Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

Kuamka mapema sio tatizo.. mradi wawahi kulala tuu
 
tengenezeni uchumi ambao familia inaweza ku-survive kwa kipato cha mzazi mmoja,. Inalazimika kufanya hivyo ili wazazi wao waweze kuwahi makazini
 
Wengine wanaona ujanja mtoto miaka miwili anaanza kupelekwa day care..principle yangu ni mtoto akae home awajue siblings, ajue viumbe vya dunia, atembee ahave fun, ajue milima mito na bahari, ajue abc -z akiwa home, 1 to 100 akiwa home.. alale, acheze, ale.

Nursery nataka asome mwaka mmoja tu..sitaki kuskia ya baby class, kg 1, kg 2, pre grade 1 ..Halaf baada ya hapo ndo agraduate aende class 1 lol..watu wanafanywa mtaji
Nani atamfundisha yote hayo?Kama mzazi unarudi saa tatu usiku.
 
Tunaendeshwa sana na Mentality.

Mtu anaishi Tabata anataka kumpeleka Mwanaye shule iko Mbezi Beach, kisa workmates wake wamepeleka watoto wao kule.

Kiufupi kuna ujinga mwingi sana unaendelea kwa habari ya haya mashule na Wazazi tumeupokea kama Mazombie.

Pia kuna hili suala la watoto Wa Madarasa ya mitihani kulazimishwa kukaa Bweni.
Hayo madarasa ya mitihani watoto wanarudi nyumbani saa moja
 
Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

Mwenye mtoto ndio mjinga, hili swala halihitaji time, Wala Cheti Cha ufaulu mtiahan wowote wa kitaifa kujua n sawa au sio sawa hata wangu tuu wa class 5 kuamka saa 11:30 aende Shule huo ujinga sifanyi nimewapa 15minutes za kujiandaa asubuh chai 5minutes saa 1:10 safari ya Shule ianze
 
Nani atamfundisha yote hayo?Kama mzazi unarudi saa tatu usiku.
mifumo ya kifamilia zetu zilizojaa wajomba mashangazi na kina bamdogo tumeziacha.. tupo radhi tuwe na mabeki tatu hata wawili ila sio kuweka ndugu wa kukaa nao ambao ndio walikua chachu ya watoto kujifunza michezo, elimu za awali na awareness ya ndugu..siwezi laumu sana
 
Watoto wanatia huruma, ila nawashauri wazazi kama wana nafasi, nibora wapeleke watoto wao wenyewe..
Binafsi mwaka wa tano huu nafanya kazi ya kuwapeleka na kuwachukua, na najisikia vizuri kama mama!! Kwani muda huo napata wasaa wa kupata yaliyojiri shuleni kwa siku hiyo!!
Mwanzoni rafiki zangu walisema sitaweza ni kazi ngumu, lakini sasa na wao wanafanya kama mimi!!
Ila kama wazazi mnatafutia kipato mbali, hapo ndo changamoto
 
Hakuna mateso mabaya kama haya mzazi unaamka saa 10 na wewe unajiandaa kumpeleka mtoto kituoni akasubiri basi.

Ndio ukute basi limeondoka utajuta maana madereva wengi wa basi za wanafunzi wajeuri sana.

Unakuta vimelaliana kwenye gari. Huu ni zaidi ya ukatili ni vyema tuboreshe shule zetu za kata.
Nakubaliana na wewe
 
Umesahau wana mabegi makubwa kama kilo 12 hivi kila mmoja.
 
Kuna mzazi mmoja ana vitoto viwili mmoja miaka 4 na mwingine miaka 2, anavisomesha "english medium school" ,vitoto saa 11 vipo road vinasubiri school bus, vikirudi jioni vinasinzia hadi haviwezi kutembea. Ada anawalipia milioni 3 kila mmoja!!

Sasa najiuliza yaani mtoto wa miaka 2 anakwenda shule kufanya nn na ada bado analipiwa 3M ?!!!
 
Sidhan Kama wazazi wa kaliba Hii wanalitambua hili,

Went mamlaka wanapaswa kuingilia Kati, Elimu imefanywa biashara wameacha kuzingatia utu na Haki za watoto.
Hakuna biashara inayolipa kwa kuanzisha shule...wanafunzi wa nurseries n primaries wanalipa ada zaidi ya tuition fee ya kozi za chuo kikuu cha dar es salaam.

Imagine shule ina wanafunzi 1000-2000 tu ...ada milioni 2.5-3...!!
 
Hawapitwii

Screenshot_20220304-085051.png
 
Its insanity 😡, wazazi wakiwa na maamuzi ya ovyo wanaoteseka ni watoto. Hapo mtoto anaamshwa saa kumi na moja ili aandaliwe alishwe yaani ni mateso matupu. Mie nilikosa mdada wa kazi nikaenda ki Day care kimoja eti wananiambia saa kumi na mbili na nusu mtoto awe tayari nikawaambia huo ujinga sifanyi alivyokosa haya ananijibu mbona hawa wote mama zao wanawapakia saa kumi na mbili nikawaambia ni hao mwalimu sio mimi. Nikapata nyingine ujinga huo huo eti watoto wa miaka 3 na miezi 3 saa kumi na mbili wawe tayari nikachomoa kabisa ikabidi tunagotiate kuwa wangu wawe wanafuatwa 7.20am ambao ndio muda ninaoenda kazini. Hebu tuwahurumie watoto wetu jamani
 
Ulifanya vizur Sana, wewe Ni mmojawapo wa wazazi Bora Sana. Bravo[emoji106]
 
Back
Top Bottom