Saalah (Silent Ocean): Anavyotakatisha na kutorosha pesa nchini, Uhujumu Uchumi, Kuteka na Kutesa watu, anavyolindwa na viongozi

Saalah (Silent Ocean): Anavyotakatisha na kutorosha pesa nchini, Uhujumu Uchumi, Kuteka na Kutesa watu, anavyolindwa na viongozi

Kama mtu anaweza kufanya unyama huu wa Kutesa watu ofisini kwake,wizi na kudhulumu watu,uhujumu uchumi na Uchafu wote huu,Hivi tuna usalama wa taifa wanaojielewa kweli?Tuna polisi kweli?
IGP anapaswa kubaki kwenye nafaasi take kweli?

Mheahimiwa Raisi, kwakuwa juzi umesema huwa unapitia hapa Jamii Forums,chukua hatua juu ya hili.

Hili ni tukio moja tu,Je amefanya mangapi ambayo hatujui?
Ukipitia ule Uzi wa kwanza utaona jinsi watu walivyofunguka juu ya Uhuni wa huyu mtu,mpaka analawiti watu?

Tunaaubiri tuone hatua gani utachukua.

Mleta Mada Mungu akulinde.
Hilo la kumlawiti kijana wa KitZ kisa katembea na dada yao limenichanganya akili kabisa, yaaani ulawiti, jamani?! Hawa watu wavuliwe uraia ikiwezekana, watafute nchi ya kwenda kufanyiana ulawiti, this is too much!!
 
Uko sahihi kaka. Haya ni machache sana kati ya mengi makubwa sana. Hata mbolea zinaingizwa na hawa Watanzania wenye asili ya Asia. Ukigusa kuleta mbolea kwa bei nafuu wanakuua.

Hivi sasa wanatamba kuwa wamepata mtelezo kwa Mama Samia.

Kwa kuwa anapitia humu tuone hatua anayoweza kuchukua.

Kama anawalinda aendelee kuwalinda.

Ni Tanzania pekee unalala masikini kesho unanunua nyumba Masaki na hakuna anayekuuliza umepata wapi hizo pesa.

Mifumo ikiwa mibovu uchumi hauwezi kukua.
Mungu wangu!!! My Goood!!
 
Na apitie na kuonyesha uamiri jeshi wake.

Sio kuunda Tume ya Haki jinai ili kuhalalisha wahujumu uchumi waliotaifishiwa mali zao walizokwiba serikalini warejeshewe. Wahujumu uchumi walichukuliwa hatua toka enzi za Mwalimu Nyerere.

Anyway hata wakituma majini sasa nitakufa kwa amani maana kamwe sitaishi milele.

Ukweli una gharama sana.
Hebu refusha uzi kidogo hasa hapo kwenye mbolea, kumbe ndio maana maisha yetu yataendelea kuwa maguku hata kwenye basic needs kama chakula, yaani wanaondoa competition kwa kutishiwa wapinzani KIFO??!!!
 
Ninapodili na wewe na kukuamini inakubidi uwe makini sanaa la sivyo itakugharimu, natoa pesa zangu nyingi kuwekeza kwenye biashara yako na unapoteza umakini na ushahuri nakupa bure na unashindwa kuufanyia kazi narudia tena itakugharimu

Kila mtu mzuri ana ubaya wake hakuna mzuri wa 1 Kwa 1

Katika kesi ya hao jamaa hakuna la kumsaidia yeyote hapo kwani ni ndani na nje ya makubaliano ya biashara yao wenyewe ukiweka wazi juu ya uzembe wa jamaa aliyewekezewa pesa kwenye biashara yake na akaleta mzaha wa kumuamini kijana mwenzake kupelekea kupoteza kila kitu

Kikubwa, awe makini anapoinuka tena au anapoaminiwa na mtu mwingine kwa kuwekeza pesa kwako aongeze umakini zaidi asirudie kosa, na sikuona sababu yeyote ya kukubali kupewa au kukopeshwa pesa na huyo jamaa angeendelea na kazi yake ile ile ya MARKETING na ukusanyaji wa pesa ilikuwa inamtosha sana

Kuhusu jamaa kuchunguzwa na serikali ni jambo muhimu ila sio lenye manufaa sana WAFANYABIASHARA wana mambo mengi sana katika biashara zao haswa hao wafanyabiashara wakubwa

Kukwepa kodi kama sio kukimbia kabsa,hiyo kusafirisha pesa, kuexchange pesa ,kudhulumu na kudhulumiana kuhusu umafia kwa wenye pesa ni kawaida sanaa

Lazima ujilinde kana kwamba mtu asikuzoee zoee kwenye mambo yako yaani mtu asiingilie plan zako akaziharibu ikitokea mtu anataka kuingilia mipango yako na kuiharibu unatakiwa umpotezee mbali sana asionekane hata dalili ikitokea watataka kumtafuta

Kuna vijana sita walipotea kariakoo wauza simu mwaka juzi kama nna kumbu kumbu vizuri na mpaka sasa hakuna taarifa ya kupatikana na vyombo vilitangaza Kama walikamatwa na police na walipelekwa mpaka kituoni na mpaka sasa hakuna taarifa yeyote kuhusu wao, so ni mambo hayo hayo tu ya kudhulumiana na kupotezana

Be careful unapodili na mtu anayejiweza yaani wanakuwa mahesabu yao kupata na sio kupoteza hasara inaweza ikawa ya kibinaadamu lakini yeye akaona kama umeisababisha kwa makusudi - kama Tajiri umekutana nae tu juu kwa juu na akataka mfanye biashara inabidi uwe makini sana ila kama unafahamiana siku nyingi mnaweza mkafanya kitu na kikaenda vizuri

Asantum
Sasa nini maana ya kuwepo kwa vyombo vya sheria kama kila kitu unatumia uninja?

