Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Kuamka mapema sio tatizo.. mradi wawahi kulala tuu
 
tengenezeni uchumi ambao familia inaweza ku-survive kwa kipato cha mzazi mmoja,. Inalazimika kufanya hivyo ili wazazi wao waweze kuwahi makazini
 
Nani atamfundisha yote hayo?Kama mzazi unarudi saa tatu usiku.
 
Hayo madarasa ya mitihani watoto wanarudi nyumbani saa moja
 
Mwenye mtoto ndio mjinga, hili swala halihitaji time, Wala Cheti Cha ufaulu mtiahan wowote wa kitaifa kujua n sawa au sio sawa hata wangu tuu wa class 5 kuamka saa 11:30 aende Shule huo ujinga sifanyi nimewapa 15minutes za kujiandaa asubuh chai 5minutes saa 1:10 safari ya Shule ianze
 
Nani atamfundisha yote hayo?Kama mzazi unarudi saa tatu usiku.
mifumo ya kifamilia zetu zilizojaa wajomba mashangazi na kina bamdogo tumeziacha.. tupo radhi tuwe na mabeki tatu hata wawili ila sio kuweka ndugu wa kukaa nao ambao ndio walikua chachu ya watoto kujifunza michezo, elimu za awali na awareness ya ndugu..siwezi laumu sana
 
Watoto wanatia huruma, ila nawashauri wazazi kama wana nafasi, nibora wapeleke watoto wao wenyewe..
Binafsi mwaka wa tano huu nafanya kazi ya kuwapeleka na kuwachukua, na najisikia vizuri kama mama!! Kwani muda huo napata wasaa wa kupata yaliyojiri shuleni kwa siku hiyo!!
Mwanzoni rafiki zangu walisema sitaweza ni kazi ngumu, lakini sasa na wao wanafanya kama mimi!!
Ila kama wazazi mnatafutia kipato mbali, hapo ndo changamoto
 
Nakubaliana na wewe
 
Umesahau wana mabegi makubwa kama kilo 12 hivi kila mmoja.
 
Kuna mzazi mmoja ana vitoto viwili mmoja miaka 4 na mwingine miaka 2, anavisomesha "english medium school" ,vitoto saa 11 vipo road vinasubiri school bus, vikirudi jioni vinasinzia hadi haviwezi kutembea. Ada anawalipia milioni 3 kila mmoja!!

Sasa najiuliza yaani mtoto wa miaka 2 anakwenda shule kufanya nn na ada bado analipiwa 3M ?!!!
 
Sidhan Kama wazazi wa kaliba Hii wanalitambua hili,

Went mamlaka wanapaswa kuingilia Kati, Elimu imefanywa biashara wameacha kuzingatia utu na Haki za watoto.
Hakuna biashara inayolipa kwa kuanzisha shule...wanafunzi wa nurseries n primaries wanalipa ada zaidi ya tuition fee ya kozi za chuo kikuu cha dar es salaam.

Imagine shule ina wanafunzi 1000-2000 tu ...ada milioni 2.5-3...!!
 
Its insanity 😡, wazazi wakiwa na maamuzi ya ovyo wanaoteseka ni watoto. Hapo mtoto anaamshwa saa kumi na moja ili aandaliwe alishwe yaani ni mateso matupu. Mie nilikosa mdada wa kazi nikaenda ki Day care kimoja eti wananiambia saa kumi na mbili na nusu mtoto awe tayari nikawaambia huo ujinga sifanyi alivyokosa haya ananijibu mbona hawa wote mama zao wanawapakia saa kumi na mbili nikawaambia ni hao mwalimu sio mimi. Nikapata nyingine ujinga huo huo eti watoto wa miaka 3 na miezi 3 saa kumi na mbili wawe tayari nikachomoa kabisa ikabidi tunagotiate kuwa wangu wawe wanafuatwa 7.20am ambao ndio muda ninaoenda kazini. Hebu tuwahurumie watoto wetu jamani
 
Ulifanya vizur Sana, wewe Ni mmojawapo wa wazazi Bora Sana. Bravo[emoji106]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…