Ninapodili na wewe na kukuamini inakubidi uwe makini sanaa la sivyo itakugharimu, natoa pesa zangu nyingi kuwekeza kwenye biashara yako na unapoteza umakini na ushahuri nakupa bure na unashindwa kuufanyia kazi narudia tena itakugharimu
Kila mtu mzuri ana ubaya wake hakuna mzuri wa 1 Kwa 1
Katika kesi ya hao jamaa hakuna la kumsaidia yeyote hapo kwani ni ndani na nje ya makubaliano ya biashara yao wenyewe ukiweka wazi juu ya uzembe wa jamaa aliyewekezewa pesa kwenye biashara yake na akaleta mzaha wa kumuamini kijana mwenzake kupelekea kupoteza kila kitu
Kikubwa, awe makini anapoinuka tena au anapoaminiwa na mtu mwingine kwa kuwekeza pesa kwako aongeze umakini zaidi asirudie kosa, na sikuona sababu yeyote ya kukubali kupewa au kukopeshwa pesa na huyo jamaa angeendelea na kazi yake ile ile ya MARKETING na ukusanyaji wa pesa ilikuwa inamtosha sana
Kuhusu jamaa kuchunguzwa na serikali ni jambo muhimu ila sio lenye manufaa sana WAFANYABIASHARA wana mambo mengi sana katika biashara zao haswa hao wafanyabiashara wakubwa
Kukwepa kodi kama sio kukimbia kabsa,hiyo kusafirisha pesa, kuexchange pesa ,kudhulumu na kudhulumiana kuhusu umafia kwa wenye pesa ni kawaida sanaa
Lazima ujilinde kana kwamba mtu asikuzoee zoee kwenye mambo yako yaani mtu asiingilie plan zako akaziharibu ikitokea mtu anataka kuingilia mipango yako na kuiharibu unatakiwa umpotezee mbali sana asionekane hata dalili ikitokea watataka kumtafuta
Kuna vijana sita walipotea kariakoo wauza simu mwaka juzi kama nna kumbu kumbu vizuri na mpaka sasa hakuna taarifa ya kupatikana na vyombo vilitangaza Kama walikamatwa na police na walipelekwa mpaka kituoni na mpaka sasa hakuna taarifa yeyote kuhusu wao, so ni mambo hayo hayo tu ya kudhulumiana na kupotezana
Be careful unapodili na mtu anayejiweza yaani wanakuwa mahesabu yao kupata na sio kupoteza hasara inaweza ikawa ya kibinaadamu lakini yeye akaona kama umeisababisha kwa makusudi - kama Tajiri umekutana nae tu juu kwa juu na akataka mfanye biashara inabidi uwe makini sana ila kama unafahamiana siku nyingi mnaweza mkafanya kitu na kikaenda vizuri
Asantum