Rwanda yafunga Parokia 47 za Kanisa Katoliki

Rwanda yafunga Parokia 47 za Kanisa Katoliki

Nawaza sana nchi ndogo mnoo kama Rwanda ambayo kieneo ni ndogo kuliko hata mkoa wa Pwani hapa Tanzania (huenda kieneo haifiki hata nusu ya mkoa wa Pwani), inawezaje kuwa na nyumba rasmi za ibada maelfu kwa maelfu. Yaani kama Kanisa Katoliki pekee Rwanda lina Parokia zaidi ya 231 (Kanisa katoliki ni mfano mzuri zaidi katika kujipanga kiutarabu wa kujenga nyumba zake za Ibada), hizo ni nyingi mnoo katika eneo la nchi kama Rwanda. Mleta mada anaeleza mpaka sasa Rwanda imeshafungia zaidi ya nyumba za ibada 10000.

Kwa utiriri huo, tukubali tu, Afrika (Rwanda ikiwa ni mfano halisi) tuna shida kubwa mnoo kuhusu ulevi wa kidini, tumegeuza dini kuwa kishaka cha kulewa ili kujisahaulisha matatizo yetu.
 
Serikali ya Rwanda imezifunga Parokia 47 za Kanisa Katoliki kwa madai ya kukiuka kanuni na sheria za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ambayo imetolewa na Maaskofu wa Kanisa Katoliki, inasema kuwa suala la uhuru wa kuabudu limekuwa changamoto kubwa nchini Rwanda.

Ripoti hiyo inasema kuwa kati ya Parokia 231 zilizopo nchini humo, 47 tu ndizo ambazo zimefungwa kutoka katika Dayosisi tisa.

Hadi kufikia mwanzano mwa mwezi wa Septemba mwaka huu, Serikali ya Rais Paul Kagame ilikuwa imeyafunga Madhehebu na Misikiti takribani 10,000 kwa kile ilichokiita kukiuka sheria za nchi hiyo
Good kwa ajili ya kuepuka sampuli za kiboko ya wachawi na watu kutegea miujiza badala ya kazi
 
Serikali ya Rwanda chini ya Paul Kagame imezifunga Parokia 47 za Kanisa Katoliki kwa madai ya kukiuka kanuni na sheria za nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti ambayo imetolewa na Maaskofu wa Kanisa Katoliki, inasema kuwa suala la uhuru wa kuabudu limekuwa changamoto kubwa nchini Rwanda.

Ripoti hiyo inasema kuwa kati ya Parokia 231 zilizopo nchini humo, 47 tu ndizo ambazo zimefungwa kutoka katika Dayosisi tisa.

Hadi kufikia mwanzano mwa mwezi wa Septemba mwaka huu, Serikali ya Rais Paul Kagame ilikuwa imeyafunga Madhehebu na Misikiti takribani 10,000 kwa kile ilichokiita kukiuka sheria za nchi hiyo.

Misikiti mingi haina vyoo, ni michafu na makosa mbalimbali huku wakufunzi wake wakiwa hawana elimu dunia kitu ambacho utawala wa Kagame unasema ndio unasababisha kupotosha watu na kuleta machafuko. Ikumbukwe ilianza na walokole wote walikuwa wachungajinna manabii ambao hawana digrii ya dini walifungiwa na makanisa yao yakafungiwa.

65% ni Wakatoliki
9% Walokole
1% Waislamu

Uislamu ndio cult inayokuwa kwa kasi hapo Rwanda.

Wakati kagame anafunga makanisa ya walokole, baadhi ya Cult zilifurahia sana, zikafanya sherehe , sasa nazo cult zimefikiwa huku Makanisa yanayomwamini Yesu yakiwa yamejirekebisha na kuhubiri amani na mshikamano tofauti na cult!
 
Kagame msabato. Wasabato na wakatoliki ni maji na mafuta

Unauliza au unasema?

IMG_20241015_072450.jpg

Paul Kagame - Wikipedia

Acha kuchafua dini za watu kwa umburula wako.
 
Wakati walokole wanafungiwa sisi waumini wa "cult" tulipiga vigelegele, kumbe sisi ndio wachafu kuliko hao walokole, sema tu jamaa alikuwa anatuvutia kasi.

Hii dini yetu "tunayoita ya kwanza" tunajihesabia haki, tunajiiona sisi ndio waanzilishi wa wafuasi wa MESIAH, tumeamua kuwa standard unit ya ukristo wakati tunayohubiri na kutenda ni mbali mbali.
 
Serikali ya Rwanda imezifunga Parokia 47 za Kanisa Katoliki kwa madai ya kukiuka kanuni na sheria za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ambayo imetolewa na Maaskofu wa Kanisa Katoliki, inasema kuwa suala la uhuru wa kuabudu limekuwa changamoto kubwa nchini Rwanda.

Ripoti hiyo inasema kuwa kati ya Parokia 231 zilizopo nchini humo, 47 tu ndizo ambazo zimefungwa kutoka katika Dayosisi tisa.

Hadi kufikia mwanzano mwa mwezi wa Septemba mwaka huu, Serikali ya Rais Paul Kagame ilikuwa imeyafunga Madhehebu na Misikiti takribani 10,000 kwa kile ilichokiita kukiuka sheria za nchi hiyo
Naungamkono ...mimi natamani serikali zipige marufuku madhehebu ya dini zote tubaki na ukristo na uislamu usio wa madhebebu hivyo kuwe na nyumba chache za ibada zilizo hulia ambazo zitajengwa na serikali moja kila wilaya basi pia ipige marufuku shule za elimu dunia kuwa za kidini yaani kama mkristo akifungua shule hiyo shule iweshule tu siyo kwa mlengo wa dini ya mmiliki au dini ya dhehebu felani na kwa waislamu hivyo hivyo kwa sasa hadi fremason watafungua shule zao ya primary na secondary na kuzidi kuligawa taifa vibaya kupitia roho za watoto toka wadogo ....kumbukeni maandiko yanayo sema ufalme uliofarakana hauta simama .. serikali ipige marufuku vipindi na masomo ya dini kwenye shule zote za serikali na binafsi watoto wasomeshwe dini kwenye shule zisizo toa elimu.lasmi ya dunia
 
Ninacheka kama mazuri, Rwanda Makanisa yameacha kuhubiri habari za Yesu, sasa ni mwendo wa kuhubiri, amani na mshikamano. Kama Tanzania tu, sasa hivi, usiposifia chama na mama, watakusativa tu. Afrika bara letu...
 
Back
Top Bottom