kidogo tu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app


Ishu sio udogo au ukubwa wa nchi, ishu ni maono ya viongozi, nchi yao wanataka iwe wapi, mfano ndani ya miaka ishirini na hatua gani watazichukua kutimiza maono yao.

Ukimuweka Kagame Tanzania na hawa viongozi wa Tanzania ukiwapeleka kuongoza Rwanda mambo yatakuwa kinyume.

Mfano kwa TZ, shida za maji, umeme, ajira, miji iliyopangwa, afya, elimu, makazi, miundombinu, kilimo, uvuvi, ufugaji, masoko, mazingira ya uwekezaji, biashara, kodi zenye uhalisia, wezeshi, kuondoa urasimu, rushwa.

Tungekuwa na viongozi makini kwa miaka yote 60 hadi sasa tungetakiwa tuwe tumepiga hatua kubwa sana.

Ila sisi tunaendelea kuchagua watu wasio na uwezo wala weledi vigezo vyetu ni vya kisiasa, kiukabila, kiukanda, kijinsia, kidini, umaarufu, kusifia,mapambio.
 
Umeme wa nyuklia ni gharama sana kwa mtumiaji .Rwanda hawana vya zo vingi vya kuzalisha umeme ndio maana wamejenga.
Sisi tuna vyanzo rahisi kibao vya kuzalisha umeme Tuna mito kibao yenye maporomoko tuna gesi tuna upepo kibao mikoa ya singida nk.tuna volcano zinazochemka ardhini kwa ajili ya thermal electricity nk hakuna haja ya kujisumbua kuwekeza kwenye nyuklia

Tatizo management ya huo mtambo wa nyuklia Nchi nyingi Zilizoendelea zimeshapata majanga kibao kuanzia Japan,urusi nk Rwanda tuwaomber lingine shughuli ni pevu ku dispose nuclear waste.Nchi Zilizoendelea zinahonga third world countries president s kutupa hizo nyuklia waste
 
Nilipigana vita ya Kagera hammy!
Baada ya hapo?

Umeshajenga chochote cha kuacha alama?

Au ukishapigana vita unakaa chini na kulalama hadi uingie kaburini?

Nawaza for the past 40 years (baada ya vita) uneshafanya nini kinachowarrant malalmiko kama mtoto mayai?
 
Wakijenga kinu wataimport madini ya Urani toka Tunduru Tz, kwahiyo bado ngoma droo mkuu. Rwanda haina Urani inajenga kinu, Tz tuna Urani hatuna kinu.
Afu wewe ni mjinga sijui unawaza kwa kutumia Nini. Haya afu watawauzia umeme kwa Bei ya juu. Bidhaa zao zitazalishwa kwa Bei ndogo Mana power sio ishu kwao.
Yaani unajifariji kumuuzia pamba anatengenezea nguo afu anakuja kukuuzia hizo nguo
 
Jamani Rwanda kutengeneza kinu cha nyuklia cha kuzalisha umeme ni jambo ambalo linaweza kuonekana ni jambo zuri kwa baathi ya watu ila Rwanda ni kama wilaya karika Ukanda wa Africa Mashariki.So I personally term having this Nuclear Plant as very dangerous act since any mistake of mismanagement of the plant will harm the whole East Africa.
 
Mwendazake amewaacha mataga wengi sana
Hahaa siasa za nchi hii kweli ni ngumu jambo limewashinda chama chenu unawasingizia Chadema.
Umenikumbisha mwendazake na kauli yake ya upinzani "wanatucherewesha".
 
Well done
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…