Tatizo hawa matajiri wanatumia silaha kubwa sana kudili na watu ambao wanajua kabisa hawana uwezo wa ku fight back.

Kama una power serikalini why uanze kuhangaika na kumtesa mtu mpaka uathiri maumbile yake ashindwe ku-erect?

Hawa matajiri ni miyeyusho sana halafu umafia huu huwezi kumkuta anamfanyia mkubwa mwenzake kwasababu anajua tu hata ukim time bado ana backup ambayo itakuja kumlipia revenge at any time at any cost.
 
naona kwenye uzi huu baada ya kuujua ukweli, akili imekukaa sawa japo kwenye ule uzi wa awali wa mleta mada, ulijaribu kuleta hoja za kichawa kumtetea salah.
Ule Uzi ulikuwa hauna details mm sio mtu wa kupaparikia mambo angetakiwa alete hivi sio kutishia nyau. Maana hakukuwa na sababu za kuleta vitisho.

Ila details hizi ndio zinazofaa kuchangia
 
Bado naendelea kusema ,akija mtu na habar yake ichunguzeni kwanza kabla ya kuconlude na kufanya maamuzi.
Sisi wengine tunajaji kupitia scenario hiyo ilivyoelezwa na kukemea ukatiri huo.

Kama ameongopa, hilo ni juu yake ila mimi nimepokea hilo kama funzo na ujumbe kama fictional characters wanavyotumika kufikisha ujumbe
 
Nilichomkubali mwandishi hakutaka kuficha uovu ambao uliofanywa kutoka upande ulio athirika na huyo Boss

Angekuwa mtu mwingine ili kuifanya story iwe convincing asingeweza kuandika negative upande ambao anautetea
Yah,Afande kanyoosha maelezo,nami nilipenda nijue chanzo.Nasikitika kijana kwa aliyoyapitia,huruma tu itokee walau arudishiwe kianzio.
 
Masikitiko hatunae jpm. Wale hawakuelewa aliposema utawala wake tajiri anaweza kufanywa lolote ni matajiri kama huyu salaah. Chini ya samia hawa wanaweza mfafanya raia yoyote wa kawaida lolote.
Tuombe mungu utawala huu uweze kumkomesha salaah.
Mi naona hawa mbwa wana mizizi inayo run deep hadi ikulu, hata Rais hana la kuwafanya hawa wahuni, na akikaza shingo ataondoka yeye, hapa ndipo tunamkumbuka mwamba, Jiwe, JPM
 
Ila pia sisi Waafrika tujifunze uaminifu mzizi wa huu ugomvi uko kwa huyu kijana Pius.Haikuwa vizuri kumwibia Eliud na pia kwa Salah ni vyema ukafanya haki kumpa Eliud anachostahili maana ni haki yake chukka chako mrudishie chake
Uaminifu ni kitu ambacho sisi tumekuwa tukifeli

Mtaani kuna dogo anakibanda cha makuti anauza utumbo wa ng'ombe kipo eneo moja na parking ya bodaboda

Huyo dogo nimemshuhudia mara kibao akiwasaidia hao madereva bodaboda kuwapa utumbo for free na kuwachangia unga wawe wanapika kijiweni.

Lakini juzi dogo kaacha simu kwenye kibanda akaongozana na mteja kwenda kuomba chenji dukani.

Anarudi anashangaa simu haipo, kila bodaboda aliyekuwa pale akiulizwa anakataa anasema sio mimi.

Kumbe wao ndio wamechukua simu halafu wakawa wanataka dogo awape 15K ndio wamrudishie.

Dogo ikabidi atoe hiyo 15K kwasababu ndio simu anayotegemea kufanya request ya mzigo kwenye biashara yake.

Mtaji wa biashara hata 40K haufiki, fikiria faida ni kiasi gani halafu muda huo 15K imetolewa nje ya hesabu ku-rescue simu.

Baada ya siku mbili kupita Brother mmoja ndio alijitokeza kuwakemea wale bodaboda na kunyang'anya simu ya mmoja wao na kusema hairudishi mpaka wamrudishie dogo 15K yake.

Ndio hapo wakairudisha 15K
 
Mengine yote nimefuta ili nukuu isiwe ndefu. Hapo ulipoelekeza ofisi za silent ocean zilipo napenda kuuliza kidogo kwa kuwa hiyo mitaa naifahamu sana kupita maelezo.

1) Umeandika zilipo ofisi za silent ocean ni "Mkabala na...", nijuavyo, Mkabala na jengo la CCM ni Shule ya Mnazi Mmoja, unamaanisha kiwanja cha shule ya Mnazi Mooja ndiyo kimeuzwa? Maana nilisikia licha ya Mnazi MMoja Primary School pia kwenye hivyo viwanja vya shule pia imejengwa Sekondari. Tafadhali fafanua.

2) Au kama hukumaanisha "mkabala" kwa maana ya kutazamana (opposite), Je, ulimaanisha pembeni ya jengo la CCM?

Shule ya mnazi mmoja ipo upande wa pili wa barabara ya lami. Ni lazima uvuke bara bara ya lami ndio ufike shule ya msingi mnazi mmoja kama unatokea ccm lumumba
 
Back
Top Bottom