rukia16
JF-Expert Member
- Feb 27, 2020
- 2,977
- 30,973
Zilikua zangu hizo ila sijaacha nimepunguza tu.Sina hata hela nimezurura mjini vya kutosha nikiona kitu kizuri na ninajua kwamba bei yake imechangamka ,basi naulizia ilhali najua sina hata hela.. Hapo bei itapunguzwa hadi najuta kwa nini niliuliza na hela sina.tatizo wafanyabiashara wetu wa bongo ni wakarimu[emoji23] unaenda kuulizia kitu anataja bei unamwambia basi siku nyingine lakini yeye anazidi kukupunguzia tu bei.kuna siku jamaa alinipunguzia laki nzima kwenye fridge
Mimi: hii fridge bei gani ?
muuzaji: hii laki nne na nusu boss wangu
Mimi: oh basi nitarudi (huku naanza kuondoka)
muuzaji:boss nipe nne kamili (huku ananishika mkono)
mimi:hapana,parefu sana
Muuzaji:basi nipe tatu na nusu
Sent from my Redmi 8 using JamiiForums mobile app