Saa ya Rais Samia yadaiwa kuwa na thamani ya Tsh. Milioni 111,601,22/=

Saa ya Rais Samia yadaiwa kuwa na thamani ya Tsh. Milioni 111,601,22/=

Mbona na nyie mnatia aibu?

Kila mtu anaulizia picha aliyovaa ina maana hiyo picha hapo juu hamuion?

Nyie vipofu? Mnaona kabisa picha ya saa imezungushiwa na peni nyekundu hapo kwenye mkono wake lakin bado mnaulizia picha
Mwanzo hakuweka wadau chini ndio wakamsaidia kuweka
 
Hii ndio athari ya kulelewa na Shemeji kwa hisani ya dada mtu! Unazijua hata gharama za ujenzi??
We kaa nyuma ya keyboard hapo.

Nyinyi ndio raia mwenye kiwango cha upumbavu ambao mafisadi wa nchi hii wanawahitaji, bila shaka ulitarajia kusikia kuwa kila darasa litagharimu 40M.

Kwa standard ya majengo ya madarasa kwa shule nyingi za kata hapa Tz, mimi nikipewa budget ya 11M kila boma la darasa, najenga vizuri tu.

Twende taratibu, nieleze darasa moja la shule za kata linahitaji vifaa gani ambavyo nikiwa na 11M haitoshi kulikamilisha?
 
Haha hii longines gold watch nikiweka bei iliyochukuliwa ntashambuliwa humu

Ova
Kama ni gold sawa, ila asieelewa thamani atabeza wengine wananununua za elfu 30 sasa ukitaja bei watakuita majina ya kila aina 😄
 
Hatutaki unafiki wa kujifanya raisi hana uwezo ilihali upo, raisi ni tajiri mpaka watoto na wajukuu huenda wakarithi huo utajiri, sasa asiishi kitajiri sababu nchi ina raia masikini? Ok, Nchi inawavuta bange hiì, raisi anatakiwa afanane na wananchi wake naye apulize mibange.
Kuna vijana wangapi wamenyimwa mikopo na loan board eti bajeti haitoshi, hapo hapo rais unatupia saa ya milioni mia na ushee......hii ni kejeli kwa watanzania.
 
Kwani marupurupu yake na mshahara wake hawezi nunua?.mnataka raisi avae casio ya kukonyeza?
Kuna designer watches nzuri kabisa ambazo hazivuki milioni moja, acha kujitoa fahamu......chukulia mfano kuna suti designer ambazo bei yake hata kama unanunua ulaya hazivuki milioni moja ya kitanzania, kwa hiyo kisa ni rais utaenda kutafuta suti ya milioni 100 ili uonekane tofauti sana na watanzania wengine, siyo?​
 
Kuna vijana wangapi wamenyimwa mikopo na loan board eti bajeti haitoshi, hapo hapo rais unatupia saa ya milioni mia na ushee......hii ni kejeli kwa watanzania.
Ndo uhalisia sio kejeli. Yaani raisi asipovaa hiyo saa ndo itahalalisha vijana kukosa mkopo? Tusipende unafiki, Yaani raisi ajifanye kuwa na yeye ni masikini wakati sio masikini. Uhalisia ni kuwa raisi si masikini, watoto wake si masikini, wajukuu si masikini. Kijana anayekosa mkopo chuo anatakiwa ajue hilo, iwe raisi kavaa cheni ya Billion au kavaa gunia.
 
Kuna watumishi wangapi wa umma ambao jumla ya mshahara wao kwa mwaka mzima unafika milioni mia moja?

Au tuseme mafao yao baada ya kustaafu wakilipwa kwa mkupuo kwa kikokotoo cha sasa yanafika milioni mia moja?

Imagine milioni mia ndo thamani ya saa ya mtumishi huyu wa umma, vipi mali nyingine........ni watumishi wangapi wa umma au watanzania wenye huo ukwasi wa kumudu kununua saa ya milioni mia moja kwa kutumia mshahara wao?
 
Kuna designer watches nzuri kabisa ambazo hazivuki milioni moja, acha kujitoa fahamu......chukulia mfano kuna suti designer ambazo bei yake hata kama unanunua ulaya hazivuki milioni moja ya kitanzania, kwa hiyo kisa ni rais utaenda kutafuta suti ya milioni 100 ili uonekane tofauti sana na watanzania wengine, siyo?​
Unampangia?
 
Back
Top Bottom