Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Nimeumia sana moyoni!
Ukitaka kuelewa ni jinsi gani hii SYNDROME ya kufaulisha kwa MAUMIVU YOYOTE YAWAYO kwa mtoto ilivyobebwa na wazazi vs walimu.

1: Jaribu kulieleza hilo siku ya kikao cha wazazi na walimu.

2: Eleza kwenye grupu la usafiri la watoto wa shule

Utaonekana wewe ni mpinga elimu na ufaulu wa watoto.
Ni ulemavu tumeshatwishwa wazazi na wizara iko kimya.

Pia, watoto wanatembea na mabegi utafikiri wanajifunza kuwa makuli. Mwishowe ni kesi za kutibu migongo ya vijana wadogo kuongezeka.

Vijana wanafikia kuona shule kama adhabu na hatujui ni kwa kiadi gani tunawaumiza ubongo na kutengeneza magonjwa ya afya ya akili vs mengine physical.
 
Kuna shida mahali kwenye mindsets za mtu mweusi!

Hao waliotuletea hii elimu wanasoma kwa ku relax sana na bado hadi leo hii ni wagunduzi hodari.

Sisi tulio ipokea elimu , tunasoma kwa kujitesa sana na hatuvumbui chochote
 
Nasemaga kila siku watanzania tukiletewa Jambo linakuwa letu kwelikweli kuliko hata wenye Jambo lao,Sasa hizo shule zimekuwa shule😅😅
 
Ni kawaida yetu watu weusi kujifanya ndio tunajua sana kupokea mapokeo kuliko walioleta, angalia dini!
Kuna shida mahali kwenye mindsets za mtu mweusi!!!
Hao waliotuletea hii elimu wanasoma kwa ku relax sana na bado hadi leo hii ni wagunduzi hodari
Sisi tulio ipokea elimu , tunasoma kwa kujitesa sana na hatuvumbui chochote
 
Tatizo linaanza kwenye kero za usafiri wa umma, uhaba wa barabara nyingi, uchache wa shule nyingi bora....hayo yakisharekebishwa, ndipo unapoweza kutupa lawama kwa mzazi
Wakati sisi wazazi tunasoma shule bora zilikuwa nyingi? Au ndo tulikuwa tunahesabu shule chache sana zilizokuwa chini ya usimamizi wa vyuo vya walimu?
Tumevurugwa tu kichwani kama jamii.
 
Dar ni mkoa wenye maisha ya taabu Kwa watu walio wengi, na maisha ya kifahari Kwa watu wachache
Uko sahihi.

Una matajiri wa kiwango cha juu.

Na una masikini wa kiwango cha chini zaidi.

Kuna ndugu yetu aliingia Dar miaka ya 2006, aliporudi kijijini akawa anatuhadithia hili, mimi halikuniingia akilini hadi na mimi nilipoingia mjini ndio nikathibitisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…