Mkuu usichanganye haya mambo maana utafikia hitimisho batili. Hakuna aliyetaka Nusrat kuendelea kubaki jela, na kila mtu anataka ubunge. Lakini unapokubali kuupata ubunge kwa kukiuka msimamo wa chama, hapo inakuwa umejijali binafsi. Huyo dada angeitikia wito wa kamati kuu utetezi wako ungekuwa na mashiko. Tusichanganye huyo dada kukaa jela, na kilichofanyika kwenye huo ubunge maana tunapoteza mantiki.
You are so smart and intelligent ndugu...
Ni kweli, Nusrat angefika mbele ya kamati na kusema tu kuwa, yeye alikuwa gerezani na hakujua lolote linaloendelea huku nje, wajumbe wa KK wangemwelewa vizuri na kirahisi sana...
Angeendelea kujitetea kwa kusema kuwa, alipoona anakuja kutolewa gerezani hakuwa na sababu kuanza kuhoji haya mambo yamekuaje. Kilichokuwa kichwani mwake kwa wakati huo ni kufurahia uhuru wake wa kutoka gerezani...
Na angeendelea kujitetea kwa kusema pia kuwa, alijiona ni mwenye bahati ya mtende kutoka gerezani na moja kwa moja kuukwaa ubunge...
Angejitetea hivi, nina hakika wajumbe wa KK wangemwelewa vizuri sana na asingekuwa kwenye adhabu hii ya jumla na wenzake...
Kwa upande mwingine Nusrat ni kweli anayo makosa yake, lakini yasiyo ya adhabu ya kufutiwa uanachama. Mf. kosa la kushawishiwa kutenda uasi kwa mamlaka na kukubali...
Kinyume chake, mtu hawezi kuwa na shaka yoyote kuwa, dada huyu anafuata mkumbo. Amedanganywa na akadanganyika na kwa hiyo kajiunga na Kundi la waasi bila yeye kupenda...!!